Makapuku Forum

Makapuku Forum

2004 - Marekani yaiondolea vikwazo Libya baada ya miaka 18 na kurudisha mahusiano yao upya.
e42dd703b328b0cec617e1283e2a1ab5.jpg
USA wanafiki sana halafu baadaye wakaja kumuua Caddafi
Wazee wa maslahi
....
 
1962 - Stuart Pearce anazaliwa.

Ni beki wa zamani wa England.

Mmoja kati ya mabeki wa shoka waliokuwa wanacheza kibabe enzi zake.

Aliwahi pia kuwa kocha wa Man city na Timu ya Taifa ya England chini ya miaka 21.
6229bf95622d764a133099e819abe082.jpg
0e0553fbc314fbbbb8823c2637a6208e.jpg
Siku hizi EPL kumejaa akina Merteseker na John Stones(Jiwe linalobonyea km mkate)
.....
 
NUKUU YA LEO

Those who fight corruption should be clean themselves

Watu wanaopambana na Rushwa wanapaswa kuwa wasafi
990451bfe4f5c65643e2884454e6b173.jpg

Hayo yalipata kutamkwa na Rais was wa sasa wa Russia Bw. Vladimir vladimirovich Putin aliezaliwa 7/10/1952 katika jiji la Sait Petersburg nchini Russia.

Kitaaluma Putin ni mwanasheria na alihitimu shahada ya sheria chuo kikuu cha Sait petersburg mwaka 1975.

Putin alikuwa ni afisa usalama wa Russia Komitet Gosudarstvennoj Bezopasnosti (KGB) kwa miaka 16 .

Amefanya kazi kama afisa usalama wa kimataifa, majukumu yake mengi yalikuwa ni ya kushughulika na nchi za kigeni..

Mwaka 1991 Putin alianza siasa Rasmi akiwa na cheo cha luteni Kanali wa KGB.

Putin amekuwa Waziri mkuu na Rais wa Russia kwa nyakati 2 tofauti kwa kila cheo..
f6c5243f35e54844cbce937177df85f9.jpg
eed1f5ea18707078864c4dd90bbdb1a0.jpg
02216a1eac9f0a92547b05dd1094c24b.jpg

Uongozi wake wa kwanza mwaka 2000-2008 ulikuza uchumi wa Urusi na kuongeza purchasing power kwa 72%


Putin anaamini Rushwa ni adui wa haki, ukipigana kuondoa Rushwa lazima uwe msafi kwanza.

Putin anafahamika kwa uongozi makini huku akitaka Urusi iwe taifa lenye nguvu zaidi duniani japo ukweli unabaki kuwa marekani ataendelea kuleta changamoto kwa urusi .

Hata Tanzania tukitaka kupambana na Rushwa, basi wale tunapambana nayo tuwe na mikono safi..


Gooodmorning.
 
KINYWA CHAKO KIJAZWE NINI ILI KUMTUKUZA MUNGU NAKUWATIA MOYO WENGINE

ZABURI 71:8

Kinywa changu kitajazwa sifa zako,Na heshima yako mchana kutwa.

Tunapoianza siku mpya na wiki mpya hebu vinywa vyetu vijazwe furaha,upendo,uponyaji tunene maneno ya kuinuana na kumsifu Mungu kila wakati.

Tuwe waponyaji ,wafariji,watia moyo tukitamani kuona kila mtu anafurahia uumbaji na anauishi upendo...

Haijalishi unapitia changamoto gani..mahali hapa pawe faraja na nafasi ya kujiona kuwa unayosababu ya kuendelea kuwepo na kufurahia baraka tele Mungu anazotujalia

Vinywa vyetu vijazwe sifa na heshima kwa Mungu Baba ili duniani pawe mahali pazuri pa kuishi na kuwasaidia wengine wajisikie vizuri.



Tunakushukuru Mungu kutufikisha umbali huu hakika wewe ni Ebenezer,

Umetutoa mbali na hujawahi kutuacha wakiwa.

Asante kwa siku ya leo na wiki inayoanza leo tembea pamoja nasi.

Tunaomba kibali chako katika kila jambo tutakalotenda,Tupe kauli njema,tupe Roho ya Upendo,na kunyenyekea mbele zako.

Tuweke mbali na kuonewa,magonjwa,chuki,mikosi,hila na ajali mbaya.

Tupe ujasiri Amani na Imani katika Kristo Yesu kupitia jina la Yesu Mpatanishi na Mwokozi wetu Amen


WIKI NJEMA
KAZI NJEMA
JUMATATU NJEMA
MBARIKIWE
Amen Mama Mchu
 
Kila kitu kina umuhimu
Mfano mabaki ya chakula hutumika kulishia mifugo ndo ilovyo pia kwenye ishu zetu
Ingekuwa stori za mapenzi haziruhusiwi thread isingeweza kufika ilipofika
Thread hii haichoshi sababu ina vitu mchanganyiko tofauti na thread zingine
Pia hata waokota makopo mitaani wana umuhimu maana husaidia kusafisha mazingira
.........
Na wavuvi wa kambale kuna wakati huvua hata Nyoka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom