Makapuku Forum

Makapuku Forum

Binti mwenye umri wa miaka 17 Mkazi wa Mtaa wa Semtema Iringa amejinyonga na kufariki kutokana na msongo wa mawazo baada ya kutoelewana na Mzazi mwezie ambaye anadaiwa kutotoa hela ya matumizi ya Mtoto wao na Binti huyo ambaye alikatisha masomo akiwa kidato cha kwanza baada ya kupata ujauzito.

Mama mzazi wa Marehemu, Agness Donald amesema Binti huyo alikuwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kihesa lakini mwaka jana alipata ujauzito aliosababishiwa na Mwanafunzi mwenzie ambapo ilimlazimu kukatisha masomo yake akiwa kidato cha kwanza na hata alipojifungua hakurudi Shule.

Mama huyo amesema siku ya tukio Binti yake aliaga anakwenda kutembea lakini alichelewa kurudi na aliporudi Mama yake alimuuliza kwa nini umechelewa kurudi maswali ambayo yanaonesha yalimkera pia na baadae kujinyonga.

Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi cha Semtema, Cosmas Ngai amesema Mtoto huyo alikosa kushauriwa na kuwataka Wazazi wawe na ukaribu zaidi na Watoto wao na kuwakumbusha kuepukana na mambo nje ya umri wao.
Screenshot_20230121_042658_OGInsta%2B.jpg
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Mpango amesema uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika licha ya changamoto iliyoikumba Dunia ya UVIKO-19 na vita kati ya Urusi na Ukraine.

Ameyasema haya leo Januari 20 2023 kwenye hotuba yake ambayo iliyosomwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Angellah Kairuki katika hafla ya kuufahamisha umma mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika Mkoa wa Dodoma.

Amesema tathimini ya Benki ya Dunia inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ambapo kulingana na taarifa za Benki Kuu, katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 uchumi umekua kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 3.8 katika kipindi kama hicho mwaka uliotangulia 2021.

"Hata hivyo, kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na Serikali, tunatarajia uchumi utakua zaidi hadi kufikia wastani wa asilimia 5, nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi kubwa na mikakati thabiti inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita iliyopelekea uchumi wa nchi yetu kukua kwa viwango hivi”
Screenshot_20230121_043258_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) imemzuia Mfanyabiashara Maryam Shaaban Laurent kutoendelea kufanya biashara ya kuuza bidhaa za Lump Sugar maarufu ‘vipipi’ vinavyodaiwa kutumiwa na Wanawake kujiweka sehemu za siri ili kupata mvuto na kubana maumbile yao.

Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari, ZFDA imetoa tahadhari ya kutotumika kwa vipipi hivyo huku ikiendelea kufanya msako wa kuviondoa sokoni.

Mkuu wa Divisheni na Vipodozi ZFDA Salim Hamad Kassim amesema wanazichukua sampuli za bidhaa hiyo na kuzipeleka Maabara ili kujiridhisha huku akisema sababu nyingine ya hatari iliyopo kwenye bidhaa hiyo ni kuwa haina lebo, haina ujazo wala ‘expire date’ na vilevile haijulikani imetoka wapi

Mfanyabishara Maryam alipohojiwa ili kuelezea ‘vipipi’ hivyo amesema amekuwa akiviuza kwa njia ya mtandao ——— “Wateja wote nilikuwa najihakikishia kuwa hiki kitu hakina madhara ni cha asili ndicho kilichonitia moyo kufanya hiyo biashara na sitofanya tena hadi vikibainika havina madhara”
Screenshot_20230121_043350_OGInsta%2B.jpg
 
Club ya Singida Big Stars kwa kushirikiana na Familia ya Mchezaji Mohamed Banda leo wamekamilisha taratibu za mazishi ya Mchezaji huyo aliyekuwa Nahodha wa Singida Big Stars U-17 na kumzika kwao Mlalanda njia ya kwenda Iramba.

Mohamed Banda alifariki jana January 19, 2023 mazoezini baada ya kugongana na Mchezaji mwenzake walipokuwa wameruka juu kuwania mpira kitendo kilichopelekea kuanguka vibaya.
Screenshot_20230121_043637_OGInsta%2B.jpg
 
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimetoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuanzia leo January 20, 2023, kuhakikisha vishkwambi vilivyotolewa na Serikali kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa.

CCM imesema imepokea malalamiko ya kutotekelezwa kikamilifu kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji wa vishkwambi hivyo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Edward Mjema, alisema wakati akizundua ugawaji wa vishikwambi hivyo Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kuhakikisha vifaa hivyo vinakwenda kwa walengwa.

"Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivyo ambao ulikuwa unaishia January 15, mwaka huu, lakini Chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo.

"Kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane wawili wanaachwa”

"Chama kinatoa maelekezo, kinaielekeza wizara husika (Wizara ya Elimu na TAMISEMI) kuhakikisha zoezi hili linakamilika na walengwa wote wanaostahili kuhakikisha wamevipata vishikwambi hivyo, lakini sio hivyo tu bali pia wahakikishe malalamiko haya hayapo na wasimamie zoezi kuona makundi yaliyopaswa kupewa yanafikiwa na wale ambao hawajapata wapate. Baada ya wiki moja tupate taarifa zoezi hili limekwendaje”
Screenshot_20230121_043820_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanamke mmoja aitwaye Sabina Barma (27), Mkazi wa Kijiji cha Saidoda Kata ya Ufana Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara amekutwa amefariki dunia huku mwili wake ukiwa kitandani na majeraha sehemu mbalimbali za mwili huo.

RPC wa Manyara, George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema baada mwili kufanyiwa uchunguzi umekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili huku Mtuhumiwa wa mauaji hayo akiwa ni Mume wa marehemu ambaye ametokomea kusikojulikana.

RPC Katabazi amesema Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa wa mauaji hayo huku akiwaomba Wananchi kutoa taarifa ili kufanikisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa na kuwataka kuacha kujichukulia sheria mkononi.

@ayotv_ imefika eneo la tukio ambapo mauaji hayo yamefanyika kuzungumza na Mashuhuda wa tukio ambapo wamesema Marehemj ameacha Watoto wadogo watano huku mkubwa katika hao akiwa na umri wa miaka saba.

Tukio hilo limezua hisia wa Watu wengi baada ya Mtoto mdogo wa mwisho wa Marehemu kukutwa akiendelea kunyonya maziwa kwenye mwili wa Mama yake ambaye tayari alikuwa ameshafariki mpaka pale Watu walipokuja kumuondosha katika mwili huo.
Screenshot_20230121_043939_OGInsta%2B.jpg
 
PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Muigizaji Maarufu wa Filamu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD alipokuwa Davos nchini Uswizi.
Screenshot_20230121_044151_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni Mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye Madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe huku sababu zikiwa bado hazijajulikana.

Katibu wa Kanisa hilo, Elias Ngailo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Mwanaume huyo amekutwa akiwa mtupu amelala na kulazimika kumsaidia kumvalisha nguo na kumpeleka Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako huku wakiwa hawajui kama anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili.

"Tumemuhoji baadhi ya maswali amesema yeye ni wa Morogoro sasa umekujaje huku hawezi kujieleza ila tulifadhaika tukaona walau tumsaidie kwa kumtafutia nguo asitiri mwili wake baada ya hapo tukampeleka kwenye Vyombi vya Usalama ili wajue namna ya kumsaidia"

Mwinjilisti wa Kanisa hilo John Kisogo amesema awali baada ya kumkuta Mtu huyo katika madhabahu walilazimika pia kumfanyia maombi “Huyu Mtu alisema alijikuta tu yupo Madhabahuni tukamuuliza ulikuwa peke yako akasema nilikuwa na mwenzangu"
Screenshot_20230121_044252_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom