Makapuku Forum

Makapuku Forum

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema huduma ya umeme ambayo ilikua imekosekana kwenye maeneo yote ya mikoa yaliyokuwa yameathirika tayari imerejea "Shirika linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza"
Screenshot_20220614-035729_OGInsta%2B.jpg
 
Bondia Mtanzania anayeishi nchini Sweden Awadhi Tamim amemtwanga Bondia Shkelqim Ademaj wa Ujerumani kwa TKO katika pambano la raundi 10 lililofanyika Essen nchini Ujerumani.

Awadh Tamim ameshinda taji lililokuwa wazi la World Boxing Foundation (WBF International) mjini Essen Ujerumani, kwa kumpiga Shkelqim Ademaj kwa Technical Knock Out katika raundi ya kumi ambapo mpinzani wake alishindwa kuendelea na pambano hilo.

Awadhi Tamim alianza kwa kumlambisha sakafu Ademaj katika raundi ya sita lakini baadae aliamka na kuruhusiwa kuendelea na pambano, Tamim aliongoza kwa pointi wakati wote wa pambano hilo hadi lilipovunjwa kutokana na Ademaj kushindwa kuendelea, Awadhi Tamim anasema huu ni ushindi muhimu zaidi kwake.

Hivi Karibuni Bondia huyo alikutana na kuzungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango alipokuwa ziarani nchini Sweden ambapo alimueleza juhudi zake katika kuitangaza Tanzania kupitia mchezo huo wa ngumi pia alimuahidi kuiwakilisha vema Tanzania katika pambano hilo la uzito wa juu lililofanyika Ujerumani.
Screenshot_20220614-042001_OGInsta%2B.jpg
 
Yanga imemuongezea mkataba Mchezaji wa Kimataifa Farid Mussakwa miaka miwili mingine huku Mchambuzi wa habari za michezo Oscar Oscar akiungana na Farid kama Meneja wake.

“Oscar ana exprience ya mpira, ana exposure passport yake imegongwa ameenda Marekani na Ulaya atamconnect na Dunia na Oscar anajua kiingereza vizuri, nyie Wachezaji mambo ya kuchukua Meneja kiingereza chenyewe anababaisha Dunia haiwezi kwenda" asema Msemaji wa Yanga Haji manara
Screenshot_20220614-042105_OGInsta%2B.jpg
 
Meya wa zamani wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu aliyevuliwa wadhifa huo baada ya kupigiwa kura za siri na madiwani za kukataliwa amejitokeza tena leo kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi hiyo.
Screenshot_20220614-042235_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kutoa uamuzi mdogo Juni 22, 2022 wa mapingamizi yaliyowasisilishwa na Mawakili wa CHADEMA katika kesi ya maombi yaliyowasilishwa na Wabunge 19 waliovuliwa uanachama na CHADEMA wakiongozwa na Halima Mdee.

Mbali na hilo, Mahakama hiyo inatarajia kusikiliza maombi mengine ya kuiomba Mahakama iweke zuio la kutokuchukuliwa kwa hatua zozote dhidi ya Wabunge hao hadi pale ambapo maombi yao ya msingi yatakapoamuliwa.

Halima Mdee na wenzake walifungua maombi hayo mahakamni hapo kwa nia ya kuiomba mahakama itoe kibali cha wao kufungua kesi ya kupinga mchakato wa kuvuliwa uananachama wao.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Jaji John Mgetta baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwa takribani saa 6 kuanzia saa 6 mchana hadi saa 12 jioni.
Screenshot_20220614-042339_OGInsta%2B.jpg
 
Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) leo umetangaza kufikia makubaliano na Kampuni ya Azam Marine kutoa huduma ya kuvusha Abiria kati ya Magogoni na Kigamboni ili Wananchi wapate huduma ya uhakika wakati huu ambao Wakala unaendelea kufanyia matengenezo vivuko vyake “Tunawashauri Wananchi wasitumie mitumbwi kwa ajili ya usalama wao”
Screenshot_20220614-042441_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom