Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Wizara ya Afya hivi karibuni itazindua ‘Booster’ dozi ya nyongeza ya Covid-19 ili Wananchi waweze kuongeza kinga zaidi dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 na kusema kuwa ni hiari kwa Mtu yeyote kwenda kupata chanjo hiyo.

Ummy amesema kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2022 Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya wamefanikisha utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19 na kufikia asilimia 86 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kupata dozi kamili ya chanjo dhidi ugonjwa huo.

Ummy amesema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Afya kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba 2022 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Jijini Dodoma.

Ameema hadi kufikia Desemba 31, 2022 jumla ya dozi 46,848,520 zilikuwa zimepokelewa ambapo dozi 41,581,670 zilikuwa zimesambazwa nchi nzima huku kiasi cha chanjo zilizosalia kwenye bohari ya kutunzia chanjo ni 5,266,850 ambazo zote ni aina ya J.J.

Kuhusu huduma za chanjo kwa Watoto, Waziri Ummy amesema huduma hizo zimeendelea kutolewa kwa Watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja kwa chanjo ya Penta3 ambayo hutumika kama kipimo kikuu ilifikia asilimia 107 ukilinganisha na mwaka 2021 iliyofikiwa kwa asilimia 96.
Screenshot_20230121_044352_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati kukiwa na taarifa kuwa Mtanzania aliyefia nchini Russia, Nemes Tarimo, alikuwa amejiunga na vikosi vya jeshi la nchi hiyo vinavyopambana na majeshi ya Ukraine, familia yake imeiomba Serikali kueleza undani wa kifo hicho.

Nemes aliyekuwa akisoma nchini Russia anadaiwa kufariki Desemba 2022, huku baadhi ya video zilizosambaa mitandaoni zikionyesha Mtanzania huyo akipewa heshima za kijeshi.

Mwananchi limefika nyumbani kwa familia ya Nemes, Mbezi kwa Msuguri jijini hapa na kukuta wanandugu wakiwa wamekusanyika, wakisema wanasubiri taarifa ya Serikali.
Screenshot_20230121_044504_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Juventus imekatwa alama 15 kwenye ligi kuu soka nchini Italia huku baadhi ya Viongozi wake wakifungiwa, Andrea Agnelli aliyekuwa Rais amekula kitanzi cha miaka miwili huku Mkurugenzi wa Tottenham ambaye aliwahi kuhudumu Turin amepewa kifungo cha miaka miwili na nusu nje ya soka, ijapo wana nafasi ya kukata rufaa.

Sababu ya hukumu hiyo ni kukiuka kwa kanuni za mauzo na manunuzi ambapo kuna udanganyifu wa bei juu ya bei halisi ya kununua na kuuza kwa wachezaji, ambapo mamlaka nchini Italia zimebaini uovu huo.

Mkurugenzi wa Mashtaka wa FIGC, Giussepe Chine awali alipendekeza wapokwe alama tisa na endapo wakikata rufaa na kufeli basi wakatwe 15, lakini Shirikisho limechukua uamuzi tofauti na Juventus wamelimwa 15 na kwa maana hiyo wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo.
Screenshot_20230121_044614_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230121_044628_OGInsta%2B.jpg
 
Nyota Clatous Chama amesalia jijini Dar Es Salaam kutokana na sababu za kiafya ikiarifiwa kuwa baada ya mazoezi alimfuata Kocha Mkuu na timu ya Madaktari kuwa anasumbuliwa na homa, bench kwa kushauriana na Madaktari wakampa ruhusa yakusalia Dar Es Salaam kujiuguza.
Screenshot_20230121_044738_OGInsta%2B.jpg
 
Nyota wa zamani wa Barcelona na Brazil, Dani Alves amekamatwa na Polisi jijini Barcelona, Hispania kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kingono, ikisemekana alitenda tukio hilo mwezi Desemba kwenye klabu moja jijini humo.

Alves amekamatwa majira ya saa nne asubuhi kwa saa za Hispania na anashikiliwa kwenye kituo cha Polisi cha Mossis d’Esquadra de Les Corts huku ikitegemewa apelekwe Mahakamani kwa haraka.
Screenshot_20230121_044837_OGInsta%2B.jpg
 
NUNGUNUNGU KUIKOSA DODOMA
.
—Hii hapa Orodha ya Wachezaji Majeruhi wa Simba wataikosa game ya Dodoma

⌾ Henock Inonga
⌾ Jonas Mkude
⌾ Moses Phiri
⌾ Peter Banda
⌾ Clatous Chama
Screenshot_20230121_044958_OGInsta%2B.jpg
 
KINDA JOASH OUT !!
.
🟨—Hii hapa Orodha ya Wachezaji ambao hawakusafiri kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
.
⌾ Joash Onyango
⌾ Sadio Kanoute
⌾ Mzamiru Yassin
⌾ Pape Sakho
Screenshot_20230121_045102_OGInsta%2B.jpg
 
KANOUTE, MZAMIRU OUT
.
Kocha wa Simba, Robertinho inabidi aanze kukuna kichwa mapema juu ya kuziba pengo la viungo wake wa kati Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute ambao watakosekana kwenye mchezo wa Ligi Jumapili dhidi ya Dodoma Jiji kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.
Screenshot_20230121_045237_OGInsta%2B.jpg
 
KWANINI UNAFUNGWA MASHUTI YA MBALI
.
Kipa Ali Ahmada wa Azam FC amezungumzia namna anavyofungwa mabao ya mbali ambapo anasema;
.
“Mawasiliano baina ya kipa na mabeki yanatakiwa kuwa sahihi muda wote ili kipa afanye maamuzi ndani ya sekunde na kuendelea kuliweka lango salama, lakini wakati mwingine mawasiliano ya haraka yanakosekana.
.
“Sasa makosa yanapotokea matokeo ya mchezaji na kipa kutokaa sawa katika kulinda lango, juhudi za wote zinatakiwa, sio kweli kwamba naogopa mashuti ya mbali au mashuti ya chini,”
Screenshot_20230121_045702_OGInsta%2B.jpg
 
MWAMBUSI KASEPA IHEFU
.
Baada ya kimya kingi kutanda, hatimaye Kocha Juma Mwambusi ametoka hadharani na kukiri kuachana na Ihefu kwa makubaliano maalumu, huku mabosi wake wakibaki na kigugumizi.
.
Kwa muda mrefu wadau na mashabiki wengi wamekuwa na sitafahamu baina ya Mwambusi na Ihefu wakijiuliza kinachoendelea baada ya kumtangaza kwa muda mfupi kisha kupotea kikosini kimyakimya.
.
“Sitaki iongezwe au kupunguzwa, ibaki kwamba nimeachana nao lakini kwa makubaliano maalumu, ishu ya kurudi au kutorudi achana nayo,” alisema kocha Mwambusi.
Screenshot_20230121_045759_OGInsta%2B.jpg
 
Tayari wachezaji Yanick Bangala na Aziz Ki wamejiunga na wenzao katika mazoezi kuiwinda Ruvu Shooting mechi ya Ligi Kuu itakayopigwa Jumatatu Januari 23 katika uwanja wa Mkapa.

Screenshot_20230121_045900_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Jezi hii ya PSG ni templates mpya za NIKE hiyo black! Idea nyuma ya hii jezi ni miaka ya 1860 kuhusu Jiji la Paris ambapo hii timu inatokea, Paris hutambulika kama The City of Light kutokana na kuwa ni moja kati ya miji ya mwanzo kabisa kuwa na taa mjini ambazo zilikuwa zinatumia Gesi.

Hivyo PSG kwenye fourth Kit wakaja na idea kwa ajili ya Jiji lao! Rangi nyeusi kwa ajili ya kumbukumbu za mechi zote za Ulaya na kubwa zilizopigwa Parc des Princes.

Hiyo mistari ya njano ni kama miale (beams) zilizotokana na Mnara wa Eiffel ambao ndio kielelezo cha Jiji la Paris, kisha ukiitazama jezi kwa mbali ni kama umeme ikiwa na maana ya Speed (Kasi).

Ndio idea nyuma ya huo uzi wa PSG.
Screenshot_20230121_050120_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

CRISTIANO RONALDO, Kylian Mbappe alitaka kusogea wakati wapo vyumbani kabla ya kuelekea uwanjani, lakini Elders of the village wakamwambia tunajua unampenda sana Cristiano lakini huu ni wasaa wa yeye kuongea na Captain wake Sergio Ramos, tunahitaji picha ya UEFA tisa kwa usiku huu hapa Mashariki ya kati.

Picha ambayo itatukumbusha the Great European nights from the best of Siberian Europe type of climate! Picha ya usiku wa Lisbon na header ya Ramos, picha ya usiku wa kutisha ndani ya Bernabeu Ronaldo anakata kamba tatu mbele ya Wolfsburg, picha ya kutisha kuanzia Allianz Arena ilipo Bayern Munich mpaka Turin ilipo Juventus! Captain alitakiwa apate muda wa kuongea na Mwanajeshi wake, true Son of the Bernabeu.

The streets be like! Ni wakati wa S2Kizzy na Diamond wa Morogoro kupata picha ya pamoja, picha ambazo hupigwa kwa merit ila sio favor! By default the steeets of Madrid are crying! Kuanzia Concha Espina mpaka Cibeles hadi Finca nyumbani kwa Ronaldo, tulifahamu siku itafika na tutaishi kwa kumbukumbu ila gone are the days! Nani anakata vitunguu basi inatosha machozi yametoka sana, picha za kuishi zaidi ya video za utupu, picha za kuishi kama Sikinde Ngoma ya Ukaye!

Am not crying but you are! Literally th ADMN is crying! Tunatamani turudishe nyuma mshale wa saa lakini hatuwezi kubadili muda na nyakati, it was the past, tunaishi kwenye leo! Asanteni kwa kumbukumbu bora, asanteni kwa ile usiku wa Ulaya yenye ladha kuliko usiku mmoja na Giggy Money ama Hamisa, thamani ya usiku ule ni kama Watoto wa Chuo na macho matatu au Mabinti wa Uswazi wakisema Kama kweli unanipenda ninunulie chips.

Screenshot_20230121_050248_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom