Farhan Jr
CLATOUS CHOTA CHAMA, leo ni Jumapili Machi 19, Dominika ya 4 ya Kwaresma na leo Mama Kanisa anatukumbusha kuhusu Kuponywa kwa Upofu (Healed of Blindness)!
Nimshukuru sana Mama Kanisa kwa somo hili la leo! Ngoja niwape kidogo kuhusu somo hili, nasi tunataka kuwaponya watu upofu leo hii! Kuhusu Mchezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea nchini.
Somo linaanza na kuwa kuna Kijiji alizaliwa kipofu, yeye kila ifikapo jioni huchukua taa yake kukatisha kwenye msitu mmoja mkubwa sana, siku moja kuna Mtu akamuuliza!
“Wewe ni kipofu kwanini unabeba taa?” Nae akamjibu kuwa anabeba taa ili wao wanaoona wasigongane na yeye kwakuwa haoni, tazama ukuu wa heshima na busara hii.
Ni kama sisi tunaposema CLATOUS CHAMA ndie MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA, kwakuwa tunafahamu macho yenye afya hayawezi kuona yote, trust me! Nasi tunataka mbebe taa ili tusigongane, hizo taa ziwe takwimu kama hazipo basi msitembee wakati wa jioni.
Kuna upofu mwingine pia ambao umejikita katika mizani ya ulimwengu,: pesa, mafanikio, kazi, mapenzi, afya na ugonjwa, ujana na uzee! Nasi kwa kufahamu hayo tunaendelea kuwakumbusha bila kuchoka kuhusu CHAMA.
Mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu kwenye hatua ya makundi kutoka timu za Tanzania, Mchezaji wa kwanza eneo la Kiungo kufikisha mabao 14 kwenye Champions League, Mchezaji wa kwanza kutoka Zambia kufanya hivyo Champions League na anaongoza mabao manne na assist moja mbele ya wote Afrika.
Upofu ni nini? Upofu” ni kushindwa kuona mkono wa Mungu ukifanya kazi kati yetu. Tunakazana kutafuta miujiza ya Neema za Mungu zinazo onekana kwetu na kwa wengine.
Hili ni somo la kwanza Jumapili ya leo!

Makala bado zipo, Asante!
Niwatakie Dominika Njema Watu wa Mungu
