Makapuku Forum

Makapuku Forum

NEYMAR AMWOMBA RADHI HADHARANI MPENZI WAKE
.
Wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Supastaa wa Kibrazili, Neymar ameweka kando ugumu wote na kuomba radhi hadharani akimtaka mpenzi wake ambaye ni mjamzito, mrembo Bruna Biancardi amsamehe huku akisisitiza: “Nimefanya makosa.”
.
Staa huyo wa PSG, Neymar, 31, na Biancardi, 29, walithibitisha Aprili mwaka huu kwamba wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Hata hivyo, taarifa hizo ambazo Neymar alizitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram alipoweka picha yake na ya mpenzi wake, inaonekana kumtibua mrembo Bruna, kwa sababu hakutaka mambo ya ujauzito wake ujulikane hadharani na jambo linalomfanya Neymar kuomba radhi ili asimpoteze mrembo wa maisha yake.
.
Staa huyo wa zamani wa Barcelona alisema: “Bru, nafanya hivyo kwa ajili yako na familia yako. Hebu jaribu kufikiria. Hakuna haja ya kuendeleza matatizo, tunakuhitaji sana kwenye maisha yetu. “Nimeona namna gani nilivyokuanika, najua ni jinsi gani hukupendezwa na hilo, lakini naona wazi jinsi ninavyokuhitaji uwe karibu yangu. Nipo pamoja nawe. Nimefanya makosa. Nimekosea sana.
.
“Nathubutu kusema nimekuwa nikikosea kila siku, ndani na nje ya uwanja. Lakini, makosa yangu binafsi ninayofanya nyumbani, namalizana nayo kwa ubinafsi huohuo na familia yangu na marafiki… “Lakini, hii imemhusu mtu spesho sana katika maisha yangu. Mwanamke ambaye nimekuwa na ndoto za kuwa naye karibu, mama wa mtoto wangu. Niliikosea familia yako, ambayo ni familia yangu pia. Niliingilia mambo yako binafsi katika kipindi hiki ambacho ungehitaji usiri mkubwa.”
.
Neymar aliendelea: “Bru, nimeshaomba radhi kwa makosa yangu, kwa kukutangaza bila ya sababu ya msingi, lakini najiona nalazimika kulieleza hili hadharani. Kama vitu binafsi viliwekwa hadharani, basi hata msamaha uombwe hadharani. Sipati picha maisha bila ya wewe. Nakupenda.”

Screenshot_20230624_064725_Instagram.jpg
 
Ukiniuliza mchezaj wangu bora basi nitakutajia Fiston (Mayele) Yanga tulipata bahati kubwa kuwa na Mayele ni mchezaji mwenye kiu ya mafanikio anafunga na kuipagania timu.
.
Kuna wakati zilikuja Ofa za Fiston nilikuwa sehemu ya kuzuia asiuzwe kwa kuwa sio kila wakati utapata bahati ya kumpata mchezaji kama yeye sokoni, watu wajiulize ni lini walimkosa Fiston uwanjani?

jibu litakuwa rahisi ni pale alipoumia, wapo wachezaji waliowahi kudanganya wanaumwa ili wasicheze lakini sio Fiston. Anaweza kubaki Yanga lakini itategemea uongozi utazungumza naye vipi.” Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nabi [Mwanaspoti]
Screenshot_20230624_064859_Instagram.jpg
 
“Kama kuna mchezaji aliyenishangaza juu ya kipaji chake basi ni Dickson Job, wakati nafika na nilipoambiwa anacheza beki wa kati nilisubiri kuona ana kitu gani cha ziada lakini alinijibu kwa vitendo uwanjani, huyu ni kijana mdogo ambaye ana akili kubwa sana anapokuwa uwanjani, Job hajui kukataa jukumu unalomtuma amekuwa ni rahisi kwake kubadilika wakati wote kocha ukimtaka kufanya hivyo, ana nidhamu kubwa ni sawa na wale rafikizake Kibwana (Shomary) na mwanangu Mshery bahati mbaya aliumia lakini ni kipa mzuri, kwa Job ni bahati mbaya sana anacheza soka Tanzania.” - Aliyekuwa Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi [viaMwanaspoti]
Screenshot_20230624_065000_Instagram.jpg
 
YANGA baada ya kung’oa mtukutu Bernard Morrison sasa wako kwenye mazungumzo ya mwisho kushusha chuma kutoka Union Maniema winga Maxi Mpia Nzengeli (23) ambae ni mtu wa kazi lakini pia mkwanja wake wataumudu.
.
Maxi ambaye ni nahodha wa Maniema anasifika kwa kasi huku akiwa kwenye kikosi cha DR Congo kilochoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa mdani CHAN.

Screenshot_20230624_065406_Instagram.jpg
 
Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Esther Noah wa Shule ya Sekondari Pandahili aliyepotea May 18, 2023 amepatikana katika chumba cha kupanga cha Mama Abdul kilichopo maeneo ya Ifisi Mbalizi Mkoani Mbeya na imebainika kuwa alipelekwa hapo na muuza mkaa aitwaye Baba Jose na kusema ni Mke wake hivyo anaomba hifadhi baada ya siku mbili angemchukua ili wakaishi wote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amesema Baba Jose baada ya kukaa na Mtoto huyo kwa muda alienda kumpeleka kwa Mama Abdul na kuahidi kwenda kumchukua siku atayapota chumba Ili wakaendelee kuishi pamoja.

Akiongea ofisini kwake ambako Binti huyo amepelekwa akiwa na Mama yake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa rai kwa Walimu wa Pandahill kupunguza kasi ya kuchapa viboko Wanafunzi kwani ni miongoni mwa sababu inayoelezwa kuchangia Mtoto kukimbia Shule

Homera amesema vipimo vyote vya kiafya vimefanyika na Ester hana ujauzito na hivyo ataendelea kukaa na Maafisa ustawi wa jamii ili kumsaidia kumpa ushauri wa kisaikolojia arudi Shule, na Mwanaume huyo atasakwa mpaka akamatwe.

Amesema amepimwa pia kipimo cha mimba Ili kujua hali yake na majibu yameonyesha hana mimba na kwa siku zijazo akibainika ana mimba watampa nafasi ya kwenda kujifungua na kurudi Shule.
View attachment 2666925

Tobaa
 
.
ANAENDA: KYLE Walker bado hajakata tamaa ya katika mpango wake wa kutaka kujiunga na Bayern Munich na mazingumzo kuhusu uhamisho wake bado yanaendelea kwa mujibu wa ripoti.
.
Kocha wa Bayern, Thomas Tuchel anataka huduma ya beki huyo wa kimataifa wa England kwa mujibu waripoti. Ilielezwa Walker alichukizwa kuwekwa benchi na kocha wake Pep Guardiola kwenye fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan.

Screenshot_20230624_082241_Instagram.jpg
 
.
HAKIELEWEKI: Mohamed Salah huenda akatimkia Saudi Arabia baada ya Liverpool kushindwa kufuzu michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Moja ya klabu kutoa Saudi Arabia inavutiwa na fowadi huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 31. Hata hivyo Jurgen Klopp alikana taarifa hizo kwamba staa huyo hana mpango wa kuondoka dirisha hili la usajili la kiangazi.

Mwishoni mwa msimu uliopita Salah alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu

Screenshot_20230624_082351_Instagram.jpg
 
NKETIAH PRESHA JUU KISA HAVERTZ
.
Eddie Nketiah ameingiwa na hofu kuhusu hatima yake ndani ya Arsenal kutokana na ujio wa Kai Havertz, SKY SPORTS wamefichua.
.
Nketiah 24, alikuwa sehemu ya kikosi cha Mikel Arteta msimu uliopita baada ya Gabriel Jesus kukaa nje kwa muda mrefu alipoumia goti.
.
Nketiah alifunga mabao nane na kutengeneza asisti tatu katika mechi 39 alizocheza msimu uliopita. Lini baada ya Arsenal kumsajili Havertz, fowadi huyo amepata presha anaweza kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza msimu ujao.
.
Sasa timu kama West Ham, Crystal Palace na Fulham zinafumfuatilia na chochote kitakachotokea kuhusu hatima ya Nketiah basi watapigana vikumbo kuwania saini yake.

Screenshot_20230624_082504_Instagram.jpg
 
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anaamini kuwa kiungo wa Uingereza Declan Rice, 24, ndiye nahodha wa baadaye wa klabu hiyo na The Gunners wanajiandaa kuwasilisha ofa ya tatu hivi karibuni na mahitaji mengine ya West Ham. (Mail)

Rice bado ana nia ya kujiunga na Arsenal licha ya Manchester City kuonyesha nia ya kujiunga na kinyang'anyiro hicho na washindi wa Treble pia kuweza kukidhi bei ya £100m. (Guardian)

Screenshot_20230624_082928_Instagram.jpg
 
Manchester United wameafikiana na Chelsea kuhusu dili la la kumsajili kiungo wa Uingereza Mason Mount, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akikaribia kununuliwa kwa pauni milioni 60. (Mirror)
Screenshot_20230624_083036_Instagram.jpg
 
Borussia Dortmund wanapanga kutoa kitita cha pauni milioni 13 kumnunua kiungo kinda wa kati wa Manchester United na Tunisia Hannibal Mejbri, 20, ambaye msimu uliopita alichezea Birmingham kwa mkopo . (Manchester Evening News)

Screenshot_20230624_083123_Instagram.jpg
 
Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Esther Noah wa Shule ya Sekondari Pandahili aliyepotea May 18, 2023 amepatikana katika chumba cha kupanga cha Mama Abdul kilichopo maeneo ya Ifisi Mbalizi Mkoani Mbeya na imebainika kuwa alipelekwa hapo na muuza mkaa aitwaye Baba Jose na kusema ni Mke wake hivyo anaomba hifadhi baada ya siku mbili angemchukua ili wakaishi wote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amesema Baba Jose baada ya kukaa na Mtoto huyo kwa muda alienda kumpeleka kwa Mama Abdul na kuahidi kwenda kumchukua siku atayapota chumba Ili wakaendelee kuishi pamoja.

Akiongea ofisini kwake ambako Binti huyo amepelekwa akiwa na Mama yake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa rai kwa Walimu wa Pandahill kupunguza kasi ya kuchapa viboko Wanafunzi kwani ni miongoni mwa sababu inayoelezwa kuchangia Mtoto kukimbia Shule

Homera amesema vipimo vyote vya kiafya vimefanyika na Ester hana ujauzito na hivyo ataendelea kukaa na Maafisa ustawi wa jamii ili kumsaidia kumpa ushauri wa kisaikolojia arudi Shule, na Mwanaume huyo atasakwa mpaka akamatwe.

Amesema amepimwa pia kipimo cha mimba Ili kujua hali yake na majibu yameonyesha hana mimba na kwa siku zijazo akibainika ana mimba watampa nafasi ya kwenda kujifungua na kurudi Shule.
View attachment 2666925
Mmmmh baba Jose

Ila kuna jambo linafichwa kuhusu huyu mtoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom