Makapuku Forum


Neno
"Dikteta" wamelipachika Wamarekani tu....namfahamu zaidi Bikteta Ceorge W Bush
........
Kweli hakuna haki hapa duniani. Leo nchi yote imeparaganyika. Na bado wakafanya lile lile kwa Gaddafi. Jamaa wala hawajifunzi kutokana na makosa yao. Hata hayo mafuta waliyokuwa wanayatafuta hawajaweza kuyapata. Wameishia kuharibu nchi na kuua mamilioni ya watu bure.
 
Ila "madikteta" mara nyingi huwa na mwisho mbaya sana kihistoria na vinginevyo sijui kwa nini. Kuna documentary moja hapa ya Hitler na jinsi alivyomtumia huyu jamaa kivita ilinishangaza sana.
 
Ndio yeye mkuu
KK is also an intellectual. Nilihudhuria warsha yake moja na nilifurahishwa sana na uwezo wake wa kujenga hoja mpaka maprofesa wakawa wanamshangaa. First generation ya viongozi wa Afrika ambayo haitasahaulika. Angalau walikuwa na idea walichotaka kufanya na japo hawakufanikiwa lakini angalau walijaribu na malengo yao na falsafa zao za kitaifa zilikuwa wazi. Siyo kama sasa hata haijulikani kinachoendelea...
 
Hapo talaka ingehusika
 
List ya nchi 5 zilizotumia fedha nyingi kwa ajili ya majeshi 2016

Inaelezwa kuwa sifa ya nchi yoyote ni uwezo wa Jeshi lake katika kujilinda na kupambana kwa ajili ya wananchi ambapo tumekuwa tukishuhudia gharama inayotumika kuhakikisha Idara hiyo inaimarika kwa kulipa mishahara minono na kununua vifaa vya kisasa.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm ‘SIPRI’ zimetajwa nchi 5 zinazotumia fedha nyingi zaidi kwa ajili ya Jeshi hadi kufikia 2016 zikiongozwa na Marekani.

SIPRI imesema kuwa matumizi ya dunia katika majeshi yaliongezeka hadi Dollar 1.7 trillion mwaka 2016 ambapo Marekani inasalia kinara kwa kutumia fedha nyingi kwenye jeshi mwaka 2016 ambapo matumizi yameongezeka kwa 1.7% kuifanya ifikishe Dollar 611 billion.

China ilitumia Dollar 215 billion na kuifanya kukamata katika nafasi ya pili huku Urusi ikikamata nafasi ya tatu ikitumia Dollar 69.2 billion. Saudi Arabia inakamata nafasi ya nne ikitumia Dollar 63.7 billion na India katika nafasi ya tano ikitumia Dollar 55.9 billion.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…