Rais wa Club ya soka ya Yanga Injinia Hersi Said @caamil_88 leo amemkaribisha rasmi kwenye Club hiyo Rais wa Wasafi Mwimbaji Staa Diamond Platnumz baada ya parade ya shangwe la kulipokea Kombe la Azam Federation, kauli ambayo ameitoa baada ya perfomance kubwa aliyoifanya Staa huyo Makao Makuu Jangwani wakati wa kupokea kombe hilo.
Rais Hersi ameweka picha yake na Diamond wakiwa wamelibeba kombe hilo na kuandika "Mwanamuziki bora Afrika katika Klabu bora Afrika, karibu
diamondplatnumz katika klabu ya Wananchi, Mabingwa wa muda wote nchini Tanzania na finalist wa CAF CC, pokea ubingwa na iwe ishara ya utamaduni wa kufurahi pamoja katika mafanikio yetu"
"Leo pale Jangwani imepigwa show ya hatariiiiiiii... top performance kutoka kwa Mwamba
diamondplatnumz nomaaaaa

, ama hakika wananchi wamefurahi kibingwa!!!"
Siku chache zilizopita kwenye kusherehekea siku 100 za @manaratv__ Diamond Platnumz alikiri kushawishiwa na Semaji @HajisManara kuishabikia Timu hiyo aliyasema yafuatayo "Katika mambo ya kimpira hakuna asiyefahamu na hakuna ambaye atapingana na hili kwamba nguvu yako kubwa imesababisha kuongeza mwamko mkubwa katika football Nchini Tanzania”
“Wakina kama sisi sio Watu wa kujua mpira sana lakini tumekua tunapenda kufatilia mpira sana kwa sababu yako na nisiongee unafiki, ulipo nipo" alimalizia Platnumz.