Makapuku Forum

Makapuku Forum

THANK YOU! VICTOR AKPAN
.
OFFICIAL: Uongozi wa Simba SC umetangaza kufikia Makubaliano ya kuachana na kiungo mkabaji Victor Akpan raia wa Nigeria
Screenshot_20230620_143335_Instagram.jpg
 
TAARIFA zilizonifikia Julai 15, kikosi cha Simba kitaondoka nchini kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi (Pre season) ya msimu ujao ambayo itakuwa si chini ya wiki mbili.
Screenshot_20230620_143450_Instagram.jpg
 
SABABU SAIDO KUTEMWA HII
.
Timu ya taifa ya Burundi itakuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10:00 jioni kucheza kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Namibia huku ikimkosa nahodha Saidi Ntibazonki 'Saido' aliyepewa mapumziko.
.
Licha ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu huu akicheka na nyavu mara 17 na asisti 12, Saido hatakuwa uwanjani kutokana na kupewa mapumziko ya kimkakati.
.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya
Burundi, Ettiene Ndayiragije alisema amemuacha kutokana na kucheza mechi nyingi msimu huu akiwa na Simba na Geita, hivyo kumpa muda wa kupumzika kwani kuna mechi nyingi zijazo zitakazohitaji awepo zile za klabu yake ya Simba.
Screenshot_20230620_143551_Instagram.jpg
 
THANK YOU! HELMY GUELDICH
.
Nipo hapa kuthibitisha Kocha wa viungo, Helmy Gueldich anaondoka Yanga baada ya kumaliza mkataba.
.
Kaizer Chiefs na Orlando Pirates ni miongoni mwa vilabu vilivyoweka Ofa kubwa kunasa saini yake.
Screenshot_20230620_143726_Instagram.jpg
 
.
KIUNGO wa PSG, Marco Verratti anatajwa kuwa ni staa mwingine ambaye huenda akatimkia Saudi Arabia ambapo ripoti zinadai kuna timu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili lakini kuna uwezekano mkubwa akajiunga na Al-Hilal.
.
Staa huyu ambaye mkataba wake na PSG unamalizika 2026, ameshawishika kuondoka kutokana na ofa kubwa iliyopo.

Screenshot_20230620_143823_Instagram.jpg
 
.
TAYARI straika wa Chelsea, Kai Havertz, 24, amefikia hatua za mwisho na huenda akasaini mkataba wa kuichezea Arsenal wakati wowote kuanzia sasa licha ya kwamba Bayern Munich imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.
.
Nyota huyo aliomba kuondoka kikosini tangu msimu uliopita wa usajili, lakini hakufanikiwa. Havertz ambaye mkataba wake na Chelsea unamalizika 2025, msimu uliopita alicheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao tisa.

……………..
Screenshot_20230620_143920_Instagram.jpg
 
.
AWAGOMEA:: Fowadi wa Arsenal, Folarin Balogun amegomea kutolewa tena kwa mkopo msimu ujao na kuhitaji kupigwa bei jumla kama mambo yataendelea kuwa magumu kwa upande wake kupata nafasi katika kikosi cha kwanza huko Emirates.
.
Balogun alitolewa kwa mkopo Middlesbrough kabla ya mkopo mwingine huko Reims, ambako alitamba msimu uliopita na kufunga mabao 21 kwenye Ligue 1 na kushika namba nne kwa mabao kwenye ligi hiyo.
Screenshot_20230620_144021_Instagram.jpg
 
ANASAKWA
.
PARIS Saint-Germain inaripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kabisa za kumalizana na Kocha Luis Enrique kwa ajili ya kumpa dili la kwenda kuinoa timu yao.
.
Mabingwa hao wa Ligue 1 waliachana na Christophe Galtier mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kushindwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa wanahitaji kocha atakayewafanya kuwa na nguvu kwenye michuano hiyo ya Ulaya kwa msimu ujao.

Screenshot_20230620_144220_Instagram.jpg
 
STAA WA UHOLANZI JELA
.
Nyota wa zamani wa Ajax, Quincy Promes amefungwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kumdunga kisu binamu yake kwenye tafrija ya familia. Mholanzi huyo amehukumiwa kifungo cha miezi 18 kwa kosa la unyanyasaji, tukio hilo lilitokea mwaka 2020 baada ya mabishano kuzuka kati ya Promes na binamu yake. Chanzo cha mabishano hayo ni kutokana na mkufu kuibiwa.
.
Awali Promes alikuwa akikabiliwa na kesi ya kutaka kumuua binamu yake hata hivyo, kesi hiyo ilitupiliwa mbali, sasa Promes amepatikana na hatia ya kumshambulia binamu yake na atalipa faini Pauni 6000.
.
Aidha Promes alikanusha mashtaka hayo lakini mahakama ikatumia ushahidi kutoka kwa watu wawili walioshuhudia tukio hilo pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu ya Promes na kumkamata nyota huyo anayekipiga Spartak Moscow.
.
Inadaiwa Promes alikuwa na nia ya kumpiga kisu binamu yake shingoni, huku winga huyo akimuonya kwamba ana bahati kwa sababu hakubeba bunduki. Promes, mwenye umri wa miaka 31, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, huku ripoti zikidai adhabu yake ingepunguzwa endapo angehudhuria kesi hiyo inayomkabili.
.
Mchezaji huyo wa zamani wa Sevilla kwa sasa yuko Moscow na taarifa zimeripoti ana mipango ya kuomba uraia wa Russia, hiyo inamaanisha kwamba anaweza kuepuka jela nyumbani kwao Uholanzi. Promes anatarajiwa kufikishwa tena mahakamani mwaka huu kwa kosa la kuingiza dawa za kulevya baada ya kutuhumiwa ana shehena mbili za madawa ya kulevya aina ya ‘Cocaine’ mwaka 2020.
Screenshot_20230620_144310_Instagram.jpg
 
MARCUS Rashford atakuwa mchezaji anayelipwa mkwanja mrefu zaidi Manchester United atakaposaini mkataba mpya kwani mazungumzo yamefikia hatua nzuri.

Straika huyo wa kimataifa wa England atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 375,000 (Sh 896milioni) kwa wiki huku David de Gea akipunguzwa mshahara.

Kwa sasa Rashford anapokea mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki katika mkataba wake unaomalizika mwezi huu, lakini mabosi wa Man United wanataka kukitumia kipengele cha kumuongeza miezi 12 kilichopo katika mkataba wake huo.

Kwa upande wa De Gea alikuwa akipokea mshahara wa Pauni 375,000 ambao Rashford anaandaliwa kulipwa endapo atasaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Old Trafford.

Screenshot_20230620_144452_Instagram.jpg
 
Golikipa wa Young Africans Djigui Diarra jana ameitumikia timu yake ya Taifa ya Mali kwa dakika zote 90 wakati ikivaana na CONGO kwenye mchezo wa kufuzu AFCON 2023

FT: CONGO Mali

CLEAN SHEET.
PRE-ASSIST/ KEY PASS

Screenshot_20230620_144550_Instagram.jpg
 
Benki Kuu ya Tanzani imeukumbusha umma kuwa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaelekeza kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusia kutumika nchini, hivyo hakuna Mtu au Kampuni yoyote inayoruhusiwa kuikataa kwa malipo yoyote halali na kwamba kitendo cha kukataa malipo kwa shilingi ya Tanzania ni kuvunja Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuukumbusha umma kwamba Serikali ilishatoa tamko kuhusu katazo la matumizi ya fedha za kigeni kwa Wakaazi wa Tanzania katika kulipia bidhaa na huduma nchini, tamko la kwanza lilitolewa mwezi Agosti 2007 na la pili mwezi Desemba 2017”

“Hata hivyo, katika siku za karibuni imebainika kuwepo kwa ukiukwaji wa tamko hilo, hivyo Benki Kuu inapenda kuukumbusha umma kwamba maagizo yaliyotolewa hapo awali kuhusu matumizi ya fedha za kigeni yanapaswa kuendelea kuzingatiwa kuwa bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania, bei hizi zinajumuisha kodi za kupangisha ardhi, nyumba na ofisi, gharama za elimu, huduma za afya, vifaa tiba na vitendanishi, gharama za usafiri, lojistiki za bandari, vifaa vya kielektroniki na huduma za mitandao ya mawasiliano”

“Bei ambazo walengwa wake Wakuu ni Watalii au Wateja wasio Wakaazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni, bei hizi zinajumuisha gharama za hoteli, usafiri, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa Wageni, usafirishaji kwenda Nchi za nje kupitia Tanzania na gharama za mizigo bandarini”
Screenshot_20230620_144709_Instagram.jpg
 
Hiki Chombo kimepotea baharini jana. Kilikuwa na matajiri wa Uingereza na kilikuwa kinawapeleka kuona mabaki ya meli ya Titanic iliyozama miaka 111 iliyopita.

Chombo hiki kilikuwa na watu watano, miongoni mwao ni bilionea Hamish Harding.

Licha ya utajiri wake Hamish Harding amekuwa akicheza michezo ya hatari sana kama wafanyavyo malast born ikiwemo kukaa muda mrefu zaidi kwenye sehemu ya kina kirefu zaidi cha bahari hapa duniani.

Watu wengine waliokuwemo kwenye chombo hicho ni tajiri mwingine kutoka Uingereza bwana Shahzada Dawood aliyekuwa na mtoto wake.

Watu wanauwezo wa kukaa siku 3 wakiwa hai kwenye hicho Chombo cha Kampuni ya Ocean gate vinginevyo wanapoteza maisha kwa sababu kina uwezo wa kutunza Oxygen kwa siku 3 tu.

Kwa sasa mabaki ya meli ya Titanic yako kwenye kina cha mita 3962 katika bahari ya Atlantic. Ili kusafiri na chombo hicho kwenda kuona mabaki ya Titanic mtu mmoja analipa nauli ya Shilingi Milioni 600.

Pichani ndie Bilionea Hamish Harding mwenye michezo ya hatari kama last born.. Ana umri wa miaka 48.

Bilionea huyu anashikilia rekodi tatu za Guinness kutokana na hiyo michezo yake ya hatari.

Pia anashikilia rekodi ya binadamu wa kwanza kuizunguka dunia kwa spidi kubwa zaidi..!!
Screenshot_20230620_150934_Instagram.jpg
Screenshot_20230620_151000_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom