Madenge. Mambo mengine ni kuyapotezea tu. Huyu dogo naye atakuja na kwenda. Walikuwepo akina Lyatonga Mrema na hii impromptu justice wakivuma sana mpaka kuundiwa cheo kisichokuwepo cha naibu Waziri Mkuu. Walifika wapi? Kuna kitu kinachotaka kufanywa na kikikamilika basi utaona mambo yanapoa menyewe. Matamko mangapi alishatoa lakini hakuna hata moja lililofanikiwa?
Suala hili la sasa ni tete sana na dunia nzima linawakunisha vichwa na kamwe halitamalizwa kwa kiki za kisiasa, ajenda za siri na michezo angamizi isiyofuata utaratibu wala mihimili ya kisheria . Mimi namuunga mkono sana na kijamii naona amefanikiwa kuwasha moto japo ni wa mabua. Ngoja pepo zivume sasa na dhoruba za wahusika zimshukie ndo utaona. Jipe muda na kamwe kabisa kabisa usimwamini mwanasiasa hata kama ni dingi wako!