Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nazi zake ziko je? Tui lake je? Unaweza kuhisi tofauti yo yote (ladha, ubora, thamani...) kati ya nazi iliyochukua miaka mi3 na ile iliyochukua miaka 15?
Ziko tofauti sana unaweza tumia moja ya miaka kumi na tano lkini tatu za miaka mitatu kwa mboga ileile,kwa biashara naona inawasaidia
 
Amen,nimeumia sana leo ila Mungu anazidi kunitia nguvu
Walighushi vyeti au walitumia majina ya watu wengine kusoma? Kughushi vyeti ni kosa lakini kama umenunua jina la mtu mwingine (kama enzi zile kurudia darasa la 7 hairuhusiwi) halafu kwenda kusoma kweli ukasoma wewe ukahenyeka mpaka ukamaliza na maarifa ukapata kwa maoni yangu usomi wako ni halali kwa sababu uliyesoma ni wewe na siyo jina. Bashite anaandamwa kwa sababu hakusoma/hakufaulu form IV. Huyu ana kesi ya kujibu.

Kuna daktari mmoja bingwa pale Muhimbili namfahamu alifeli darasa la saba akanunua jina la mtu mwingine huyooo akasoma mpaka Muhimbili hadi Cambridge UK kwenye specialization ya magonjwa ya akina mama (Gynecology). Leo hii ukimtoa kwa sababu eti alitumia jina la mtu mwingine ni uonevu kwa sababu aliyesoma na mwenye maarifa ni yeye na siyo jina. Hawa waliokumbwa na masaibu haya ya kutimuliwa kazini sijui wanaangukia kundi gani.

Kama umeghushi cheti cha udaktari, ualimu, unesi hata ulinzi halafu hukusomea na huna maarifa hayo kusema kweli umefanya kosa la jinai na ukifurushwa usilalamike!

Pole sana mtumishi. Mungu Atawafungulia milango mingine!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom