Makapuku Forum

Makapuku Forum

Badala ya kucheza mechi za kirafiki wakati wa kalenda ya FIFA, UEFA wao waliamua kuanzisha mashindano [UEFA Nations League].

Mwanzoni mashindano hayo yalilalamikiwa na wachezaji kwa kuona kama UEFA wameamua tu kutengeneza chanzo cha mapato huku wao wakiendelea kutumika kama nyenzo.

Kicha ya kupigwa vita mwanzoni lakini kwa sasa mashindano ya UEFA Nations League yanakua na yale mataifa makubwa yameanza kuweka nguvu na kuyapa thamani mashindano.

Spain ni bingwa wa tatu wa UEFA Nations League, bingwa wa kwanza alikuwa Ureno [2018|19] bingwa pili Ufaransa [2021|21] na bingwa wa tatu Spain [2022|23].

Kwa hiyo UEFA Nations League ni mashindano makubwa yanayotoa platform kwa timu za Ulaya na kuzijenga, timu bora zinaonekana.
Screenshot_20230619_152038_Instagram.jpg
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amewataka Wanawake wa kitanzania kuwa makini kutokana na Wanaume Raia wa kigeni kubuni mbinu mpya ya kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Wanawake wa kitanzania zaidi ya mmoja na kuficha dawa za kulevya kwenye makazi ya Wanawake hao huku wao wakipanga nyumba tofauti na pale dawa zikimamatwa huwakana Wanawake hao.

Akiongea leo Dar es salaam amesema “Kutokana na udhibiti kuwa mkubwa, Wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameendelea kubuni mbinu mpya za usafirishaji wa dawa za kulevya ili kukwepa kukamatwa, Mamlaka imebaini mbinu hizo na kuchukua hatua, mbinu mojawapo inayotumika ni Raia wa kigeni mmoja kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Wanake wa kitanzania zaidi ya mmoja na kuficha dawa za kulevya kwenye makazi ya Wanawake hao huku wao wakipanga nyumba tofauti na wanakoishi Wapenzi wao”

“Hali hii husababisha Wanawake wa kitanzania kuingia kwenye matatizo makubwa ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria huku Wanaume wakiwakana Wanawake hao, Mamlaka imejipanga kikamilifu kupambana na biashara ya dawa za kulevya hivyo wanaojihusisha au wenye mpango wa kujihusisha na biashara hiyo waache mara moja au wajisalimishe wenyewe kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria”

“Wananchi wanapaswa pia kuwa makini na mizigo wanayopewa kubeba au kuhifadhi pasipo kujua ndani yake kuna nini, Wanawake wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani katika baadhi ya matukio wamekuwa wakitumiwa na Wapenzi wao hasa Raia wa kigeni kusafirisha na kupokea mizigo wasiyoijua na wakati mwingine mizigo hiyo huwa na dawa za kulevya na hivyo hujikuta matatani”
Screenshot_20230620_055511_Instagram.jpg
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama imefanya operesheni katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Arusha na kufanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 200.5.

Akiongea leo Dar es salaam, Lyimo amesema “Tumekamata pia bangi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978, bangi mbichi gunia 5,465, bangi iliyosindikwa (skanka) kilogramu 1.5, methamphetamine gramu 531.43, heroin kete 3,878, cocaine kete 138, mililita 3,840 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine pamoja na kuteketeza ekari 1,093 za mashamba ya bangi”

“Aidha, kwa kushirikiana na Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (INCB) Mamlaka imezuia kuingia nchini jumla ya kilogramu 1,507.46 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya”

“Ukamataji huo uliofanyika kuanzia tarehe 25 Machi, 2023 hadi tarehe 19 Juni, 2023 unahusisha Watumiaji 109 wakiwemo Raia watatu wa kigeni, baadhi ya Watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani na wengine wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika”
Screenshot_20230620_055655_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imesema imepokea taarifa na pia kuthibitisha uwepo wa baadhi ya watoa huduma wa mabasi yanayokwenda Mikoani kucheza na mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi na kusababisha kusafiri kwa mwendokasi kwa lengo la kufanya mashindano ya kufika wa kwanza kwenye vituo/stendi za mabasi hivyo imefuta ratiba za mabasi 9 yaendayo Mikoani yanayoanza safari saa 9 alfajiri.

“Watoa huduma hao wanatumia pia fursa iliyotolewa ya kuanza safari mapema (saa 9 - saa 11 alfajiri) na kufanikisha azma ya kufanya mashindano na kufika wa kwanza kwenye vituo, takribani wiki mbili sasa, kumekuwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mabasi ya Ally's Star, Katarama Express na Ismamilo yakishindana kufika katika vituo vya mabasi, basi lililoshinda lilimwagiwa maji na kushangiliwa”

“Hapana shaka na waliobashiri litawahi walipata ushindi kwenye Kamari waliyoicheza kinyume na taratibu, LATRA kwa kuzingatia jukumu lake la kukuza usalama wa sekta zinazodhibitiwa ikiwa ni pamoja na usalama wa watumiaji wa huduma za sekta zinazodhibitiwa haiwezi kuacha matendo haya hatari yenye kuhatarisha usalama na maisha ya wat pamoja na mali zichezewa bila kuchukua hatua”

“Hivyo, kutokana na hali hii na kwakuwa watoa huduma Ally's Star na Katarama Express wameendelea kukiuka Sheria, kanuni na taratibu hata baada ya kupatiwa elimu na maonyo kadhaa, kwa kuzingatia mamlaka tuliyonayo, tumefuta ratiba zote za mabasi tisa yanayoanza safari zao kuanzia saa 9.00 alfajiri, mabasi hayo ni sita ya Ally's Star (T946 EBF, T947 EBF, T948 EBF, T354 DXS, T357 DXS a T360 DXS) na matatu (3) na Katarama Express (T835 EBR, T836 EBR, T212 ECR), mabasi hayo sasa yatapaswa kuanza safari saa 12.00 asubuhi kuanzia Jumatano, tarehe 21 Juni, 2023, endapo wataendelea kukiuka maelekezo haya, tutafuta leseni zao
Screenshot_20230620_060013_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom