Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230316_073227_Opera%20Mini.jpg
 
Serikali Wilayani Ludewa Mkoani Njombe imepiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe, kuingiza mfugo wa Nguruwe pamoja na kutumia mazao yeyote ya Nguruwe ikiwemo Damu, samadi, mifupa na nywele kwa muda usiojulikana isipokuwa kwa idhini ya Daktari wa mifugo wa Wilaya hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Daktari wa mifugo wa Wilaya hiyo Dkt. Festo Mkomba imeeleza yafuatayo "kwa Mamlaka niliyopewa na sheria ya mifugo namba 16 (2),17 ya mwaka 2003, kuanzia leo tarehe 15/03/2023 natangaza kwamba Wilaya ya Ludewa itakuwa chini ya Karantini mpaka hapo itakavyotangazwa vinginevyo hii ni kutokana na matukio ya ugonjwa wa homa ya Nguruwe kujitokeza katika Wilaya ya Ludewa"

Taarifa hiyo imeeleza kuwa adhabu kali itatolewa kwa mujibu wa sheria kwa yeyote atakayekiuka masharti yaliyotolewa kutokana na uwepo wa ugonjwa huo wa homa ya Nguruwe.

Aione huyu mzee mtu chake na auntie yangu Makiwendo hawataelewa kabisaView attachment 2553201
Hii ht mm cjaielewa kbs
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa tahadhari juu ya uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana Mkoani Kagera katika Wilaya ya Bukoba Vijijini ambapo Watu 7 wanasadikika walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi na Watu watano kati yao wamefariki na wengine wawili wako Hospitali wanaendelea na matibabu.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ametoa taarifa hiyo leo katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma “Wizara imepokea taarifa za uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana Kagera, Bukoba Vijijini, Kata ya Maruku na Kanyangercko, Vijiji vya Bulinda na Butayaibega, mwenendo wa ugonjwa huu unaashiria uwezekano kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza hivyo Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu na kuchukua hatua za kudhibiti ili usisambae”

Prof. Nagu amewataka Wananchi kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu endapo ataona dalili kama kupatwa na homa, kutapika, kuharisha, kutoka damu na mwili kuishiwa nguvu, pia amewakumbusha kuwahi Kutoa taarifa mapema kwenye kituo cha kutolea huduma kilicho karibu au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo utamuona au kukutana na Mtu mwenye dalili kama hizo.
Screenshot_20230317_045200_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230317_045216_OGInsta%2B.jpg
 
Daktari Bingwa wa Pua, Koo na Masikio, Dkt. Jane Bazilio wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi, Kibaha amewashauri Watu kutoingiza maji kwenye masikio yao wakati wa kuoga au kuyasafisha kwa kutumia pamba za masikio kwani kwa kawaida sikio hujisafisha lenyewe.

Dkt. Bazilio ameyasema haya wakati wa kambi ya huduma za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora-Kitete na kusisitiza kuwa sikio huwa linajisafisha lenyewe hivyo Mtu anapotumia pamba anakuwa anatoa nta iliyoko kwenye sikio ambayo kazi yake ni kulilinda sikio.

“Katika kambi hii tumewaona Wagonjwa wengi wenye matatizo ya masikio na pua, Wananchi wengi wanafikiri ile nta ni uchafu kutokana na rangi yake ile ya brown (kahawia) na kusema wanatoa uchafu ile sio uchafu ina kazi yake ya kulinda sikio, nta ile msiitoe ina utaratibu wake wa kutoka kwenye sikio”

Amesema Wagonjwa wengi waliojitokeza kwenye kambi hiyo wanakuwa na shida ya fangasi masikioni ambayo husababishwa na unyevunyevu kwenye masikio hivyo akawataka Watu wasiingize maji kwenye masikio yao pindi wanapooga au kunawa kichwa.

Daktari huyu amewashauri pia Wazazi na Walezi kuacha kuwasafisha Watoto wadogo kwa pamba kwani wanaposafisha nta ile inaweza kuingia kwenye sikio na kusababisha kuziba kwa sikio na kwamba ni hatari hata kwa Watu wazima pia.
Screenshot_20230317_045344_OGInsta%2B.jpg
 
Daktari Bingwa wa Pua, Koo na Masikio, Dkt. Jane Bazilio wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi, Kibaha amewashauri Watu kutoingiza maji kwenye masikio yao wakati wa kuoga au kuyasafisha kwa kutumia pamba za masikio kwani kwa kawaida sikio hujisafisha lenyewe.

Dkt. Bazilio ameyasema haya wakati wa kambi ya huduma za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora-Kitete na kusisitiza kuwa sikio huwa linajisafisha lenyewe hivyo Mtu anapotumia pamba anakuwa anatoa nta iliyoko kwenye sikio ambayo kazi yake ni kulilinda sikio.

