
ZABURI 116
1.Haleluya,Nampenda BWANA kwa kuwa anansikiliza sauti yangu na dua zangu.
2.Kwa maana amenitegea sikio lake,Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
3.Kamba za mauti zilinizunguka,Shida za kuzimu zilinipata,Naliona tabu na huzuni.
4.Nikaliita jina la BWANA ,Ee BWANA ,nakuomba sana ,uniokoe nafsi yangu.
5.BWANA ni mwenye neema na haki,Naam ,Mungu wetu ni mwenye rehema.
6.BWANA huwalinda wasio na hila,Nalidhilika akaniokoa.
7.Ee nafsi yangu urudi rahani mwako,Kwakuwa BWANA amekutendea ukarimu.
8.Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,Macho yangu na machozi Na miguu kuanguka
9.Nitaenenda mbele za BWANA katika nchi ya waliohai.
10.Naliamini ,kwa maana nitasema Mimi naliteswa sana
11 Mimi nalisema kwa haraka yangu wanadamu wote ni waongo
12 Nimrudishie BWANA nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?
13 Nitaipokea kikombe cha wokovu;Na kulitangaza jina la BWANA,
14 .Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,Naam ,mbele za watu wake wote.
15.Ina thamani machoni pa BWANA mauti ya wacha Mungu wake
16 Ee BWANA ,hakika mimi ni mtumishi wako,Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako,umevifungua vifungo vyangu .
17.Nitakutolea dhabihu ya kushukuru ;Na kulitangaza jina la BWANA.
18.Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA ,Naam ,mbele ya watu wake wote.
19.Katika nyua za nyumba ya BWANA ,ndani yako ,Ee Yerusalemu.
Wapendwa nashukuru sana Mungu ameniponya ,nawashukuru kwaupendo, maombi na kunijali haikua rahisi ila Mungu amenitendea makuu kwa maombi yenu.
MBARIKIWE SANA SANA,NAWAPENDA MUWE NA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO