Makapuku Forum

NUKUU YA LEO

The first World Cup I remember was in the 1950 when I was 9 or 10 years old. My father was a soccer player, and there was a big party, and when Brazil lost to Uruguay, I saw my father crying.

Kombe la Dunia la kwanza nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1950 nikiwa na miaka 9 au 10. Baba yangu alikuwa mwanasoka na kulikuwa na sherehe kubwa, na Brazil ilipofungwa na Uruguay nilimuona Baba yangu akilia


Hayo ni maneno yaliyopatwa kutamkwa na mwanasoka wa Brazil Edson Arantes do Nascimento almaarufu kama PELE.

Pele alizaliwa 23/10/1940 katika mji mdogo wa minas Girais na kukulia ktk jiji la Sao Paulo.

Mwaka 1999 Pele alipigiwa kura ya kuwa mchezaji bora wa karne ya 20.

Pele amefunga magoli 1281 katika michezo yote 1363 aliyocheza ktk maisha yake ya soka.

Pele anashika nafasi ya pili kwa ufungaji wa magoli katika maisha ya soka akiwa nyuma ya mbrazil mwenzie Arthur Friedenreich aliyefunga magoli 1329 katika michezo 1239.

Kuna mengi sana kuhusu pele..lakini baba yake mzazi alilia machozi baada ya Brazili kupokea kipigo cha goli 2 kwa 1 toka kwa uruguay na inakuwa mara ya kwanza uruguay kuchukua kombe hilo baada ya Vita ya pili ya dunia.


Brazil wanakunywa mpira, Brazil wanakula mpira,
Brazil wanavaa mpira,
Brazil wanaishi mpira,
Brazil wanapenda mpira.

 
Hii kitu imewachanganya sana wanasayansi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…