“Katika kambi hii tumewaona Wagonjwa wengi wenye matatizo ya masikio na pua, Wananchi wengi wanafikiri ile nta ni uchafu kutokana na rangi yake ile ya brown (kahawia) na kusema wanatoa uchafu ile sio uchafu ina kazi yake ya kulinda sikio, nta ile msiitoe ina utaratibu wake wa kutoka kwenye sikio”

Amesema Wagonjwa wengi waliojitokeza kwenye kambi hiyo wanakuwa na shida ya fangasi masikioni ambayo husababishwa na unyevunyevu kwenye masikio hivyo akawataka Watu wasiingize maji kwenye masikio yao pindi wanapooga au kunawa kichwa.

Daktari huyu amewashauri pia Wazazi na Walezi kuacha kuwasafisha Watoto wadogo kwa pamba kwani wanaposafisha nta ile inaweza kuingia kwenye sikio na kusababisha kuziba kwa sikio na kwamba ni hatari hata kwa Watu wazima pia.
Screenshot_20230317_045344_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzani, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Aretas James Lyimo kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA) akichukua nafasi ya Gerald Kusaya ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Screenshot_20230317_045643_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameteua Gerald Msabila Kusaya, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, kabla ya uteuzi huu, Kusaya alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.

Rais Samia pia amemteua Ally Senga Gugu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, kabala ya uteuzi huu, Gugu alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na amemteua Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro akichukua nafasi ya Willy Machumu ambave amestaafu.

Rais pia amemhamisha Fatuma Ramadhani Manga, kutoka Mkoa wa Dodoma kwenda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida akichukua nafasi ya Dorothy Aidan Mwaluko ambaye amestaafu, Rashid Kassim Mchata, amehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani akichukua nafasi ya Zuwena Omari Jiri ambaye amehamishiwa Mkoa wa Lindi akichukua nafasi ya Ngussa Samike ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Screenshot_20230317_045739_OGInsta%2B.jpg
 
Kampuni ya ASAS ( @asas_dairies ) yenye Makao Makuu yake Mjini Iringa ikijishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za maziwa, imetoa shilingi milioni 100 kwa Wafanyabiashara wadogowadogo wa Iringa maarufu kama Machinga ili iwasaidie kujenga vibanda vyao vya kufanyia biashara.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo Salim Abri ASAS ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Wa Iringa (MNEC) ndiye aliyetangaza msaada huo wa fedha.

Akizungumza na Wafanyabiashara hao, Salim amesema katika fedha hizo milioni 50 itatumika katika ujenzi wa Vibanda vya kufanyia biashara na milioni 50 iliyobaki itatumika kama Mtaji kwa Wafanyabiashara hao.
Screenshot_20230317_045852_OGInsta%2B.jpg
 
Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza imepokea Meli ambayo imebeba mzigo wa magari pamoja na shehena nyingine za mizigo kutoka Nchini China.

Meli hiyo ijulikanayo kwa jina la Della imepakia shehena ya mizigo katika Bandari ya Zhanjiangang iliyoko Shanghai, China na kusafirisha mizigo katika Bandari mbalimbali ikiwemo ya Tanga.

Akiongea wakati wa upokeaji wa shehena hiyo ya mzigo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amesema ujio wa Meli kubwa za mizigo unatokana na maboresho makubwa yaliyofanyika ya ujenzi wa gati mpya yenye urefu wa Mita 450.

"Hii Bandari ndio moyo wa uchumi wa Mkoa wa Tanga hivyo huu ni mwanzo tuu wa ujio wa Meli kubwa kwani tutaendelea kuvunja rekodi kila mara na niwaombe Wafanyabiashara kuitumia Bandari ya Tanga kwa ajili ya uhakika wa usafirishaji wa mizigo "

Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amesema kuwa Meli hiyo yenye urefu wa Mita 176 imeweza kutia nanga katika gati na itaweza kuhudumia kwa siku moja pekee “Uwepo wa vifaa vya kisasa umerahisisha shughuli za upakuaji wa shehena ya mizigo ikiwemo kupunguza muda wa kuhudumia shehena katika Bandari yetu"
Screenshot_20230317_045958_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mtoto wa Rais Museveni ametangaza nia yake ya kutaka kumrithi Baba yake kiti cha Urais wa Uganda ambapo amesema atagombea Urais wa Nchi hyo mwaka 2026.

