Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki ni Kujitafakari

Habari za kutwa nzima na sasa uziku umeingia Makapuku wenzangu. Ni imani yangu kuwa umekuwa na wikend zuri na sasa ni mwisho wa wikend. Binafsi nimekuwa na weekend nzuri, nashukuru sana.

Nimekaa namsubiri Sweetiepie alete ngoma maana alisema Jumamosi na Jumapili atazimilik yeye (au ni mimi ni sikujihoji alikuwa anaongelea jmosi na jpili zipi? Maana hakuweka tarehe yaani ni kama SHIMBA YA BUYENZE na ahadi yake ya 'stupid criminals).

Wakati tunaendelea kuwasubiri hawa wadau basi nikaona si vibaya tukapata nyuzi kidogo za gitaa kutoka kwa wadonoaji mahiri. Na leo tunaenda USA na tunamkuta Gillian Welch.

Nilipomsikia mara ya kwanza nikadhani ninamsikiza Alison Krauss lakini mara nilipoona video clip yake nikajua niliongeza sukari kwenye asali.

Gillian anajua kulipiga gitaa na anavyolipakata huwezi amini kama gitaa lake lina nyuzi sita tu na shanga zake shingoni. Nyimbo zake kama alivyo Alison Krauss ambaye huimba na Robert Plant, yeye huimba na mpiga gitaa mwingine anayejua kwa jina la David Rawlings.
Na namna anavyolipiga gitaa lake hakyanani masikio yako yasipotabasamu basi inabidi umuone dakitari wa meno.
Keshashinda tuzo kadhaa ikiwemo ya Grammy.

Hebu tumwangalie hapa akicharaza gitaa katika Elvis Presley Blues. bhbb



Shunie , sijui kwanini silipendi jina mkuu, ukipona kikamilifu nitakujuza kwanini silipendi.

mzee wa saa mpya


binamu mm nitaanza kukuita mkuu
 
beec9e14c46f56f15c53ef907bb2c8e9.jpg
Chaplin kwenye ubora wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom