Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nafahamu kwa wiki nzima mamilioni ya Watanzania walikua wakijiuliza hii "Kontena la Anko Tajiri" ambalo CLOUDS wanalitangaza kwa wiki nzima ni kitu gani ? ......hatimaye Kontena hilo la Kaka yake Mama a.k.a Uncle limefunguliwa leo, ni mzigo au package iliyokamilika kwa ajili ya Tamasha la FIESTA 2022.

Kwa ubunifu na staili ya kipekee CLOUDS MEDIA wamefungua kontena hilo la Uncle Tajiri Jijini Dar es salaam leo ambapo Wakali mbalimbali wa Bongofleva wameonekana wakitoka ndani yake akiwemo Marioo, Rayvanny, Kings Music, Dogo Janja, Navy Kenzo, Country Wizzy, Saraphina, Nay wa Mitego, WEUSI, Whozu, Maarifa na wengine.
Screenshot_20220905-032333_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Bondia Mtanzania @HassanMwakinyoJR_ amesema kutokana na Refa wa pambano la jana kuwa ‘unfair’ kwake, Promota Benjamin Shalom amekubali pambano hilo lirudiwe January 23 2023 vs Liam Smith.

Usiku wa Septemba 3 2022 Mwakinyo katika pambano dhidi ya Muingereza Liam Smith lililochezwa jijini Liverpool England alipoteza kwa TKO round ya 4 katika pambano la round 12 ambalo hata hivyo lilikuwa gumzo kutokana na jinsi lilivyomalizika kwa utata.

"kutokana na mchezo wa jana na kitendo cha Refa kuwa unfair kwangu kimemlazimu Promoter Benj Shalom kutupa nafasi ya re-match na Liam January 23" ——— ameandika Mwakinyo.
Screenshot_20220905-032830_OGInsta%2B.jpg
 
  • Masikitiko
Reactions: Obe
Watu wa Manchester United jitambulisheni kwa emoji tatu za kusuuza moyo tafadhali…..
Screenshot_20220905-032942_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Rapper Kanye West kupitia ukurasa wake wa Instagram leo ameupigia salute wimbo wa "essence" wa Mwimbaji wa Nigeria Wizkid ft. Tems na kusema wimbo huo ni wimbo bora zaidi katika historia ya muziki hadi sasa.

Wimbo wa "essence" ambao upo kwenye album ya nne ya Wizkid iitwayo "Made in Lagos" uliachiwa tarehe 30 October mwaka 2020 huku video yake iliyofanyika Accra, Ghana ikiachiwa April 2021 ambapo mpaka sasa wimbo huu umeshinda Tuzo 10 ikiwemo ya Best Collaboration kwenye Tuzo za BET 2022 na nominations ikiwemo ya Tuzo za 64 za Grammy.

Wimbo huu pia umetajwa kuwa wimbo wa kwanza wa Nigeria kwenye historia ya dunia kutamba kwenye chati za muziki za dunia za 100 bora za Billboard na 200 kali za Billboard.
Screenshot_20220905-033031_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma kuongeza kasi ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na kwa viwango.

“Kazi inaendelea vizuri, tunataka kazi ikamilike ikiwezekana hata kabla ya muda, Rais Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi hii ili iwanufaishe Watanzania, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunasimamia na inakamilika kwa viwango na wakati”

Amesema hayo leo Jumapili, Septemba 04, 2022 wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma, mradi huo ni sehemu ya uendelezaji wa Jiji hilo.

Waziri Mkuu amewataka pia Wahandisi Wasimamizi wa mradi huo wahakikishe wanasimamia kikamilifu Wakandarasi ili barabara hiyo iweze kujengwa kwa viwango vilivyokubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi wake.

Akizungumza na Watanzania walioajiriwa katika mradi huo, Majaliwa amewataka wawe Walinzi wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi na wahakikishe vifaa vinabaki salama “Pambaneni na wote wenye nia ya kuiba vifaa hivi, tunataka tupate barabara yenye viwango”
Screenshot_20220905-033146_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, George Chiteto amefariki dunia muda mfupi baada ya kutoa mahubiri katika Ibada ya mazishi ya Mke wa Askofu mwenzake, Hilda Lugendo iliyofanyika, Muheza mkoani Tanga.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Mndolwa aliyeongoza Misa hiyo katika Kanisa la Kristo Mfalme Muheza, ameiambia @ayotv_ kwamba walipewa taarifa kutoka Hospitali kuwa Askofu Chiteto alipatwa na mshtuko wa moyo.

“Madaktari wametuarifu kuna kitu kinaitwa cardiac arrest, alikuwa na shida ya Shinikio la Moyo na Kisukari, mwili wake utaagwa Jumatatu kisha utasafirisha kwenda Mpwapa Mkoani Dodoma”

Askofu Chiteto alikuwa akitoa mahubiri Kanisani hapo mbele ya umati wa Waombolezaji kwa kumuombea Marehemu Hilda Lugendo na alimaliza kutoa mahubiri hayo kwa kusema ‘Namatani kufa kama hivi’ ndipo alikaa na kupisha wengine na ghafla alianguka kutoka kwenye kiti alichokaa baada ya kusikia kizunguzungu kilichosababishwa na Presha na baada ya kufikishwa Hospitali ikabainika amefariki.
Screenshot_20220905-033234_OGInsta%2B.jpg
 
  • Masikitiko
Reactions: Obe
Qatar itawaruhusu Mashabiki kununua bia zenye kileo katika mechi za soka za Kombe la Dunia saa chache kabla ya kuanza na kumalizika kwa filimbi ya mwisho, lakini sio wakati wa mechi.

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limesema Mashabiki wataruhusiwa kununua bia katika maeneo maalumu yaliyotengwa katika viwanja lakini sio ndani.

Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu inafanyika kwa mara ya kwanza katika nchi ya Kiislamu yenye udhibiti mkali wa unywaji pombe, na hivyo kutoa changamoto kwa Waandaji wa hafla inayofadhiliwa na Kampuni kubwa ya bia.

Katika mashindano mengine yaliyopita, bia zilikuwa zikiruhusiwa kuuzwa ndani ya viwanja muda wote, Qatar imefanya kampeni ya miaka 12 ili kuwa Mwenyeji wa kwanza wa Kombe la Dunia katika eneo la Mashariki ya Kati.
Screenshot_20220905-033449_OGInsta%2B.jpg
 
  • Kicheko
Reactions: Obe
Wakulima watano katika Kijiji cha Mambegwa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wamejeruhiwa na Wafugaji baada ya kutokea mapigano baina ya pande hizo mbili kwa madai Wafugaji wamelazimisha kulisha mifugo kwenye mashamba ya Wakulima kwa nguvu.

@ayotv_ imefika katika Kijiji hicho na kuzungumza na majeruhi ambapo wamesema siku ya tukio Wafugaji walifika katika mashamba ya Wakulima hao na kulazimisha kuingiza kwa nguvu kwa madai tayari wameshalipia Tsh. Milioni moja kwa Viongozi bila kuwataja Viongozi hao na baada ya mabishano ndipo wakajeruhuiwa na kuvunjwa mikono na Wafugaji.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo ikamlazimu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga kufika katika kijiji hicho na kutoa maagizo kukamatwa kwa Mtendaji wa Kijini cha Mambegwa, Samson Chilendu na Mtu mmoja anayedaiwa kuwa Dalali wa Wafugaji.
Screenshot_20220905-033710_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Kikosi Kazi cha kuratibu na kukusanya maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini, kimeanza kuandaa ripoti ya majumisho ya hoja zote zilizojitokeza katika mchakato mzima wa ukusanyaji wa maoni.

Kikosi hicho kimeanza kuandaa ripoti hiyo baada ya kutumia miezi mitano kukusanya maoni hayo wakianza upande wa Tanzania Bara kabla ya kumalizia Zanzibar walikodumu kwa wiki mbili.

Akizungumza leo Jumapili Septemba 04, 2022, Mwenyekiti wa Kikosi hicho, Profesa Rwekaza Mukandala ameleza kuwa wamekuwa katika ofisi ndogo za Bunge zilizopo Dar es Salaam kuanza kuandaa ripoti hiyo na baada ya kukamilika waiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji.

Profesa Mkandala hakuweka wazi shughuli hiyo ya kuandika ripoti itadumu kwa muda gani huku akieleza bado kunakazi kubwa ya kuchambua hoja hizo ambazo wajumbe wake wanahitaji muda wa kutosha katika kuziandaa.
Screenshot_20220905-033918_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza usaili kwa wanachama wa Tanzania Bara walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala).

Usaili huo umeanza leo Jumapili Septemba 4, 2022 jijini Dodoma ambapo walioomba nafasi hizo wamejitokeza kwa wingi kufanyiwa uhakiki na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiwa na nyaraka muhimu zinazohusu sifa za kugombea nafasi hiyo.

Baada ya mchakato huo wa usaili kukamilika majina ya wagombea yatapelekwa mbele ya Kamati kuu ya Chama hicho ambapo mchujo utafafanyika kwa ajili ya kupata majina ambayo yatapelekwa bungeni kupigiwa kura na wabunge.

Wanachama 178 wa chama hicho walichukua fomu za kuomba kuwania nafasi hiyo baada ya dirisha la uchukuaji fomu kufunguliwa Agosti Mosi, 2022 na kufungwa rasmi Agosti 10 Mwaka huu.
Screenshot_20220905-034138_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Kesho Jumatatu Septemba 5, 2022 majaji saba wa Mahakama ya Juu ya Milimani nchini Kenya wanatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais mteule wa Kenya, William Ruto iliyofunguliwa na Raila Odinga.
Kupitia uamuzi utakaotolewa na Jaji Mkuu Martha Koome na majaji Philomena Mbete Mwilu, Mohamed Ibrahim, Dk Smokin Wanjala, Njoki Susanna Ndung’u, Isaac Lenaola na William Ouko utatoa uelekeo kama Ruto ataapishwa Septemba 13, 2022 kuwa Rais wa Kenya au kinara wa Azimio la Umoja, Raila Odinga atapata fursa nyingine ya kuwania urais kama matokeo yatabatilishwa au atakwenda kustaafu siasa.
Uamuzi wa kesi hiyo ya kupinga matokeo ya kura za urais utajikita kwenye mambo tisa yaliyotambuliwa kuzua utata;

1. Ikiwa mitambo ya kiteknolojia almaarufu Kiems, iliyotumika kuwatambua wapiga kura na kupeperusha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9 ilifikia ubora unaohitajika.

2. Ikiwa mtandao wa Tume ya Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ulivurugwa.

3. Ikiwa Fomu 34A zilizotumwa katika mtandao wa IEBC zilikuwa tofauti na walizopewa maofisa wa kusimamia uchaguzi katika vituo vya kupigia kura pamoja na zile walizopewa maajenti wa wawaniaji urais vituoni.

4. Ikiwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa magavana Kakamega na Mombasa, pamoja na maeneo mengine sita kuliwanyima wapiga kura fursa ya kupiga kura za urais.

5. Ikiwa kulikuwa na tofauti za kura zilizopigiwa wawaniaji urais na nyadhifa kama Ugavana, Useneta, Ubunge na Udiwani.

6. Ikiwa IEBC ilikagua, kutathmini na kutangaza matokeo ya kura za urais kwa mujibu wa Katiba.

7. Ikiwa Rais Mteule Dk William Ruto aliyetangazwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alipata asilimia 50 + 1 ya kura zilizopigwa kulingana na Kifungu nambari 138 cha Katiba.

8. Ikiwa kulikuwa na makosa ambayo yatachangia kubatilishwa kwa matokeo ya kura za urais.

9. Maagizo yanayofaa kutolewa.
Screenshot_20220905-034226_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Saa zinahesabika kufikia muda ambao majaji saba Mahakama ya Juu ya Milimani nchini Kenya watatoa hatima ya ushindi wa Rais mteule wa Kenya, William Ruto na mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Ni kesho Jumatatu Septemba 5, 2022 ambapo Jaji Mkuu Martha Koome (Pichani katikati) na majaji Philomena Mbete Mwilu, Mohamed Ibrahim, Dk Smokin Wanjala, Njoki Susanna Ndung’u, Isaac Lenaola na William Ouko wanatarajiwa kutoa uamuzi wao kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya rais yaliyompa ushindi Ruto, iliyofunguliwa na Odinga na baadhi ya watu wakipinga matokeo ya urais yaliyotangazwa na IEBC

Uamuzi wa kesi hiyo utatoa uelekeo kama Ruto ataapishwa Septemba 13, 2022 kuwa Rais wa Kenya au kinara wa Azimio la Umoja, Raila Odinga atapata fursa nyingine ya kuwania urais kama matokeo yatabatilishwa au atakwenda kustaafu siasa.
Screenshot_20220905-034311_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linadaiwa kumkamata Katibu wa Chadema wilaya ya Nyamagana, David Nyakimwe na mwanachama wa chama hicho, Oswald Mang'ombe wakati wakiendelea na maandalizi ya mkutano wa hadhara uliotarajiwa kufanyika uwanja wa shule ya msingi Mabatini jijini Mwanza.

Akizungumza leo Jumapili, Septemba 4, 2022 na Mwananchi kwa simu, Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zakaria Obadi amesema wanachama hao wamekamatwa asubuhi ya leo wakiendelea na maandalizi ya eneo ulipotakiwa kufanyika mkutano huo.

Obadi amesema pamoja na kutoa taarifa Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Nyamagana kwamba mkutano huo utafanyika leo katika viwanja vya shule hiyo lakini anashangaa kuona jeshi hilo linawakamata wanachama wake.

Mwanchi imezungumza kwa simu na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya kuhusu tukio hilo ambapo amesema hana taarifa za kukamatwa kwa wanachama hao wa Chadema kutokana na kuwa nje ya ofisi.

Msuya ameahidi kufuatilia suala hilo na kutoa mrejesho wa hatua za kuchukua atakapokuwa amejiridhisha iwapo wanachama hao wamekamatwa.

Kuhusu Chadema kutoa taarifa ya kuwepo mkutano huo, Msuya amekanusha chama hicho kutoa taarifa ya kuwepo mkutano huo huku akisisitiza kufanya mkutano wa hadhara bila kibali ni kinyume na sheria.

Screenshot_20220905-034409_OGInsta%2B.jpg
 
“Kwa niaba ya uongozi wa Yanga, wanachama na mashabiki tumepokea kwa masikitiko msiba huu. Tuendelee kumuombea huko aendako. Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele,”Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat Haji akitoa salamu za timu hiyo kwenye msiba wa aliyekuwa Dakatari wa Simba, Yasin Gembe

Screenshot_20220905-034652_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imesema ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata umeme, imeunda timu ya wataalamu ambayo iko kazini kuona uhalisia na hatimaye kuja na bei inayoendana na mazingira ya nishati hiyo hasa katika maeneo ya vijijini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma.

Amesaema kuwa huo ni miongoni mwa mikakati mbalimbali ya Wizara ya kuhakikisha inaendelea na utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Screenshot_20220905-034802_OGInsta%2B.jpg
 
Mzambia Lazarous Kambole aliyesajiliwa hivi karibuni ameondolewa kwenye usajili kumpisha Tuisila Kisinda anayetarajiwa kutua muda wowote na klabu itaendelea kuwa nae na kumlipa stahiki zote lakini hatatumika kwani Yanga tayari ina wachezaji 12 wa kigeni.

Kambole ambaye amesajiliwa kutoka Kaizer Chiefs hajapata nafasi ya kuitumikia timu hiyo kwenye mechi za mashindano kutokana na kupata majeraha kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Namungo mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Avic Town Kigamboni.

Chanzo cha kuaminika kutoka kwenye uongozi kilisema kwamba wachezaji hao ni muhimu kwa Yanga na wanafikiria lolote linaweza kutokea kabla ya usajili wa Krisimasi. Wachezaji walioko kwenye hatari ya kuwapisha Kambole na Yacouba kwenye dirisha hilo ni Lucapel Moloko na Makambo ambao wanamulikwa kwa karibu sana na Nabi.

Screenshot_20220905-034849_OGInsta%2B.jpg
 
Mwili wa mwanamke ambaye hajatambulika umeokotwa katika mtaa wa Kuzenza kata ya Nyegezi jijini Mwanza huku ukiwa na majeraha maeneo mbalimbali ikiwamo shingoni na usoni.

Mwili wa mwanamke huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35 umekutwa leo Septemba 4, 2022 huku ukionekana kuchanwa shingoni na kitu chenye ncha.

Mbali na majeraha hayo, baadhi ya sehemu ya mwili wake zimeonekana kuvunjika ikiwemo mguu wa kulia na mkono wa kushoto.

Baada ya maofisa wa polisi kuwasili katika eneo hilo walifanya uchunguzi wa awali kwenye eneo ulipokuwa mwili huo na kukuta mkasi na chupa ya pombe aina ya Valeur ambayo ilikuwa na mabaki ya kinywaji hicho ndani yake.

Akizungumza kwa njia ya simu kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Gideone Msuya amethibitisha kutokea mauaji hayo huku akisema maofisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

“Taarifa ndiyo imefikia muda huu, tunaifanyia kazi na mara uchunguzi ukikamilika tutatoa taarifa,” alisema Msuya
Screenshot_20220905-040934_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali ya Tanzania imesema asilimia 50 ya mahitaji ya mbolea ya ruzuku imeshaingizwa nchini kabla ya msimu wa kilimo wa 2022/23 kuanza.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa Serikali kutoa ruzuku katika mbolea ili kuwapunguzia wakulima bei zilizopanda kutokana na majanga ya kidunia ambapo Sh150 bilioni zilitengwa kufanikisha hilo.

Septemba 2, 2022, Tanzania ilipokea tani 31,000 ya mbolea ya kupandia aina ya DAP kutoka kampuni hiyo, katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia meli ya MV Clipper Clyde.

Katika mazungumzo yake wakati wa upakuaji wa mbolea hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema tayari tani 150,000 ya mbolea hizo ipo katika maghala mbalimbali nchini kwa ajili ya kuuzwa kwa wakulima.

Alisema Tanzania inahitaji kati ya tani 400,000 hadi 500,000 za mbolea ili kukidhi haja ya wakulima wote, kabla ya msimu kuanza tayari asilimia 50 ya mbolea hiyo imeshaingia nchini.

Screenshot_20220905-041025_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom