Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230614_062718_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230614_062747_Opera%20Mini.jpg
 
Club ya Singida Big Stars leo imetangaza rasmi kuuzwa na sasa itakuwa inamilikiwa na Japhet Makau.

Singida baada ya kuuzwa imebadilishwa jina na sasa itakuwa ikijulikana kama Singida Fountain Gate FC.

Japhet Makau ni mmiliki wa shule za Fountain Gate pia ndio mmiliki wa timu za Fountain Gate FC inayoshiriki Ligi ya Championship na timu ya Wanawake Fountain Gate Princess.
Screenshot_20230614_143849_Instagram.jpg
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amelaani tabia za baadhi ya wanasiasa wanaodai kwamba Mwenge wa Uhuru umepitwa na wakati na ni mzigo kwa Taifa.

Makamba akipinga hoja hiyo amesema Mwenge ni tunu na nembo ya Taifa ambayo inapaswa kuheshimiwa hivyo, kusema kuwa unasumbua wananchi ni kuitusi nchi.

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ameitoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 14, 2023 katika Jimbo lake baada ya Mwenge kukimbizwa kwenye jimbo hilo na kuzindua na kukagua miradi tisa yenye thamani ya Sh779.1 milioni.

"Mwenge ni tunu na heshima kubwa kwa Taifa letu, tukiwa na mawazo na mtazamo kuwa hauna maana ni sawa na kuitusi nchi yetu. Wakati tunapata Uhuru hotuba ya kwanza ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alisema sasa tunawasha Mwenge ili uangaze nchi nzima," amesema.

Amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ni kielelezo cha uhuru, utaifa na ndoto hivyo, ni kiunganishi cha Watanzania na ni kielelezo cha Mtanzania.

Screenshot_20230614_144141_Instagram.jpg
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata 14 Tanzania Bara utakazofanyika Julai 13, mwaka huu.

Kuwepo kwa uchaguzi huo kumetangazwa leo Juni 14, 2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima ambaye ameeleza kuwa unafanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.

“Kwa mujibu wa taratibu, Tume kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, inatoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa uchaguzi huo wa madiwani katika kata 14 za Tanzania Bara,” amesema Kailima.

Screenshot_20230614_144249_Instagram.jpg
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Simbachawene ameonyesha kuwepo kwa mapungufu kwenye sheria ya likizo ya uzazi hasa kwa wanawake wanaozaa watoto njiti, hivyo kuwataka wabunge wapitie upya ili ikibidi ifanyiwe marekebisho.

Simbachawene ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akiongezea majibu katika swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Agnes Hokororo alihoji Serikali ina mpango gani wa kuongeza siku za likizo kwa wazazi wanaojifungua watoto njiti.

Waziri amesema kuwa siku 84 za likizo kwa mtoto aliyezaliwa Njiti bado hazitoshi kwani uumbaji huwa bado unaendelea hivyo akaomba maoni ya wabunge ili sheria hiyo ipelekwe bungeni na kufanyiwa marekebisho.
Screenshot_20230614_144407_Instagram.jpg
 
FOUNTAIN GATE YAINUNUA SINGIDA BIG STARS.

- Taarifa kutoka chanzo changu ni kuwa Mmiliki wa Fountain Gate, Japhet Makau amenunua hisa zote za klabu ya Singida Big Stars na ni rasmi anaimiliki timu hiyo kutoka Singida.

- Singida Big Stars itaitwa SINGIDA FOUNTAIN GATE FC na Makau anatarajiwa kuwa Rais na Mmiliki wa timu hiyo huku Makao Makuu ya timu yakiendelea kuwa mkoani Singida na dimba la Liti ndio Maskani yao.

- Kimuundo Makau atakuwa Rais na ataongoza bodi yenye Wajumbe tisa.

cc: @jr_farhanjrr
Screenshot_20230614_144623_Instagram.jpg
 
STARS HII NI FAINALI SI VINGINEVYO
.
Jumapili, wiki hii timu ya taifa ‘Taifa Stars’ itakuwa kibaruani tena kukipiga dhidi ya Niger katika mchezo wa kundi F wa kuwania kufuzu fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika mwakani nchini Ivory Coast.
.
Katika msimamo wa kundi lenye timu nne, Stars inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi nne sawa na Uganda ya tatu zikiongozwa na Algeria yenye alama 12 na ambayo tayari imeshafuzu, hivyo Tanzania itapaswa kuifumua Niger inayoshika mkia na alama mbili ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu.
.
Uganda, mshindani wa karibu wa Stars itaikaribisha Algeria katika mchezo ambao hautachezewa nchini Uganda kutokana uwanja wake mkubwa kuwa katika matengenezo ambayo yalitarajiwa kuwa yangekuwa yamekamilika, lakini hadi wiki za karibuni hali ilikuwa bado.
.
Hata hivyo, vyovyote ilivyo kikosi cha Stars chini ya kocha Adel Amrouche kitapaswa kujipanga vilivyo dhidi ya Niger ambayo licha ya kuwa na matokeo mabovu, lakini inaundwa na nyota wengi wanaokipiga katika mataifa ya Ulaya, hivyo wana uwezo wa kuamua mchezo wakiamua.

Kila la heri @taifastars_
Screenshot_20230614_144757_Instagram.jpg
 
ARSENAL, RICE DILI LAO LAFIKA PATAMU
.
Ndo hivyo. Arsenal imepewa nafasi kubwa ya kunasa saini ya kiungo Declan Rice, 24, kutoka West Ham United kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, huku klabu hizo zikijapanga kuanza mazungumzo juu ya ada inayopaswa kulipwa.
.
Kwa mujibu wa The Guardian, Arsenal ipo tayari kulipa ada ya awali ya Pauni 90 milioni kwa ajili ya kunasa saini ya kiungo huyo, huku ada yake ya jumla inaweza kufikia Pauni 100 milioni kutokana na nyongeza nyingine.
.
Kocha Arteta anaamini kwa kunasa saini ya Rice itamwezesha kutengeneza kikosi cha ushindani kitakachoweza kuchuana na timu imara kama Manchester City katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao.

Screenshot_20230614_145125_Instagram.jpg
 
GREALISH: SILVA, PLIZI USIONDOKE!
.
Staa wa Manchester City, Jack Grealish amejirekodi video akimtaka kiungo mshambuliaji wa mabingwa hao wa Ulaya, Bernardo Silva asiondike na aendelee kubaki klabuni hapo wapige kazi.
.
Kiungo huyo Mreno Silva amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Paris Saint-Germain dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na tayari ameshawaambia mabosi wa Man City anataka kuondoka. Silva awali alitaka kwenda Barcelona, lakini miamba hiyo ya Nou Camp bado haipo vizuri kiuchumi na hivyo haitakuwa na pesa inayofaa kunasa huduma ya mchezaji huyo.
.
Wakati Man City ikifanya paredi ya kushinda mataji matatu msimu huu, Grealish alionekana kwenye video akimwambia Silva: “Tafadhali usiondoke, Bernardo! Tafadhali usiondoke!” Alisema pia kwenye sherehe ya wachezaji hao: “Ukweli kuna mtu mmoja kwenye hii timu namkubali sana...lakini sasa anaonekana kama mtoto wa mitaani. Jina lake ni Bernardo Silva.” Silva alikuwa na mchango mkubwa kuifikisha Man City fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hatimaye kuichapa Internazionale 1-0 Jumamosi iliyopita na kuwa mabingwa wa Ulaya.
Screenshot_20230614_145313_Instagram.jpg
 
PSG KUMPIGA BEI MBAPPE
.
Paris Saint-Germain italazimika kumpiga bei supastaa Kylian Mbappe kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya baada ya nyota huyo kuamua kwamba hatamalizia mwaka wa tatu katika kikosi hicho cha Parc des Princes. Mbappe, 24, alifunga mabao 29 katika mechi 34 alizocheza kwenye Ligue 1. Mkataba wake aliosaini mwaka jana unaokwenda kumalizika 2025, imeelezwa kwamba mwaka wa tatu sio wa lazima, utatokana na uamuzi wake mwenyewe.
.
Hivyo, mkataba wa msingi utafika tamati 2024, jambo ambalo PSG itampoteza bure kama haitampiga bei dirisha hili sababu tayari alishaweka wazi hatatumikia ule mwaka wa tatu kwenye mkataba huo ambao si wa lazima. Mbappe alijiunga na PSG akitokea Monaco 2018, baada ya awali kucheza kwenye timu hiyo kwa mkopo, lakini sasa mabingwa hao wa Ligue 1 ili wapate chochote watalazimika kumuuza.

Screenshot_20230614_145408_Instagram.jpg
 
.
JUST IN: Timu nne za juu katika Ligi zitashiriki Ngao ya Jamii msimu ujao wa 2023/24, ambapo Simba watavaana na Azam FC na Singida Big Stars watacheza na Yanga na washindi ndiyo watakutana kwenye fainali ya Ngao.
.
◎ SIMBA SC AZAM FC
◎ YANGA SC SINGIGA BS

sportsarena_tz-20230614-0001.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom