Makapuku Forum

Makapuku Forum

Ni mwisho wa James Mbatia NCCR-Mageuzi? Hili ndilo swali wanalojiuliza wengi baada ya chama cha NCCR-Mageuzi kuitisha mkutano mkuu jijini Dodoma wiki ijayo, lengo likiwa ni kumweka kiti moto Mbatia, aliyesimamishwa Mei 21, mwaka huu.
Kwa miezi kadhaa sasa, chama hicho kimekumbwa na mgogoro uliokigawa makundi mawili, moja linaloungwa mkono na Mwenyekiti Mbatia, la pili ni lile linaloungwa mkono na Katibu Mkuu wake, Martha Chiomba.

Kundi hilo la Martha linalomhusisha pia Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini ndilo linaloonekana kuwa na nguvu kubwa na baraka za Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini Tanzania.

Hii inathibitishwa na ukweli kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi cha Mei 21, mwaka huu kilichomsimamisha uongozi Mbatia na Makamu Mwenyekiti wake Tanzania Bara, Angelina Mtahiwa, kilihudhuriwa na Naibu Msajili, Sisty Nyahoza na alikitambua.

Wakati NCCR-Mageuzi upande unaoungwa mkono na ofisi ya Msajili ukiitisha mkutano mkuu utakaofanyika jijini Dodoma wiki ijayo, kumekuwa na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Mbatia anajiandaa kujiunga na Chadema.

Katika mitandao hiyo ya kijamii, yakiwamo makundi ya WhatsApp yenye uhusiano na Chadema, kumekuwa na wanajukwaa wanaoandika maneno kama “Karibu Chadema Mbatia”, huku wengine wakidai amekata shauri kujiunga Chadema.

Mbatia mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia hicho kinachoendelea katika mitandao ya kijamii, hakukubali wala kukataa zaidi ya kujibu kwa kifupi tu kuwa “Hilo nitalitolea ufafanuzi baadaye”.

Screenshot_20220905-041309_OGInsta%2B.jpg
 
Mwananchi limejiridhisha kwamba Mkenya huyo amepeleka rasmi barua Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF) akiomba kutengua mkataba wake na Simba kwa kile kilichoelezwea kwamba haoni kesho yake kwenye kikosi cha kwanza cha Zoran Maki.

Mitandaoni mashabiki wamekuwa wakikejeli kwa kumhusisha na ujio wa Kisinda Yanga ingawa Mwanaspoti linajua kwamba Onyango analazimisha kuondoka Simba baada ya kuona kuna ugumu wa kupata namba mbele ya Mohammed Outtara ambaye ni chaguo la Kocha.

Lakini Simba ingawa wako kimya, wameshtukia kwamba Onyango anafosi kuondoka baada ya kupata ofa ya kimyakimya kutoka kwa vigogo wa Singida Big Stars walioanza msimu kwa moto.
Screenshot_20220905-041405_OGInsta%2B.jpg
 
Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, iliyoketi kwa siku mbili mfululizo imewapitisha Ado Shaibu na Pavu Abdallah kuwania nafasi ya ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala) kwa tiketi ya chama hicho.


Kamati Kuu hiyo iliketi kuanzia Septemba 2 na 3 Jijini Dar es Salaam, ilichagua Shaibu (Katibu mkuu wa ACT-Wazalendo) kwa upande wa Tanzania Bara pna Pavu kutoka Zanzibar watakaoipeperusha bendera ya chama hicho.


Katibu wa Katibu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Mohammed Masaga ameiambia Mwananchi leo Jumapili Septemba 4, 2022 kwamba Shaibu na Pavu walichaguliwa jana.
Screenshot_20220905-041548_OGInsta%2B.jpg
 
Mimi huwa sipendelei sana kuchat yaani napenda kupiga simu zaidi, Mimi Rasta hizo bucha za nyama situmii
Screenshot_20220905-041907_OGInsta%2B.jpg
 
Hakika.. LIMEKUFA JITU !!
.
FT: MAN UNITED 3-1 ARSENAL
35’—️ Antony
60’—️ Saka
65’—️ Rashford
75’1-️ Rashford
Screenshot_20220905-042048_OGInsta%2B.jpg
 
Hii Pacha Balaa tupu EPL
.
◉ Kinara wa mabao EPL msimu huu
️ 10– Erling Haaland
.
◉ Kinara wa Assits EPL msimu huu
04– Kevin De Bruyne
Screenshot_20220905-042217_OGInsta%2B.jpg
 
STARS KUPINDUA MEZA KIBABE
.
Baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya mtoano nyumbani ikifungwa 1-0 dhidi ya Uganda, Taifa Stars leo saa 10 jioni itahitaji kupindua meza kwenye mchezo wa marudiano kuwania kufuzu CHAN ikihitaji ushindi wa mabao mawili au zaidi kufuzu.
.
TFF ilimtimua kocha mkuu, Kim Poulsen baada ya kupoteza mechi ya kwanza na Uganda kisha kumteua Mzambia Honour Janza kuwa kocha mkuu akisaidiwa na manahodha wa zamani wa Stars Mecky Mexime.
.
Stars inahitaji kufuzu fainali hizo kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo mara mbili mwaka 2009 na 2020.
.
Kila la kheri @taifastars_
Screenshot_20220905-042325_OGInsta%2B.jpg
 
AUBA KAPEWA JEZI YA GUNDU
.
Mwamba Pierre-Emerick Aubameyang amechukua jezi Namba 9 inayotajwa kuwa na gundu kwenye kikosi cha Chelsea.
.
Auba amechukua jezi Namba 9, ambayo imedaiwa kuogopwa na wengi kwenye kikosi hicho cha Chelsea, huku kocha Thomas Tuchel akikiri kwamba namba hiyo inaogopwa, hakuna anayeitaka. Romelu Lukaku alikuwa wa mwisho kuvaa Namba 9.
.
Wengi waliovaa jezi hiyo ikawa chungu ni Steve Sidwell, Franco Di Santo, Fernando Torres, Radamel Falcao, Alvaro Morata na Gonzalo Higuain aliishia kufunga mabao matano.
Screenshot_20220905-042410_OGInsta%2B.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lee

Similar Discussions

Back
Top Bottom