STARS KUPINDUA MEZA KIBABE
.
Baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya mtoano nyumbani ikifungwa 1-0 dhidi ya Uganda, Taifa Stars leo saa 10 jioni itahitaji kupindua meza kwenye mchezo wa marudiano kuwania kufuzu CHAN ikihitaji ushindi wa mabao mawili au zaidi kufuzu.
.
TFF ilimtimua kocha mkuu, Kim Poulsen baada ya kupoteza mechi ya kwanza na Uganda kisha kumteua Mzambia Honour Janza kuwa kocha mkuu akisaidiwa na manahodha wa zamani wa Stars Mecky Mexime.
.
Stars inahitaji kufuzu fainali hizo kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo mara mbili mwaka 2009 na 2020.
.
Kila la kheri @taifastars_
View attachment 2346016