Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa mchakato wa makabidhiano ya madaraka kwa utawala mpya yanaendelea huku akisisitiza kuwa yatakuwa ya amani.
Katika hotuba yake ambayo ameitoa leo Jumatatu Septemba 5, 2022 jioni baada ya Mahakama ya Juu kuthibitisha matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais mteule William Ruto, Rais Kenyatta amesema maagizo yote ya kuwezesha mchakato huo wa kukabidhiana madaraka yameshatolewa.
"Nia yangu ni kusimamia makabidhiano ya amani kwa utawala ujao na maagizo yote muhimu ya kuwezesha mchakato huu tayari yametolewa" amesema Kenyatta wakati akitoa hutuba yake ya kwanza hadharani tangu uchaguzi ufanyike.
Rais huyo ambaye wakati wa kampeni za uchaguzi huo uliofanyika Agosti 9 mwaka huu alikuwa anamuunga mkono Odinga, amesema anaheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu wa kuidhinisha ushindi wa Ruto kama Rais mteule.
“Nilipoapishwa kuwa Rais, niliahidi kuheshimu sheria. Leo Jumatatu Mahakama ya Juuu imeidhinisha matokeo ya urais kama yalivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). Ninaheshimu uamuzi wa Mahakama” amesema
Wakati wa hotuba yake, Rais Kenyatta hakumtaja kwa jina Rais mteule William Ruto wala kumpongeza kwa ushindi wake lakini aliwapongeza Wakenya kwa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa uchaguzi na wakati matokeo yalipopingwa mahakamani.