Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230615_053551_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230615_053610_Opera%20Mini.jpg
 
RASMI | YANGA YAMUAGA NABI

Uongozi wa Yanga umethibitisha kumalizana na aliyekuwa Kocha wao mkuu Mohamed Nasreddine Nabi.

Yanga ipo kwenye mchakato wa haraka wa kutafuta Kocha mpya atakayekuja kubeba mikoba ya raia huyo wa Tunisia.
Screenshot_20230615_060805_Instagram.jpg
 
Klabu ya Young Africans SC imethibitisha kufikia makubaliano ya kuachana na Kocha mkuu Nasreddine Nabi baada ya kocha huyo kuomba kutoongeza mkataba mpya.

Kupitia taarifa yake kwa umma klabu ya Yanga imesema mkataba wa Nabi na klabu hiyo umemalizika mwisho wa msimu huu na kubainisha kuwa ilikutana na Kocha Nabi kwa ajili ya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya kocha huyo raia wa Tunisia aliomba kuondoka ili akapate changamoto mpya.

“Akiwa Kocha Mkuu wa Young Africans Sports Club, Nabi amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya NBC, mataji mawili ya Kombe la Shirikisho la Azam, mataji mawili ya Ngao ya Jamii na kuifikisha timu yetu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.” imesema taarifa hiyo.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unamshukuru Kocha Nabi kwa mchango wake katika kipindi chote alichofanya kazi kwenye timu yetu na unamtakia kila la kheri katika safari yake.”

“Aidha, Uongozi wa Young Africans Sports Club umeanza mchakato wa kumpata Kocha mpya atakayechukua nafasi ya Kocha Nasreddine Nabi.”

Screenshot_20230615_061039_Instagram.jpg
 
Jina la mmoja wa abiria watatu wa Uingereza waliofariki baada ya Boti kuwaka moto nchini Misri, limebainika kuwa ni Christina Quinn (58) ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya St Luke's Hospice Plymouth.

Msemaji wa familia yake alisema: "Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunathibitisha kifo cha kusikitisha cha Christina Quinn huko Misri.

"Alikuwa dada, binti, mke, shangazi, rafiki, na mwamba kwa wengi. Atakumbukwa zaidi ya maneno. "Tungeomba faragha kwa wakati huu."

Mwenyekiti wa Wadhamini wa St Luke, Charles Hackett, alisema: "Christina alikuwa na shauku kubwa kuhusu St Luke na mahali pake katika moyo wa jumuiya inayohudumia, na tumesikitishwa kupoteza uchangamfu wake, hekima na uongozi."

Bw Hackett alielezea kazi ya Bi Quinn, baada ya kuhudumu kwa miaka sita kwa hiari kama mwenyekiti wa bodi ya St Luke na kubainisha kuwa alipata heshima, imani na kuthaminiwa na wenzake.

Screenshot_20230615_061151_Instagram.jpg
 
Mwanaume mmoja raia wa Ubelgiji hivi karibuni alifeki kifo chake kuona nani kati ya ndugu zake anamjali.

David Barten (45) , mkewe na watoto waliamua kushirikiana kuwalaghai ndugu na marafiki.

Ili kusambaza habari za msiba huo feki, mtoto wa David aliposti kwenye mitandao ya kijamii na kuandika ujumbe wenye kuhuzunisha juu ya kifo cha baba yake.

Wikiendi iliyopita mazishi yalipangwa kufanyika karibu na mji wa Liege, na yalihudhuriwa na ndugu pamoja na marafiki wengi waliovaa nguo nyeusi.

Kila mmoja alijawa na huzuni huku wakingojea kuwasili kwa mwili, ghafla ilikuja helikopta.

Video iliyopostiwa kwenye mtandao wa TikTok na mmoja wa waombolezaji ilimuonyesha David akishuka kutoka kwenye helikopta akifuatana na timu ya wapiga picha.

Watu wengi walishikwa na mshangao huku wengine wakilia, wakimkimbilia na kumkumbatia.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times , David amesema alifeki kifo kuona nani katika familia yake anamjali,alikuwa akiona kila mmoja yuko kivyake, haalikwi popote na haonani na nduguze.

"Niliamua kuwapa somo, wasisubiri mtu akifa ndio wakutane naye.Sasa hivi wananijali, wananicheki kwa simu, kwahiyo mimi ndio mshindi."

Screenshot_20230615_061513_Instagram.jpg
 
Mwanaume mmoja raia wa Ubelgiji hivi karibuni alifeki kifo chake kuona nani kati ya ndugu zake anamjali.

David Barten (45) , mkewe na watoto waliamua kushirikiana kuwalaghai ndugu na marafiki.

Ili kusambaza habari za msiba huo feki, mtoto wa David aliposti kwenye mitandao ya kijamii na kuandika ujumbe wenye kuhuzunisha juu ya kifo cha baba yake.

Wikiendi iliyopita mazishi yalipangwa kufanyika karibu na mji wa Liege, na yalihudhuriwa na ndugu pamoja na marafiki wengi waliovaa nguo nyeusi.

Kila mmoja alijawa na huzuni huku wakingojea kuwasili kwa mwili, ghafla ilikuja helikopta.

Video iliyopostiwa kwenye mtandao wa TikTok na mmoja wa waombolezaji ilimuonyesha David akishuka kutoka kwenye helikopta akifuatana na timu ya wapiga picha.

Watu wengi walishikwa na mshangao huku wengine wakilia, wakimkimbilia na kumkumbatia.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times , David amesema alifeki kifo kuona nani katika familia yake anamjali,alikuwa akiona kila mmoja yuko kivyake, haalikwi popote na haonani na nduguze.

"Niliamua kuwapa somo, wasisubiri mtu akifa ndio wakutane naye.Sasa hivi wananijali, wananicheki kwa simu, kwahiyo mimi ndio mshindi."
Screenshot_20230615_061513_Instagram.jpg
 
Beki wa Simba HENOCK INONGA na Mshambuliaji wa Yanga FISTON MAYELE leo wameanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kilichocheza mechi ya kirafiki ya kimataifa ‘international friendly’ dhidi ya Uganda.

Mechi hiyo imechezwa Stade De Japoma, Douala, Cameroon ilimalizika kwa DR Congo kushinda kwa goli 1-0. Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Theo Bongonda nyota wa klabu ya Cadiz ya Spain.

Timu zote zipo kwenye maandalizi kuelekea mechi za kufuzu AFCON, Jumamosi Juni 18, 2023 Uganda itacheza dhidi ya Algeria na DR Congo itacheza dhidi ya Gabon.
Screenshot_20230615_061949_Instagram.jpg
 
ARSENAL KUMPIGA MNADA PARTEY
.
Arsenal imefungua milango ya kumpiga bei kiungo wa kimataifa wa Ghana Thomas Partey kwenye dirsha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi barani Ulaya. Arsenal inapambana kuboresha safu yake ya kiungo baada ya kukosa taji la Ligi Kuu England msimu uliopita mbele ya Manchester City.
.
Na kwenye mpango huo, imewaweka kwenye orodha viungo Declan Rice na Moises Caicedo ikipiga hesabu za kunasa saini zao katika dirisha hili huku wengine ikitarajia kuwafungulia mlango wa kutokea.

Partey, 30, mkataba wake umebakiza miaka miwili na kuna timu mbili za Italia zinahitaji saini yake.

Screenshot_20230615_062152_Instagram.jpg
 
️ | 𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆: 𝐊𝐚𝐢 𝐇𝐚𝐯𝐞𝐫𝐭𝐳

Arsenal waanza mazungumzo ya kumsajili Kai Havertz kwa mkataba wa kudumu kutoka Chelsea - Real wamejiondoa kwenye kumwania mchezaji huyo

◉ Arsenal waliwasiliana na Chelsea kwa Havertz, ada ya awali iliyoombwa ni £75m lakini hii inaweza kubadilika hivi karibuni.

◉ Vyanzo vinahisi Chelsea inaweza kubadilika na kukubali chini ya £70m - bila shaka, Arsenal haitalipa £75m.

◉ Jambo muhimu: mchezaji ana shauku ya kujiunga na Arsenal kwani angependa sura mpya baada ya miaka mingi katika Chelsea.

️ Real Madrid kwa sasa IMEJITOA mbioni - hawafikirii hata kulipa £50m kwa Kai.

◉ Kumbuka: Kipaumbele cha Arsenal, dili la Declan Rice litakamilika hivi karibuni - OFA rasmi inatayarishwa kwa Kai.