“Katika jina la Yesu Kristo, kwa jina la Vijana wa Uganda na Dunia kwa ujumla na katika jina la Mapinduzi makubwa nitagombea Urais mwaka 2026”

“Fidel Castro Shujaa wangu alikuwa Rais akiwa na umri wa miaka 32, ninakaribia kufikia miaka 49, sio sawa kabisa (Kutokuwa Rais), Vijana wanapaswa kuwa Marais wa Mataifa yao”

“Nani anakubaliana na Mimi kwamba muda wetu Vijana umewadia?, inatosha sasa kuendelea kuongozwa na Wazee na kututawala,ni muda wa Vijana kung’aa, Waziri Mkuu wa Uingereza ana miaka 42, Waziri Mkuu wa Finland ana miaka 37 , sisi wengine tunakaribia miaka 50, tumechoka kusubiri, nitasimama kugombea”
Screenshot_20230317_050058_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa timu hiyo haijafungiwa kusajili madirisha matatu na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake.

Na badala yake, Eymael ameiambia Mwanaspoti kuwa uamuzi uliotolewa na FIFA ni kuishinikiza Yanga kulipa madai yake ili isikumbane na adhabu hiyo.

Kauli hiyo ya Eymael imekuja muda mfupi baada ya mtandao mmoja wa Afrika Kusini kudai kuwa Yanga imefungiwa kusajili kwa madirisha matatu kwa kosa la kutomlipa kocha huyo.

"Nadhani walioandika taarifa hiyo wameripoti kinyume. FIFA walitoa uamuzi na pande zote tumejulishwa kwamba Yanga wanatakiwa kunilipa stahiki zangu ndani ya siku 45 na iwapo wakishindwa kufanya hivyo, kuna adhabu kubwa zaidi watapewa ikiwemo ya kufungiwa kusajili." alisema Eymael.
Screenshot_20230317_050347_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua wiki ya Maji kitaifa inayoanza leo Alhamis Machi 16 -22 kila mwaka kwa kuzindua mradi wa mfumo wa usambazaji maji kutoka Makongo hadi Mji wa Bagamoyo.

Uzinduzi huo umefanyika leo Alhamisi Machi 16, 2023 ma kushuhudiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na watendaji waandamizi wa Wizara ya Maji.

Screenshot_20230317_050446_OGInsta%2B.jpg
 
Msanii Burna Boy kutoka Nigeria rasmi atatumbuiza katika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitakazofanyika Juni mwaka huu katika Uwanja wa Atatürk Olympic uliopo Istanbul nchini Uturuki.

Mkali huyo wa Afrobeats Burna anatamba na ngoma kali ikiwemo its plenty, on the low, Last Last na Ye alipata pia nafasi ya kutumbuiza katika mapumziko ya mechi ya NBA All-star Game iliyofanyika Februari mwaka huu nchini Marekani.

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ni Bayern Munich, Manchester City󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿, Chelsea󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿, AC Millan, Benfica, Inter Milan, Real Madrid na Napoli.
Screenshot_20230317_050538_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi anapiga hesabu kali za kuhakikisha mastaa wa kikosi chake wanapata muda wa kupumzika pindi wanapotumika sana, ila yupo mmoja ambaye ametumia fursa kivingine.

Winga wa timu hiyo, Jesus Moloko ambaye yupo kwenye kiwango kikubwa hataki mapumziko hayo kuna wakati anamwambia Kocha Nabi kwamba anahitaji kucheza zaidi ili kujiweka fiti.

Moloko aliliambia Mwanaspoti: ”Tukitoka kucheza michuano ya kimataifa mara nyingi kocha anatoa mapumziko, lakini mimi huwa namwambia asinipe nahitaji kucheza ili kujiweka kwenye ufiti zaidi.

Aliongeza: “Kuna ushindani wa namba mkali aliyepo benchi akipewa nafasi anapambana kwa kadiri kuisaidia timu, ndio maana sitaki kuichezea kabisa nafasi ninayopata nahitaji huduma yangu iwe muhimu kikosi cha kwanza.”
Screenshot_20230317_050637_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imesema iwapo mipango ya kuongeza uzalishaji umeme utakwenda kama inavyokusudiwa itasaidia kupunguza gharama za matumizi ya gesi kwa wananchi wa kipato cha kati na chini.

Hayo yameelezwa jana Junatano Machi 15 na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Exaud Kigahe kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk Ashatu Kijaji wakati wa kongamano la maadhimisho ya kitaifa ya siku ya haki za mtumiaji duniani yaliyofanyika jijini hapa.

Kigahe amesema Serikali kama chombo chenye wajibu wa kutekeleza miradi ya nishati safi ya gesi ni kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa wananchi wote na kwa gharama nafuu ili kukuza kipato.

Screenshot_20230317_050741_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom