Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230314_064204_Opera%20Mini.jpg
 
Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Oni Sigala amewataka Watanzania kupuuza bango la kughushi linalozunguka katika mitandao ya kijamii likisema Baraza hilo limekemea vikali matumizi ya maneno ya ‘famchezo nini, famasihara nini na fautani nini ambayo kwa siku za karibuni yamekua yakitumika na baadhi ya Watu mitandaoni.

Taarifa rasmi ya Baraza hilo imeeleza yafuatayo “si kweli na Baraza halihusiki na bango hilo lenye makosa mengi ya kiuandishi lakini makosa makubwa zaidi aliyoyafanya Mwandishi ni kuonya matumizi ya misimu aliyoorodhesha ambayo kimsingi baraza halijawahi kukemea au kuonya matumizi ya maneno ya misimu”

“Tunapenda kuwakaribisha Wadau wote wa Kiswahili wenye nia ya kuelimisha jamii kupata ufafanuzi wa kina kwa jambo wanalotaka jamii ijifunze, pia tunawaomba wanaoghushi nembo na nyaraka za Baraza kuacha mara moja kwa kuwa ni kosa kisheria kutumia nembo na nyaraka bila idhini ya baraza”

“Matumizi ya misimu yanaweza kukuza lugha iwapo yatakuwa na mashiko na yatasanifiwa, Baraza linaomba kupuuzwa kwa mabango ambayo yanatengenezwa na Watu wachache wasio waaminifu kwa lengo la kujiongezea wafuasi katika kurasa zao” imeeleza taarifa hiyo.
Screenshot_20230316_044123_OGInsta%2B.jpg
 
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu Mwanafa amesema Serikali ina mpango wa kuongeza hadhi ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa kuifanya taasisi hiyo iingiliane na Kiwanda cha Muziki na Filamu hapa nchini ili Watu wote wanaofanya shughuli za Utamaduni na Sanaa waone fahari ya kupita katika Chuo hicho.

Naibu Waziri Hamisi Mwinjuma ameyasema hayo leo Machi 15, 2023 alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo.

Hamis Mwinjuma amesema miongoni mwa mambo ambayo yamepangwa kufanyiwa kazi kwa kiwango kikubwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu na vifaa ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunza

“Hatusemi kwamba vifaa tulivyonavyo haviwezi kutuzalishia Watalaamu tunaowahitaji kwenye Utamaduni na Sanaa lakini nafikiri nguvu kubwa inahitajika kuongezeka na hicho ndio nimekuja kukiangalia, tumekuwa tukikaa na Mkuu wa Taasisi kwa muda na tumekuwa tunajadiliana namna ya kustawisha mafunzo yanayotolewa hapa na hili la vifaa ni miongoni mwa mambo ambayo tumekuwa tukiyajadili”

“Nimepita niyaone kwa macho yangu kwasababu tumepanga kuyafanyia kazi kwa kiwango kikubwa, tunataka kuzalisha, Mameneja kwa ajili ya muziki, tunataka kuzalisha Waongozaji na Watengeneza Filamu, Waigizaji na vyote hivi vinahitaji vifaa na vinahitaji miondombinu inayoeleweka ili tuweze kupata Watu wa kiwango cha kushindana na kasi ya dunia kwenye nyanja hiyo”
Screenshot_20230316_044606_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230316_044930_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali Wilayani Ludewa Mkoani Njombe imepiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe, kuingiza mfugo wa Nguruwe pamoja na kutumia mazao yeyote ya Nguruwe ikiwemo Damu, samadi, mifupa na nywele kwa muda usiojulikana isipokuwa kwa idhini ya Daktari wa mifugo wa Wilaya hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Daktari wa mifugo wa Wilaya hiyo Dkt. Festo Mkomba imeeleza yafuatayo "kwa Mamlaka niliyopewa na sheria ya mifugo namba 16 (2),17 ya mwaka 2003, kuanzia leo tarehe 15/03/2023 natangaza kwamba Wilaya ya Ludewa itakuwa chini ya Karantini mpaka hapo itakavyotangazwa vinginevyo hii ni kutokana na matukio ya ugonjwa wa homa ya Nguruwe kujitokeza katika Wilaya ya Ludewa"

Taarifa hiyo imeeleza kuwa adhabu kali itatolewa kwa mujibu wa sheria kwa yeyote atakayekiuka masharti yaliyotolewa kutokana na uwepo wa ugonjwa huo wa homa ya Nguruwe.

Aione huyu mzee mtu chake na auntie yangu Makiwendo hawataelewa kabisa
Screenshot_20230316_045125_OGInsta%2B.jpg
 
Benki ya NMB imezindua huduma ya mikopo ya elimu ya juu iitwayo ‘NMB Elimu Loan’ na kuitengea kiasi cha Shilingi Bilioni 200 za Kitanzania kwa ajili ya kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa riba nafuu maalum kwaajili ya Watumishi na Wafanyakazi ambao mishahara yao inapitia kwenye Benki hiyo.

Taarifa ya @nmbtanzania kwa Vyombo vya Habari imesema Mtu yeyote anaweza kuchukua mkopo huo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu ama kwaajili ya Vijana, Watoto au Wenza.

Maelezo ya ziada ya mkopo huo ni kama ifuatavyo, mkopo unatolewa kwa Mwajiriwa yoyote ambae ni Mteja wa NMB, unaanzia TZS 200,000 hadi TZS milioni 10 kwa mwaka kwa Mtu mmoja na riba yake ni 9% na muda wa marejesho wa miezi 12 ambapo unatolewa pia kwa ngazi ya Vyuo vya kati vikiwemo Vyuo vya Ufundi.

Akitangaza kuanzishwa kwake rasmi, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema yafuatayo ““Huu ni utekelezaji wa makubaliano yetu na Wizara ya Elimu ya kuanza kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kupunguza utegemezi wa Waajiriwa kwa Bodi ya mikopo (HESLB) pale wanapotaka kujiendeleza kimasomo na pia kuwalipia ada vijana wao”.

Kwa kuanzisha huduma hii ambayo inapatikana kwenye tawi lolote la Benki hii, NMB inakuwa imetimiza ahadi iliyoitoa mwaka 2022 ya kuisaidia Serikali kuipunguzia HESLB mzigo wa kufadhili masomo ya juu na kuwa na vyanzo vipya vya mikopo ya elimu.
Screenshot_20230316_045344_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom