“Timu zetu [Tanzania] bado hatujafikia hatua ya kuwa mabingwa wa mashindano ya Afrika kutokana na aina ya vikosi vya timu zetu.”
“Ukiangalia Simba ambao wamekuwa wakishindana vizuri kwenye michuano ya Afrika hivi karibuni, utaona ni kama bado wanatengeneza timu yao.”
“Ile timu iliyokuwa inashindana haipo tena baada ya wachezaji wengi kuondoka [Okwi, Miquissone, Lwanga, Dilunga, Kagere, Mugalu, Wawa, n.k] kwa sababu tofauti ikiwa ni umri, viwango n.k. Wachezaji wachache wamebaki ambao bado wana uwezo wa kutoa mchango ambao walikuwa wanautoa misimu mitatu nyuma.”
“Wana wachezaji wengi wapya ambao wamekuja ukiwa ni mpango wa kuandaa timu, hata Simba inavyocheza mechi za Ligi bado sio timu imara.”
“Ina wachezaji wenye madaraja ya juu ambao leo wanaweza wakacheza na timu kushinda kwa magoli 7 lakini mechi inayofuata wakapambana utafuta goli moja.”
“Bado haina mwendelezo wa kiwango ambacho imekuwa ikikionesha, kwa hiyo Simba ina wachezaji wazuri lakini bado hawana timu imara.”
“Yanga wana timu imara, wachezaji wengi hawapo kwenye kiwango kizuri kwa wakati husika. Wanacheza na kupata ushindi ndio maana kwenye Ligi yetu kwao kushinda sio habari tena haijalishi wamechezaje au wamepanga kikosi gani.”
“Kwa timu zetu kutoka hatua ya makundi kwenda hatua inayofuata inawezekana. Hatua ambazo watu wanaziota [Nusu Fainali, Fainali na Ubingwa] zinahitaji miujiza ya soka kuzifikia.”
- Amri Kiemba