Makapuku Forum

Makapuku Forum

KMC HALI TETE!

Katika michezo 14 iliyopita ya Ligi Kuu 2022|23, KMC imeshinda mechi mbili tu! Ni matokeo mabaya zaidi kwa timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni katika nyakati hizi Ligi inapoelekea kumalizika.

Kwenye mechi hizo 14 zilizopita, KMC ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Coastal Union na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania. Mechi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru [uwanja unaotumiwa na KMC kwa mechi zake za nyumbani].

Mechi nyingine 12 ni mchanganyiko wa sare na kupoteza! Imepoteza mechi nane (8) na kutoka sare kwenye mechi nne (4).

Kwenye mechi tano (5) zilizopita, KMC imepoteza mechi nne (4) na kuambulia sare moja (1). Kwa maana hiyo, katika mechi tano (5) zilizopita KMC imepata alama moja tu!

Ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 23 tofauti ya alama moja (1) na Tanzania Prisons ambayo ipo nafasi ya 13 ikiwa ni sehehemu ya kucheza play offs kubaki Ligi Kuu.
Screenshot_20230208_053228_OGInsta%2B.jpg
 
Nikisikia chochote huwa nina tabia ya kuwauliza na nawasisitiza waniambie ukweli na wanafahamu siku wakinidanganya basi kesho yake hawatonikuta hapa, mara nyingi huwa wanasema sio kweli na mimi nawaamini.

- Pep Guardiola, alipohijiwa na Waandishii Julai 2022 kuhusu tuhuma za Man City.
Screenshot_20230208_053321_OGInsta%2B.jpg
 
Nadhani Simba na Yanga tukae chini kama taasisi mbili (2), pamoja ya kuona namna ya kushirikiana kuweka sawa huu mkataba wa CAF.”

“Timu zetu Wadhamini wakuu ni betting, sio afya wao kukosa mileage kimataifa kisa mkataba ambao CAF wamesaini na kampuni nyingine. Ulaya klabu zinacheza UEFA zikiwa na mikataba tofauti na shirikisho lao na hazina athari kwa klabu.”

“Timu zetu zinapambana kuwapata Wadhamini sio afya kuwanyima mileage, Liverpool alikuwa na Standard Chartered wakati EPL ina Barclays, ni kawaida ni lazima tuungane kutokomeza vipengele kandamizi kama hivi.”

- CPA @issamasoud Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba.
Screenshot_20230208_053840_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina ameibua hoja kuhusu marekebisho ya Katiba na mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya Bungeni Dodoma leo wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo.

Mpina amenukuliwa akisema “Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa mwongozo kuanzia June 2022 kuhusiana na kuanza kwa mchakato wa maandalizi ya marekebisho ya Katiba tuliyonayo sasa lakini pia mapendekezo ya Katiba mpya lakini mpaka sasa hivi Wizara ya Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu hakuna mwongozo wowote wala deadline yoyote, hakuna utafiti wowote tangu Kiongozi wa nchi atoe maelekezo leo miezi saba halijawekwa mahali popote”

“Mimi naungana na Mh. Rais kwamba ni muda wa mwafaka kuangalia Katiba yetu na moja eneo muhimu ni kwamba Katiba tuliyonayo sasa haina nguvu za kusimamia na kulinda fedha na rasilimali za Umma kwa sasa”
Screenshot_20230209_055144_OGInsta%2B.jpg
 
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) amesema hana nia ya kuendelea na kesi ya jinai namba 11 ya mwaka 2022 ya usafirishaji haramu wa Binadamu iliyokuwa ikimkabili Diana Bundala maarufu Mflame Zumaridi Jijini Mwanza.

Kesi hiyo imetajwa leo February 08, 2023 katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Mwanza na kusikilizwa na Hakimu Mwandamizi Boniveture Lema ambapo Wakili wa Serikali Dorcas Akyoo alisema shauri hilo lilipangwa kusikilizwa February 09, 2023 kwa ajili ya kumsomea maelezo ya Mashahidi ili kulipeleka Mahakama Kuu lakini DPP amesema hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Boniveture Lema amesema kwa sasa Mshtakiwa Diana Bundala yupo huru katika kesi namba 11 ya Usafirishaji haramu wa Binadamu japokuwa ataendelea kutumikia kifungo jela kwa siku 10 zilizosalia kutokana na hukumu ya kesi yake nyingine ya kuzuia Maafisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao.

Kesi hiyo ya kuzuia Maafisa wa Serikali ilimfanya ahukumiwe mwaka mmoja jela ambapo hadi sasa ni miezi zaidi ya 11 amekua jela na zimesalia siku 10 atimize mwaka mmoja.
Screenshot_20230209_055606_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom