Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230621_061649_Opera%20Mini.jpg
 
Mambo usiyo yajua kuhusu chombo kilichopotea baharini kikiwa na mabilionea ..!
Chombo hicho kinaitwa Titan, kinamilikiwa na kampuni ya Ocean Gate, mmiliki wa chombo hicho Bwana Stockton Rush ni mmojawapo wa watu waliokuwemo.

Chombo hicho hakikuwa na leseni wala hakuna mamlaka yoyote ya serikali au binafsi inayohusika na udhibiti ilikuwa imedhinisha matumizi ya chombo hicho. Watengenezaji wa chombo hicho wanadai kwamba teknolojia iliyotumika kutengeneza chombo hicho ilikuwa ya juu sana hali iliyofanya mamlaka kushindwa kukielewa kinafanyaje kazi.

Kabla ya abiria kusafiri ni lazima asaini fomu na kukubaliana na masharti yanayoeleza kwamba chombo hicho hakijasajiliwa matumizi yake yanaweza kusababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.

Abiria wanapoingia ndani ya chombo kinafungwa kwa nje. Abiria au nahodha hawana uwezo wa kufungua chombo kwa ndani.

Chombo kina uwezo wa kutoa Oxygen kwa muda wa masaa 76.. mpaka sasa yamebaki chini ya masaa 5 Oxygen ya chombo hicho kuisha. Binadamu hana uwezo wa kuishi bila Oxygen kwa muda usiozidi dakika 5...!
Screenshot_20230622_124221_Instagram.jpg
 
Mpaka muda huu Oxygen itakuwa imekwisha, matarajio ya kuwapata bado wakiwa hai sasa ni kudra za Mwenyezi Mungu..

Bado juhudi za kuwatafuta wahanga waliopotea na chombo wakielekea kuangalia mabaki ya meli ya Titanic iliyozama miaka mingi huko nyuma zinaendelea katika bahari ya Atlantic.

Matumaini ya kuwapata wahanga bado wakiwa hai yamepungua kutoka na muda wa chombo hicho kutunza Oxygen kuwa imekwisha...ni vigumu sana binadamu kuendelea kuwa hai bila Oxygen...!
Screenshot_20230622_193608_Instagram%20Lite.jpg
 
"Chombo kitakuwa kimelipuka"
Taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita na kikosi cha wanamaji wanaohusika na utafutaji wa chombo kilichopotea inaelezwa kwamba mabaki ya chombo hicho yamepatikana kwa sakafu ya bahari karibu kabisa na yalipo mabaki ya meli ya Titanic.

Mabaki yaliyopatikana ni sehemu ya mfuniko wa nyuma pamoja na cover mbele la chombo hicho.

Mvumbuzi mwenza wa chombo hicho ameeleza vyombo vya habari kwamba mabaki haya yanaonyesha kwamba chombo hicho kitakuwa kimezidiwa na mgandamizo wa bahari na hivyo kulipuka.

Hakuna taarifa zozote za kupatikana miili ya watu watano waliokuwa kwenye chombo hicho...!
Screenshot_20230622_215252_Instagram.jpg
 
"Miili haitapatikana"
Kiongozi wa Kikosi cha Wanamaji anayesimamia zoezi la uokoaji amewaambia waandishi wa habari kwamba abiria wote waliokuwa kwenye chombo cha Titan wamefariki na huenda miili ya marehemu hao isipitakane kabisa.

Pia kiongozi huyo amesema kwamba mabaki mengine matano ya chombo hicho yamepatikana.

Kiongozi huyo ameeleza kwamba mazingira yalipokutwa mabaki ni ya hatari sana. Kiongozi huyo amesema idadi ya waokozi itaanza kupunguzwa kutoka eneo hilo baada ya masaa 24 kwa sababu eneo hilo ni hatari sana kwa maisha ya watu.

Pichani ndio abiria waliokuwa kwenye chombo hicho. Abiria mmoja alikuwa analipa nauli inayokadiriwa kufikia Shilingi Milioni 600..!
Screenshot_20230623_065240_Instagram.jpg
Screenshot_20230623_065306_Instagram.jpg
Screenshot_20230623_065328_Instagram.jpg
Screenshot_20230623_065359_Instagram.jpg
 
Bilionea Last born alikuwa amepanga kuja kupanda Mlima Kilimanjaro.

Bwana David Mearns amesema kwamba walipokutana kwa mara ya kwanza na Hamish Harding walipanga kufanya safari kuja Afrika kupanda Mlima Kilimanjaro.

Bwana David ameiambia BBC kwamba alikuwa hajui kama rafiki yake huyo ni bilionea kwa sababu alikuwa mtu mcheshi sana na mwenye matani mengi na mara zote alikuwa anapenda kujaribu vitu vipya.

'Alikuwa mtu wa watu'. Hamish Harding ni raia wa Uingereza, alikuwa ni mmiliki wa kampuni la kuuza ndege la Action Aviation lenye makao makuu Dubai.

Hamish Harding ameacha mke na watoto wanne, wawili wakiwa watoto wa kambo..!
Screenshot_20230623_065610_Instagram.jpg
 
"Miili haitapatikana"
Kiongozi wa Kikosi cha Wanamaji anayesimamia zoezi la uokoaji amewaambia waandishi wa habari kwamba abiria wote waliokuwa kwenye chombo cha Titan wamefariki na huenda miili ya marehemu hao isipitakane kabisa.

Pia kiongozi huyo amesema kwamba mabaki mengine matano ya chombo hicho yamepatikana.

Kiongozi huyo ameeleza kwamba mazingira yalipokutwa mabaki ni ya hatari sana. Kiongozi huyo amesema idadi ya waokozi itaanza kupunguzwa kutoka eneo hilo baada ya masaa 24 kwa sababu eneo hilo ni hatari sana kwa maisha ya watu.

Pichani ndio abiria waliokuwa kwenye chombo hicho. Abiria mmoja alikuwa analipa nauli inayokadiriwa kufikia Shilingi Milioni 600..!View attachment 2665945View attachment 2665946View attachment 2665947View attachment 2665948
R.I.P matés 😢😢
 
Suleman alikuwa anaogopa, lakini alikwenda ili amfurahishe Baba yake..!

Shangazi yake Suleman Dawood, kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikuwa kwenye chombo kilicholipuka baharini na kuuwa abiria wote waliokuwemo amesema kijana huyo alikuwa anasitasita sana kupanda chombo hicho ili kwenda kuona mabaki ya meli Titanic.

Akizungumza na NBC News, Azmeh Dawood, dada mkubwa wa Shahzada, alisema Suleman alimwambia jamaa yao mmoja kwamba alikuwa "anaogopa sana" kusafari, lakini alimua kwenda ili kumfurahisha baba yake.

Wataalamu wa mambo ya bahari wanasema kwa mgandamizo ulioko chini ya habari kabla abaria hawajua kuna tatizo tayari walikuwa wameisha kufa, kifo katika mazingira hayo kinatokea haraka sana kama kukokoroga kahawa kwenye maji...!
Screenshot_20230623_122348_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom