Makapuku Forum

Makapuku Forum

Miili ya Watu 12 wa ukoo mmoja wa Mrema kati ya Watu 20 waliopoteza maisha kwenye ajali ya gari Wilayani Korogwe Mkoani Tanga imeagwa katika Hospitali ya Huruma, Mkuu Rombo Mkoani Kilimanjaro huku Viongozi mbalimbali wakishiriki akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda.

Miili hiyo itaapelekwa katika Kanisa Katoliki Mkuu kwa ajili ya Ibada kisha kwenda kuzikwa kwenye makaburi yaliyoandaliwa.

Miili mingine ilichukuliwa na Ndugu maeneo ya njia panda ya Himo kwenda kuzikwa sehemu mbalimbali.
Screenshot_20230206_185134_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Kheri James , ameiongoza Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo kufika katika Kijiji cha Domanga ambacho hivi karibuni yalitokea mapigano baina ya Wananchi na kusababisha kujeruhiwa kwa Wananchi wawili ambapo Kamati hiyo imemaliza mgogoro huo.

Wakizungumza katika mkutano huo, Wananchi wa Kijiji hicho cha Damanga kilichopo Kata ya Hashkesh, Jimbo la Mbulu Vijijini wamesema kuwa chanzo cha mgogoro ni kuhisi kuwa zoezi la kudhibiti maeneo yaliozuiwa kwa malisho katika Kijiji hicho halisimamiwi kwa haki na usawa.

DC Kheri James ameagiza kufunguliwa kwa Ofisi ya Kijiji iliyokuwa imefungwa na kuzungushiwa miba na Wananchi wenye hasira kali na kisha amewasikiliza Wananchi wote wa Jamii ya Wahadzabe na Wadatogwa na kuwaeleza umuhimu wa kutumia vikao vyao vya Kijiji kujadili na kuamua mambo yao.

DC Kheri amewaeleza pia Wananchi hao madhara ya matumizi ya nguvu na uharibifu wa mali, kuwa vitendo hivyo havikubaliki na ni kinyume cha sheria.

Kamati ya usalama imezipatanisha pande zote mbili na imesistiza matumizi ya vikao vya kisheria kama njia ya kujadili na kuamua mambo yote yanayo husu Kijiji na Wananchi, pia Kamati imewatembelea Wananchi wawili waliojeruhiwa katika mapambano hayo ambapo hali zao kwa sasa zimeanza kuimarika na hali ya usalama katika Kijiji cha Domanga imerejea na Wanachi wameanza kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.
Screenshot_20230206_185255_OGInsta%2B.jpg
 
Watu wawili wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara wakiwa wanasafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi kiasi cha bunda 246 sawa kilo 98 katika Kijiji cha Bonga Wilaya ya Babati wakitoka Mkoa wa Arusha kuelekea Wilaya ya Kondoa, Dodoma kupitia Babati.

RPC Mkoa wa Manyara, George Katabazi amesema Watuhumiwa hao walikutwa wameficha dawa hizo kwenye bodi la gari (Fuso) ili Askari wasiwagundue kuwa wanasafirisha dawa hizo za kulevya.

"Kwa umakini mkubwa wa Askari wetu walipohojiwa walikiri kweli wao ni Wasafirishaji wa dawa hizo na wanazipeleka Wilaya ya Kondoa kwa ajili ya kuuza"

Waliokamatwa ni Dereva wa gari hilo (37) pamoja na mwenzake utingo (45) wote Wakazi wa Jiji la Arusha ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limetoa wito kwa Wamilimi wa vyombo vya moto kutojihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya ili kuepuka kutaifishwa kwa vyombo hivyo huku akiwaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
Screenshot_20230206_185608_OGInsta%2B.jpg
 
Miili ya Watu 12 wa ukoo mmoja wa Mrema kati ya Watu 20 waliopoteza maisha kwenye ajali ya gari Wilayani Korogwe Mkoani Tanga imeagwa katika Kanisa Katoliki la Mkuu Rombo Mkoani Kilimanjaro leo tayari kwenda kuzikwa kwenye makaburi yaliyoandaliwa.

Miili mingine ilichukuliwa na Ndugu maeneo ya njia panda ya Himo kwenda kuzikwa sehemu mbalimbali.
Screenshot_20230206_185730_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Mtangazaji na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Tanzania Charles Martin Hilary kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Zanzibar.

Charles ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano- Ikulu na uteuzi huo unaanzia leo tarehe 06 Febaruari, 2023.
Screenshot_20230206_185826_OGInsta%2B.jpg
 
Staa wa zamani wa vilabu ya Chelsea na Newcastle vya England Christian Atsu (31) Raia wa Ghana ambaye kwa sasa anacheza Hatayspor ya Uturuki amekwama kwenye kifusi cha jengo lililoanguka baada ya tetemeko la ardhi.

Harakati za kumuokoa Atsu zinaendelea lakini kwenye tetemeko hilo lililotokea leo nchini Uturuki mitandao mbalimbali imeripoti kuwa watu zaidi ya 1400 wamefariki Dunia.

Atsu ambaye alijiunga na Chelsea 2013 na kuishia kutolewa kwa mkopo Newcastle na Everton, alikuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu Uturuki jana kati ya timu yake ya Hatayspor dhidi ya Kasimpasa ambapo aliisaidia kupata ushindi wa 1-0 akifunga goli dakika ya 90+7.
Screenshot_20230206_185925_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230206_185943_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230206_185959_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imesema hapa nchini kuna takribani Marubani 106 kati ya hao Marubani 11 ni Wanawake na 95 ni Wanaume na hao Wanawake wana uwezo wa kurusha ndege zote.

Kati ya hao 106, Marubani 105 wote ni Watanzania na mmoja tu ndio ambaye si Mtanzania, takwimu hizo zimetolewa Bungeni Dodoma leo February 6, 2023 wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amejibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Angelina Adam Malembeka ambaye alitaka kujua hadi sasa Tanzania kuna Marubani wangapi.
View attachment 2508659
Hivi kusomea mwisho miaka mingapi auntie?
 
Moja kati ya habari kubwa tulizoanza nazo mwaka huu ni huduma ya kuwekewa puto tumboni kwa ajili ya kupunguza uzito ambayo inatolewa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na tayari Mwimbaji Peter Msechu @peter_msechu amebainisha kupungua kilo saba, siku 7 tu baada ya kuwekewa puto katika Hospitali hiyo ili kumsaidia kupunguza uzito mwilini mwake.

@ayotv_ imefika hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili - Mloganzila na kupata fursa ya kuona Mtu akiwekewa puto pamoja na kuongea na Madaktari ambao wameelezea mengi tusiyoyafahamu kuhusu huduma hiyo.

“Gharama za kuwekewa puto ni Tsh. Milioni 4.2 na tayari tumeshawawekea Watu 34 wakiwemo Watu maarufu ambao wengine hawajataka kujitangaza”

Madaktari wanasema ukiwekewa puto likiwa tumboni unaweza kufanya mazoezi na sarakasi nyingine zozote ila hautoruhusiwa kunywa bia na soda kwakuwa ukinywa vinaathiri puto na linaweza kupasuka… kuitazama video hii kwa urefu ingia Youtube ya MillardAyo.
View attachment 2508658
Auntie mnichangie hela, nawaahidi sitokunywa pombe.
 


Siyo wote wana pua hizo, sema labda wewe tu ndio umekutana na sisi wenye pua kama tundu za bunduki, ila wapo wengi tu pua zao zimekaa vizuri

Kama yule Rafiki yako SM
Ni kweli hata dada yako Mnys hana pua ya kinyakyusa.
Sasa kaka Liii alikwamba wapiii🙆🙆🙆🙆
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom