TAFUTA KUWA NA AMANI NA WATU WOTE

MITHALI 25
21 Adui yako akiwa ananjaa ,mpe chakula;Tena akiwa anakiu ,mpe maji ya kunywa.
22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake;Na Bwana atakupa thawabu.

Katika suala gumu maishani moja wapo ni hili la kuwapenda maadui zetu,Lakini ndivyo ilivyo hata kwa Bwana Yesu alisema wasamehe maana hawajui watendalo.

Mtu akikukosea Mwambie Bwana Teta nao wanaoteta nami........Zaburi 35 ..................... usiwe na hasira ya kudumu.
Katika somo hili unapompenda na kumtendea mema adui

Bwana atakupa thawabu.

Utakuwa umemsaidia yeye kubadilika pia

Ni adhabu tosha maana neno lasema utakuwa umewasha makaa ya moto kichwani mwake.

Wapendwa siyo kazi nyepesi ila kwa msaada wa Roho Mtakatifu inawezekana.
Tunakushukuru Baba kwa ulinzi wako na kutuamsha salama ,asante kwa yote unayotutendea asante kwa afya ,riziki ,marafiki na maadui tunaomba uendelee kutuimarisha tuweze kuwa na uvumilivu wa kuwapenda maadui na kuwaombea.
Siku ya leo ponya roho zetu,ponya majeraha,ponya wafiwa,wagonjwa ,wenye mahitaji..
Tufundishe kuchukuliana mizigo kwa upendo na kuwa sababu ya furaha kwa wengine na kuwasaidia watu kubadilika na kutenda kadri wanavyopenda kutendewa
Asante Baba kwa sababu utatupa kushinda kila siku za maisha yetu na kutujenga kuimarishana maana hakuna mkamilifu.
Jumapili ya leo ikawe ya baraka ushindi na kutubdilisha.
Kwa jina la Yesu Mpatanishi na Mwokozi wetu Amen
WAPENDWA JUMAPILI NJEMA