Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo January 21 2023
Screenshot_20230121_072417_Opera%20Mini.jpg
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Mwanza leo kwenye Mkutano wa kwanza wa hadhara wa Chama hicho toka Rais Samia aliporuhusu mikutano ya Vyama vya Siasa amesema pamoja na kufanyika kwa maridhiano bado CHADEMA itaendelea kuwa Chama Kikuu cha Upinzani hadi hapo itakapofanikiwa kuwa Chama Tawala “Hatujaingia kwenye maridhiano kwa kukiua Chama kimoja”

“Chama hiki Mimi naweza kusema nilikuwa miongoni mwa waliokiasisi Chama chetu nikiwa Kijana mdogo wa miaka 29 kwahiyo hiki Chama nakifahamu kuliko wengi wanavyoweza kufikiria, maisha yangu kwa miaka 30 nimetumia fedha, rasilimali na nguvu zangu kukijenga Chama hichi nikijua Taasisi hii ina malengo mazuri kwa Nchi yangu na sio malengo mazuri kwa Familia yangu”

“Tumepitia Milima na madimbwi mengi leo nikisema tuna miaka 30 nazungumza kwa imani na ujasiri, tumepigana kuijenga CHADEMA, tulianza miaka 20 leo hakuna Chama cha kushindana na CHADEMA”

“Tumeteswa sana chini ya Utawala wa awamu ya tano, Viongozi wetu wameuawa, Vyama vingine vya upinzani vikabinafsishwa lakini CHADEMA tukasimama kwenye misingi ya haki ndio maana leo tunakuwa na mkutano unakuwa na Maelfu ya Watu”
Screenshot_20230122_050652_OGInsta%2B.jpg
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Mwanza leo kwenye Mkutano wa kwanza wa hadhara wa Chama hicho toka Rais Samia aliporuhusu mikutano ya Vyama vya Siasa amewapongeza Polisi Mkoani Mwanza kwa kusimamia usalama tangu kuanza kwa maandalizi hadi kufanyika kwa mkutano wa CHADEMA bila kuwakwaza Viongozi na Wanachama wa Chama hicho.

“Naomba Wana Mwanza kwa kauli moja muungane nami kulishukuru Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo kuanzia tumeanza hii mikutano ya hadhara na maandalizi yake wamesimama na sisi kuhakikisha usalama upo hawajatukwaza kwa hatua yoyote, wapigieni makofi Polisi“

“Na Polisi Ndugu zangu, nyinyi Ndugu zetu tambueni makofi haya ni makofi ya kulilia Taifa, haina maana kwamba CHADEMA leo tumekubaliana kwamba sisi ni Wateja wa Serikali lakini pale wenzetu wa upande wa pili wanapofanya jambo jema naomba Wana CHADEMA kote Nchi nzima tuwapongeze, hawa ni Ndugu zetu”
Screenshot_20230122_050911_OGInsta%2B.jpg
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Mwanza kwenye Mkutano wa kwanza wa hadhara wa Chama hicho toka Rais Samia aliporuhusu mikutano ya Vyama vya siasa amesema hajalamba asali kama baadhi ya Watu wanavyodai huku akisema amepoteza Mabilioni ya fedha kukipigania Chama hicho na hawezi kuwasiliti Wanachama kisa fedha au mali.

“Yaani mnaanza kusema eti Mbowe kalamba asali, hivi mnajua Mbowe nimepoteza Bilioni ngapi kwakuwa Mwana CHADEMA?, mnakubali kutunza propaganda za kitoto kwamba eti Mbowe kalamba asali hataki Katiba Mpya, hataki Tume huru so what?, upande wa pili naweza kuelewa vilevile hisia za Viongozi na Wanachama wa CHADEMA kwa maumivu ambayo tumeyapitia kwa muda mrefu”

“Kwahiyo wakitoka Wanachama wa CHADEMA wakahofu maamuzi ya Mwenyekiti binafsi nawaunga mkono naelewa kwasababu tumeumizwa sana, ni asilimi 2 tu ya Wanachama wa CHADEMA wanaiamini CCM lakini Mimi niliwaamini kwa kiwango fulani niliokuwa nazungumza nao”

“Tulipoanza mazungumzo tulikubalina misingi ikiwemo usiri, Wanachama wa CHADEMA wakiwemo Viongozi wangu Wakuu wakasema ‘Mbowe anafanya usiri hatuambii, yupo Ikulu kila siku, hii Mi-CCM sio ya kuiamini, kalamba asali’, yaani kama kuna kitu kimewahi kuniumiza ni kuwepo kwa Mtu anayeweza kuamini kwamba eti Mimi naweza kulamba asali nikawasaliti Watu ambao nimeteseka kwa miaka 30 kuwalinda”

“Nilisimama miaka 30 iliyopita kuitafuta haki nitasimama hapo kwa gharama yoyote, hakuna idadi ya fedha au mali itakayonifanya Mbowe niwasaliti Watanzania, nimepoteza Mabilioni ya fedha, anavyotokea Mtu anamuhukumu Mbowe eti amelamba asali, asali ipi?, nimezaliwa kwenye Familia yenye uwezo nimekua na kusimama kwenye Familia yenye uwezo lakini nimesema nitasimama na haki kwenye maisha yangu”
Screenshot_20230122_051210_OGInsta%2B.jpg
 
Marekani imelitangaza kundi la Wagner la nchini Urusi kama ‘Shirika la Uhalifu wa Kimataifa’ na hivyo kuongeza shinikizo kwa kundi hilo binafsi la ulinzi linalopigana vita nchini Ukraine.

Msemaji wa Usalama wa Taifa katika Ikulu ya Marekani White House John Kirby, amesema katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba kundi la Wagner lina Wapiganaji 50,000 nchini Ukraine ambao asilimia 80 ni Wafungwa.

Kirby ameonesha picha za kiintelijensia za Korea Kaskazini kulisambazia silaha kundi hilo kwa ajili ya operesheni zake nchini Ukraine na kuongeza kwamba Jeshi hilo binafsi limetoa ushindani kwa Jeshi rasmi la Urusi.

Kundi la ulinzi binafsi la Wagner linadhibitiwa na Mfanyabiashara Yev-geny Prigo-zhin ambaye ni Mshirika wa karibu wa Rais Vladimir Putin.

Moja ya matukio ya hivi karibuni kuhusu Jeshi hilo ni kifo cha Mtanzania Nemes Raymond Tarimo (34) ambaye ameripotiwa kufariki wakati akipigana upande wa Jeshi hilo binafsi la Urusi la Wagner Group dhidi ya Ukraine ambapo kundi hilo lilitoa video inayoonesha Nemes akiagwa na kutunukiwa nishani baada ya kufia vitani.
Screenshot_20230122_051314_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom