MWANDISHI:Habari yako mzee, kwani Ng'ombe wako huwa unawalisha nini?

MZEE:Ng'ombe yupi unamuulizia,? Mweupe au mweusi?

MWANDISHI:Mweupe.
MZEE:Huyo namlisha majani.



MWANDISHI:Na mweusi!!!?

MZEE:Namlisha majani pia.
MWANDISHI:Umeanza kufuga lini hawa Ng'ombe wako?

MZEE:Ng'ombe yupi unamuulizia? Mweupe au mweusi?
MWANDISHI: Mweupe.

MZEE:Huyo nimeanza mwaka jana.
MWANDISHI:Na Mweusi!!!?
MZEE:Mwakajana pia.
MWANDISHI:Hivi Ng'ombe wako huwa wanalala wapi?

MZEE:Ng'ombe yupi mweupe au mweusi?
MWANDISHI:Mweupe.
MZEE:Analala hapo kwenye boma.
MWANDISHI:Na mweusi analala wapi!!?

MZEE:Analala kwenye boma pia.
MWANDISHI:Kwanini nikikuuliza kuhusu Ng'ombe wako naww unaniuliza mweupe au mweusi alafu unatoa majibu sawa????

MZEE:Kwasababu Ng'ombe mweupe ndo wakwangu.
MWANDISHI:Enhe! Na huyo mweusi ni wanani??
MZEE:Ni wangu pia.





