Makapuku Forum

Makapuku Forum

Ndo mambo yko hayo msukuma
Mambo ya kawaida. Lakini ni lazima nikiri tu. Msambwanda wa ukweli ukipita aisee inahitaji juhudi za makusudi kutoangalia hata kwa kuibia ibia. Sijui ndo udhaifu na dhambi zenyewe. Nilishawahi kumuuliza hata mchungaji kuhusu hili kama ni dhambi. Jibu alilonipa ni siri yangu. Napambana kuacha lakini ni ngumu. Pengine ndo maana tukaambiwa jicho likikukosesha ni bora tu uling'oe kwa sababu ni bora kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na chongo au ukiwa kipofu kabisa kuliko kwenda motoni na macho yote mawili.

Mama Mchungaji njoo utoe ufafanuzi kuhusu hili. Ati vijana marijali wafanyeje ili wasigeuke kutazama mavaiburesheni ya misambwanda mabinti wakikatiza? Ni dhambi kufanya hivyo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom