Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Farhan Jr
Naandika hii post saa 4:34 usiku huu kutoka kwenye mitaa ya kawaida na vyumba bei chee Ubungo, naandika hii leo tarehe 13 Juni, 2023 siandiki kwa ajili yetu bali naandika kwa ajili ya wale wanaoitazama hii picha mwaka 2123 takribani miaka 100 kutoka hivi sasa, msiache picha hii ipotee.
Huenda soka kipindi hicho wanacheza Marobot ya Elon Musk lakini kutoka dunia yetu tunawaambia kuwa zama hizi Binadamu walisukuma kabumbu na kuipa Yanga Afrika matokeo uwanjani, majina na kumbukumbu zote rejeeni Google na Maktaba, washeni mishumaa kuwaombea zaidi pumziko jema.
Huenda miaka 100 kutoka sasa msifahamu hapo ni wapi! Hapo ni Kariakoo ilikuwa mitaa maarufu ya kibiashara ambapo TRA waliwahi kuvutana na Wafanyabiashara rejeeni kumbukumbu mtaona, ila hii siku Kariakoo ilifurahi kwa pamoja! Wananchi walipita na makombe yao! Mfanyabiashara na Mteja walibeba simu zao na kurecord kumbukumbu kwa pamoja, once in a lifetime.
Dear Future naomba niwaambie kuwa Yanga alicheza mechi nne ndani ya siku nane, mechi mbili za NBC dimba gumu la Sokoine, mechi moja Algiers na nyingine Pwani ya Kaskazini Tanga ya FA! Dear Future, kama Mashabiki tu walichoka kusafiri basi hadi wachezaji waliamka tu na mazoezi kidogo kisha wakaingia kwenye mechi, haikuwa rahisi uliza kiatu kwa sauti ya DJ Mark.
Huu ni msafara wa timu ya mpira, mitaa ilifungwa bila nguvu ya Polisi bali Mamlaka ya hisia na Mapenzi ya kweli kwa mpira wa miguu, walikatiza Msimbazi nyumbani kwa Simba na wala haikuwa vita kwakuwa Simba wanasema MY GAME IS FAIRPLAY, msigombane kisa hizi timu mmoja akifanikiwa pigeni makofi na mizimu itafurahi na mbingu za baraka zitafunguka, ninyi ni watani na sio Maadui.
Dear Future msiwe Wachoyo endeleeni kuandika kwa ajili ya vizazi na vizazi, tunzeni vyema kumbukumbu zenu kama ambavyo Mimi nilitunza hizi kwa ajili yenu.
One more time, hongereni sana Wananchi