Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwanaume mmoja raia wa Ubelgiji hivi karibuni alifeki kifo chake kuona nani kati ya ndugu zake anamjali.

David Barten (45) , mkewe na watoto waliamua kushirikiana kuwalaghai ndugu na marafiki.

Ili kusambaza habari za msiba huo feki, mtoto wa David aliposti kwenye mitandao ya kijamii na kuandika ujumbe wenye kuhuzunisha juu ya kifo cha baba yake.

Wikiendi iliyopita mazishi yalipangwa kufanyika karibu na mji wa Liege, na yalihudhuriwa na ndugu pamoja na marafiki wengi waliovaa nguo nyeusi.

Kila mmoja alijawa na huzuni huku wakingojea kuwasili kwa mwili, ghafla ilikuja helikopta.

Video iliyopostiwa kwenye mtandao wa TikTok na mmoja wa waombolezaji ilimuonyesha David akishuka kutoka kwenye helikopta akifuatana na timu ya wapiga picha.

Watu wengi walishikwa na mshangao huku wengine wakilia, wakimkimbilia na kumkumbatia.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times , David amesema alifeki kifo kuona nani katika familia yake anamjali,alikuwa akiona kila mmoja yuko kivyake, haalikwi popote na haonani na nduguze.

"Niliamua kuwapa somo, wasisubiri mtu akifa ndio wakutane naye.Sasa hivi wananijali, wananicheki kwa simu, kwahiyo mimi ndio mshindi."

View attachment 2658010
Hahahaha
 
Najarbu kuimagine ingekuwa bongo ingekuaje!!
 
Magazeti ya leo June 17, 2023
Screenshot_20230617_064459_Opera%20Mini.jpg
 
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa mkojo nchini (TAUS) pamoja na Daktari Bingwa kutoka Ufaransa kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kupandikiza uume kwa Watu wawili wenye matatizo ya nguvu za kiume ambao uume ulishindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa mbalimbali.

Akiongea baada ya kukamilisha upasuaji Dkt. Remigius Rugakingira Daktari Bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo na Wanaume kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa amesema kuwa upasuaji huu umefanyika kwa mara ya kwanza nchini.

“Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya upasuaji wa aina hii kilichofanyika hapa ni kuweka vipandikizi maalumu vitakavyowezesha uume kurudi katika hali yake ya kufanya kazi, upasuaji huu tumeshirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa mfumo wa mkojo pamoja na Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo kutoka Ufaransa na tumefanikiwa katika hilo”

Dkt. Rugakingira amesema huu ni wito kwamba Hospitali ya Benjamin Mkapa inajali afya ya Wanaume na upasuaji kama huu unaweza kufanyika Tanzania.

Hospitali ya BMH imekua Hospitali ya kwanza nchini kufanya upasuaji wa kuweka vipandikizi kwenye uume kwa wagonjwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.
View attachment 2658028

Bei gani nikapandikize kibamia changu
 
Mwanamke anayeitwa Salma Shaibu(28) amefariki dunia Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi baada ya kujiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu chanzo kikidaiwa ni kujihisi mwenye hatia baada ya kukiri mwenyewe kabla ya kujiua ya kuwa alichepuka na Mwanaume mwingine.

Salma ambaye ameacha Watoto wawili akiwemo mkubwa ambaye anasoma elimu ya awali, enzi za uhai wake alikuwa akiishi na Mumewe Ramadhan Hamisi Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na akasafiri kwenda Wilayani Newala, Mtwara ambako alishawishika na kuingia kwenye mahusiano na Mwanaume mwingine, na baada ya kurudi nyumbani kwa Mumewe Masasi, Salma hakuwa mwenye furaha kwakuwa nafsi ilikuwa inamsuta.

Salma aliamua kumsimulia Rafiki yake wa kike na Mdogo wake na wote walimpa moyo na kumwambia akae kimya kwani jambo hilo akilisikia Mumewe linaweza kuzua balaa lakini aliendelea kuonekana mwenye simanzi mpaka Mumewe akahisi tofauti na kuumuliza Rafiki wa Mkewe ambapo alimsimulia kila kitu lakini Mume huyo hakukasirika na alisema ni jambo la kawaida na akamwambia Mkewe asiwe na wasiwasi.

Licha ya kusamehewa na Mumewe Salma hakuwa na amani na akaaga kwenda Wilayani Nachingwea kumsalimia Baba yake aliyekuwa mgonjwa ambako alikaa siku mbili na kuamua kunywa sumu kali ya kuulia wadudu kwenye mikorosho na kuacha na karatasi yenye ujumbe unaosema “NIMESHINDWA KUISHI KWA MAKOSA YANGU MWENYEWE” huku mkononi mwake akiwa ameandika ujumbe ambao unaendana sawa na maneno aliyoyaandika kwenye karatasi na kusisitiza sio tatizo la yeyote bali ni ujinga wake na kujihisi ameikosea Familia na Mungu wake.

Baada ya Mwili wa Marehemu kufikishwa kwenye Hospitali ya Mnero, imebainika ya kuwa alifariki baada ya sumu aliyokunywa kuathiri zaidi viungo vya ndani ya mwili na mfumo wa upumuaji, RPC wa Lindi Pili Mande, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa vijana kushirikisha Watu mbalimbali masuala yanayowasibu na kupata ushauri namna ya kutatua huku akiwaelekeza kutumia dawati la jinsia la Jeshi hilo kuelezea changamoto mbalimbali za kisaikolojia na mahusiano ili kupata msaada na kuepusha maamuzi magumu ya kujiua.View attachment 2658025

R.I.P
 
Kongole kwa Wababa wote tuliomo ndani ya jukwaa hili adhimu. Najua hatujali sababu ni wajibu wetu kuwa wababa bora kabisa duniani.
Happy Father's Day
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom