Makapuku Forum

Makapuku Forum

Msanii na Mwanaharakati wa kutetea haki za Watu wenye ulemavu wa ngozi, Babu Sikare maarufu Albino Fulani amefariki Dunia alfajiri ya leo February 08,2023.

Babu Sikare amefariki huko Columbus, Ohio nchini Marekani alipokuwa akiishi na kufanya shughuli zake za muziki.

Msanii Wakazi amesema “Amefariki Marekani alfajiri hii, alikuwa anaumwa, siwezi kuongea zaidi mpaka nipewe ruhusa na Familia na nisipopewa ruhusa siwezi kuongea cha ziada, ni Rafiki yangu wa karibu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu hali yake ilikuwa inaimarika halafu inaenda vibaya na kwa bahati mbaya amefariki”

Kwa upande wa Mwanamitindo Flaviana Matata amesema “Nimetoa pole kama Rafiki, alikuwa Mtu mwema sana, kuongea na Vyombo vya Habari niachie Familia kuheshimu privacy yake kama Familia ndio wanaweza kuongelea”
Screenshot_20230209_060021_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Viti Maalum, Sylivia Francis Sigula @sylviasigula amesema kuwa sheria ndogo ya usafi wa mazingira inayotoa katazo la Watu kufanya shughuli yoyote ya maendeleo kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa nne asubuhi siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa lengo la kufanya usafi inarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kwamba sheria hiyo imepitwa na wakati.

Sigula ametoa kauli hiyo Bungeni Dodoma leo February 8, 2023 wakati akichangia mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022.

Mbunge Sigula amesema lengo la kufanya usafi linaweza kuwa zuri lakini agizo la kuzuia Watu kufanya biashara na shughuli za maendeleo liondolewe na Watu waruhusiwe kuendelea na biashara kwakuwa kuna aina ya biashara zinatakiwa kufanyika muda huo ambao kuna zuio.

Sigula pia amesema sheria hii ndogo kwenye utekelezaji wake haiwezekani kwakuwa Watu hawaendi kufanya usafi kama ilivyotarajiwa badala yake Watu wanafunga biashara na kusubiri ifike saa nne wafungue biashara.
Screenshot_20230209_060137_OGInsta%2B.jpg
 
️ Viní Jr amefikisha mabao 50 ndani ya Real Madrid, chini ni mchanganuo wa idadi hiyo ya mabao.

️ x 31 La Liga
️ x 12 Champions League
️ x 5 Copa del Rey
️ x 1 Supercopa de España
️ x 1 FIFA Club World Cup

Miaka 22 tu na alionekana kama hafit Bernabeu, moto huu hapa
Screenshot_20230209_084834_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya sare ya Mashetani Wekundu dhidi ya Leeds United, nimegundua kuwa Manchester United bila Casemiro na Erriksen bado nina mashaka sana na eneo la Kiungo linavuja sana, Fred na Marcel walikuwa wazuri lakini sio kwa kasi ya Vijana kutoka Yorkshire.

Bwana mdogo Alejandro Garnacho is a good player lakini ni mzuri akitokea bench aje kumalizia dakika kwa umri wake nadhani mentality hiyo ni nzuri zaidi kwake.

Wout Werghost i prefer not to speak

Huu ubingwa unautaka sana Arsenal kuliko hata Arsenal wanavyoutaka.
Screenshot_20230209_085019_OGInsta%2B.jpg
 
FT| AL AHLY 1-4 REAL MADRID

️Vini Jr
️Rodrygo
️Valverde
️Arriba

️Maaloul

Madrid watacheza fainali ya klabu bingwa duniani dhidi ya Al Hilal ya Saudi Arabia.
Screenshot_20230209_085119_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Yanga Mohamed Nasreddine Nabi leo alikuwa jukwaani kwenye uwanja wa Mahdia, Tunisia akishuhudia wapinzani wake Monastir wakiwa ugenini wakiichapa Rejiche 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu.

Baada ya mchezo huo, Monastir itakutana na Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la CAF siku ya Jumapili Februari 12, 2023.

Kwenye mechi tano (5) za Ligi ya Tunisia, Monastir imeshinda mechi tatu (3), imetoka sare moja (1) na kupoteza mchezo mmoja (1) [W L D W W]
Screenshot_20230209_085304_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Yanga Mohamed Nasreddine Nabi alikuwa jukwaani kwenye uwanja wa Mahdia, Tunisia akishuhudia wapinzani wake Monastir wakiwa ugenini wakiichapa Rejiche 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu.

Baada ya mchezo huo, Monastir itakutana na Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la CAF siku ya Jumapili Februari 12, 2023.

Kwenye mechi tano (5) za Ligi ya Tunisia, Monastir imeshinda mechi tatu (3), imetoka sare moja (1) na kupoteza mchezo mmoja (1) [W L D W W]
Screenshot_20230209_085304_OGInsta%2B.jpg
 
Amir wa nchi ya Qatar, Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani ambaye pia ndie Mmiliki wa PSG ameonesha nia ya dhati ya kuinunua Manchester United na kuanza uwekezaji mara moja.
Screenshot_20230209_085532_OGInsta%2B.jpg
 
Qatar imeanza project mpya baada ya kumchukua Kocha Carlos Queiroz raia wa Ureno ambaye alikuwa Kocha wa timu ya Taifa ya Iran kwenye Fainali za Kombe la dunia 2022 nchini Qatar.

Queiroz amepewa project kuelekea Fainali za Kombe la dunia 2026 ambazo zitafanyika Marekani, Canada na Mexico.

Baada ya Qatar kuchaguliwa kuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la dunia 2022, walianzisha project ambayo ukomo wake ulifika baada ya Fainali za 2022.

Kwa hiyo Queiroz anaenda kuendelea ilipoishia project ya 2022 huku wakitaka mchezo wa soka kuwa maarufu na ushindani ndani ya Qatar.

Wenzetu tayari wameanza maandalizi ya Fainali za Kombe la dunia 2026 wakiwa wanaendelea pale walipoishia 2022!
Screenshot_20230209_085648_OGInsta%2B.jpg
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba Salim Abdallah ‘’ yupo Mjini Tangier, Morocco akihudhuria kozi ya Diploma katika Uongozi [Diploma in Club Management] ambayo inatolewa na FIFA.

Ni fursa nzuri kwa @salim_tryagain na klabu ya Simba kwa sababu matunda ya kozi hiyo yatamsaidia Mwenyekiti wa Bodi katika kuboresha uendeshaji wa timu.

Wakati kozi hiyo ya FIFA inaendelea nchini Morocco, FIFA na CAF wanaendelea na maandalizi ya Africa Super Cup michuano ambayo Simba pia itashiriki.
Screenshot_20230209_085736_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya taarifa za kuwa Christian Atsu ameokolewa kutoka kwenye kifusi, Balozi wa Ghana nchini Uturuki sambamba na Viongozi wa timu yake wamemsaka kila hospital na hakuna iliyompokea wala jina lake halipo kwenye orodha ya manusura.

Taarifa zinadai kuwa Atsu sambamba na Mkurugenzi wake bado wapo chini ya kifusi na harakati za uokoaji unaendelea.
Screenshot_20230209_112030_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya taarifa za kuwa Christian Atsu ameokolewa kutoka kwenye kifusi, Balozi wa Ghana nchini Uturuki sambamba na Viongozi wa timu yake wamemsaka kila hospital na hakuna iliyompokea wala jina lake halipo kwenye orodha ya manusura.

Taarifa zinadai kuwa Atsu sambamba na Mkurugenzi wake bado wapo chini ya kifusi na harakati za uokoaji unaendelea.View attachment 2511294
Pole yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom