Makapuku Forum

Mi hii serikali tayar imeshanipa stress vya kutosha sijui wananitafuta nini mimi. Mambo yakiwa sawa ntahitaji mwanasaikolojia anisaidie
 
Mbaya zaidi waliotoa zile fedha za misaada ni wafanya biashara hao hao ambao wamewabana mwaka huu....Mungu anawaonyesha kwamba riziki ya mtu haizuiliwi na yeyote yule hata iweje.
Sasa ndo itabidi huyo mkulu aishushe ile kodi ya kule bandarini kama awali jamaa waendelee kuleta mizigo yao kupitia pale
 
Kama kuna jambo serikali hii ya 5 inataka kukosea ni kujaribu kuwaziba watu midomo.
Mwanadamu kwa asili ikiwa ameumia sana moyoni mwake na akapata mtu wa kumsimulia huwa anatoa nyongo na uchungu huisha. LAKINI MTU akiwa ameumia na ukamziba mdomo, na ukaja kumuumiza kwa mara nyingine, nyongo yake ikipasuka hali ya hewa itachafuka.
Naishauri serikali hii iwaache watu waropoke watoe ya moyoni huo ni usalama kwa taifa.
Vinginevyo wanatengeneza bomu la kuwaangamiza watawala.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…