Screenshot_20230615_062723_Instagram.jpg
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa hakitoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata 14 uliotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kutokana na uchaguzi huo kuendelea kusimamiwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya kinyume na uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za watu

“Leo tarehe 14 Juni, 2023 Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata 14 zilizopo kwenye Halmashauri 13 nchini, Tume imetangaza kuwa ratiba ya kampeni itaanza tarehe 01-12 Julai, 2023 bila kuelezea ni kwanini muda wa kampeni umefanywa kuwa mdogo kiasi hicho”

“Uchaguzi huo utaendelea kusimamiwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya kinyume na uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za watu katika uamuzi wake wa tarehe 13 Juni, 2023 baina ya Ndugu Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kesi namba 011/2020 uliotolewa na Majaji 10 wa Mahakama hiyo kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mkataba wa Afrika ambao Tanzania iliuridhia”

“Wakati uamuzi huu wa Mahakama ya Afrika haujatekelezwa na Serikali, Tume imetangaza uchaguzi mdogo na kuwa utasimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Tume ya Taifa ya uchaguzi kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Afrika na kutekeleza uamuzi huo kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wowote nchini”
Screenshot_20230615_063123_Instagram.jpg
 
Uongozi wa Young Africans Sports Club umetoa taarifa kuwa umefikia makubaliano ya kuachana na Kocha wake Nasreddine Nabi baada va
Kocha huyo kuomba kutoongeza mkataba mpya.

“Mkataba wa Kocha Nasreddine Nabi na Klabu ya Young Africans Sports Club umemalizika mwisho wa msimu huu, baada ya kumalizika kwa mkataba huo, Uongozi wa Young Africans Sports Club ulikutana na Kocha Nabi kwa ajili ya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya lakini Nabi aliomba kuondoka ili akapate changamoto mpya”

“Akiwa Kocha Mkuu wa Young Africans Sports Club, Nabi amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya NBC, mataji mawili ya Kombe la Shirikisho la Azam, mataji mawili ya Ngao ya Jamii na kuifikisha Timu yetu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF”

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unamshukuru Kocha Nabi kwa mchango wake katika kipindi chote alichofanya kazi kwenye timu yetu na unamtakia kila la kheri katika safari yake, aidha Uongozi wa Young Africans Sports Club meanza mchakato wa kumpata Kocha mpya atakayechukua nafasi ya Kocha Nasreddine Nabi”
Screenshot_20230615_063252_Instagram.jpg
 
Mapema hii leo Mamlaka nchini Misri imetekeleza hukumu ya kifo kwa Mohamed Adel kwa kosa la mauaji ya Mwanafunzi ambaye alikataa ombi la kufunga nae ndoa mwaka jana.

Wakuu wa Magereza wametekeleza hukumu hiyo ya kifo kwa Mohamed ambaye alipatikana na hatia mwaka jana ya kesi ya mauaji ya kukusudia ya Mwanafunzi mwenzake aitwae Nayera Ashraf, baada ya kukiri kosa hilo Mahakamani.

Mohamed alihukumiwa katika kesi iliyogusa hisia za wengi mwezi June mwaka jana mara baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha Nayera akichomwa kisu nje ya maeneo ya Chuo Kikuu alichokuwa akisoma kilichopo Mansoura, kilomita 150 Kaskazini mwa Jiji la Cairo, nchini Misri.

Kesi ya mauaji ni shtaka la jinai linaloadhibiwa kwa hukumu ya kifo nchini Misri, ambapo Misri imekuwa Nchi ya nne iliyotekeleza hukumu nyingi zaidi za kifo kwa mwaka 2022 kulingana na taarifa kutoka Amnesty International.
Screenshot_20230615_063429_Instagram.jpg
 
Mwanamke anayeitwa Salma Shaibu(28) amefariki dunia Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi baada ya kujiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu chanzo kikidaiwa ni kujihisi mwenye hatia baada ya kukiri mwenyewe kabla ya kujiua ya kuwa alichepuka na Mwanaume mwingine.

Salma ambaye ameacha Watoto wawili akiwemo mkubwa ambaye anasoma elimu ya awali, enzi za uhai wake alikuwa akiishi na Mumewe Ramadhan Hamisi Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na akasafiri kwenda Wilayani Newala, Mtwara ambako alishawishika na kuingia kwenye mahusiano na Mwanaume mwingine, na baada ya kurudi nyumbani kwa Mumewe Masasi, Salma hakuwa mwenye furaha kwakuwa nafsi ilikuwa inamsuta.

Salma aliamua kumsimulia Rafiki yake wa kike na Mdogo wake na wote walimpa moyo na kumwambia akae kimya kwani jambo hilo akilisikia Mumewe linaweza kuzua balaa lakini aliendelea kuonekana mwenye simanzi mpaka Mumewe akahisi tofauti na kuumuliza Rafiki wa Mkewe ambapo alimsimulia kila kitu lakini Mume huyo hakukasirika na alisema ni jambo la kawaida na akamwambia Mkewe asiwe na wasiwasi.

Licha ya kusamehewa na Mumewe Salma hakuwa na amani na akaaga kwenda Wilayani Nachingwea kumsalimia Baba yake aliyekuwa mgonjwa ambako alikaa siku mbili na kuamua kunywa sumu kali ya kuulia wadudu kwenye mikorosho na kuacha na karatasi yenye ujumbe unaosema “NIMESHINDWA KUISHI KWA MAKOSA YANGU MWENYEWE” huku mkononi mwake akiwa ameandika ujumbe ambao unaendana sawa na maneno aliyoyaandika kwenye karatasi na kusisitiza sio tatizo la yeyote bali ni ujinga wake na kujihisi ameikosea Familia na Mungu wake.

Baada ya Mwili wa Marehemu kufikishwa kwenye Hospitali ya Mnero, imebainika ya kuwa alifariki baada ya sumu aliyokunywa kuathiri zaidi viungo vya ndani ya mwili na mfumo wa upumuaji, RPC wa Lindi Pili Mande, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa vijana kushirikisha Watu mbalimbali masuala yanayowasibu na kupata ushauri namna ya kutatua huku akiwaelekeza kutumia dawati la jinsia la Jeshi hilo kuelezea changamoto mbalimbali za kisaikolojia na mahusiano ili kupata msaada na kuepusha maamuzi magumu ya kujiua.
Screenshot_20230615_063617_Instagram.jpg
 
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa mkojo nchini (TAUS) pamoja na Daktari Bingwa kutoka Ufaransa kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kupandikiza uume kwa Watu wawili wenye matatizo ya nguvu za kiume ambao uume ulishindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa mbalimbali.

Akiongea baada ya kukamilisha upasuaji Dkt. Remigius Rugakingira Daktari Bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo na Wanaume kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa amesema kuwa upasuaji huu umefanyika kwa mara ya kwanza nchini.

“Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya upasuaji wa aina hii kilichofanyika hapa ni kuweka vipandikizi maalumu vitakavyowezesha uume kurudi katika hali yake ya kufanya kazi, upasuaji huu tumeshirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa mfumo wa mkojo pamoja na Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo kutoka Ufaransa na tumefanikiwa katika hilo”

Dkt. Rugakingira amesema huu ni wito kwamba Hospitali ya Benjamin Mkapa inajali afya ya Wanaume na upasuaji kama huu unaweza kufanyika Tanzania.

Hospitali ya BMH imekua Hospitali ya kwanza nchini kufanya upasuaji wa kuweka vipandikizi kwenye uume kwa wagonjwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.
Screenshot_20230615_063921_Instagram.jpg
 
Saudi Arabia imetangaza mkutano wa kimataifa wiki ijayo kwa ajili ya kukusanya ahadi za msaada kwa Sudan iliyoharibiwa kwa vita ambapo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya nusu ya idadi ya Watu wanahitaji msaada na ulinzi haraka.

@dw_kiswahili inaripoti kwamba mkutano huo wa ahadi utafanyika June 19,2023 na utaongozwa kwa pamoja na Qatar, Misri, Ujerumani na Umoja wa Ulaya, pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa takribani Watu milioni 25 ikiwa ni zaidi ya idadi ya jumla ya Watu wa Taifa hilo wanauhitaji wa msaada na ulinzi na mwishoni mwa Mei kulitolewa Dola milioni 2.6 katika kukabiliana na shida hiyo ikiwa sawa na asilimia 13 tu.

Kwa zaidi ya Wiki nane Saudi Arabia na Marekani zimekuwa katika juhudi za upatanishi kati ya Mkuu wa Jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na Makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo ambaye anaongoza kikosi cha kijeshi cha dharura.
Screenshot_20230615_064015_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom