Makapuku Forum

Makapuku Forum

ZABURI 150

1.Haleluya ,msifuni Mungu katika patakatifu pake,Msifuni katika anga la uweza wake.
2.Msifuni kwa matendo yake makuu,Msifuni kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3.Msifuni kwa mvumo wa baragumu ;Msifuni kwa kinanda na kinubi.
4.Msifuni kwa matari na kucheza,Msifuni kwa zeze na filimbi.
5.Msifuni kwa matoazi yaliayo;Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6.Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.HALELUYA

TUOMBE

BABA katika jina la Yesu asante kwa Upendo wako mkuu kwetu hata kutuamsha salama na wazima.
Tunajikabidhi mikononi mwako utulinde utuongoze utuponye.
Tunaomba utuepushe na hatari mbalimbali na ajali mbalimbali.
Tunakushukuru,Tunakusifu,aTunakuabudu,Tunakushukuru na kwa Pumzi zetu tunalisifu jina lako daima HALELUYA.
Asante Baba kwa yote unayotutendea maana hatuna namna ya kuyaeleza tunashukuru.
Ponya wagonjwa,wafiwa,waliovunjika moyo,yatima wajane. usiwapungukie Mfalme wa Amani.Walinde wasafiri nchi kavu,majini angani wafike salama
Asante Baba na tunaomba ufanye yote sawasawa na mapenzi yako.
JUMAPILI YA LEO BABA TUNAOMBA TUKUTANE NAWE POPOTE TULIPO.
Tunaomba yote katika jina la Yesu amen.

JUMAPILI NJEMA WAPENDWA
Ameen mama mchuchu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom