Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara leo June 13 imemuhukumu John Simon (42) mkazi wa Dareda Babati kifungo cha miaka 20 kwenda jela kwa kosa la kukutwa na ngozi ya Chui ambayo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 8.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo 19/02/2021 katika Kijiji cha Mandi Babati ambapo wakili wa serikali Grace Mgaya amesema mshtakiwa huyo John Simon alimtegeshea Felisian Mobeshi (57)ngozi hiyo ya Chui kwenye mahindi na kisha kuipeleka nyumbani kwa Felisian na baadae kutoa taarifa Polisi.

Mgaya amesema baada ya uchunguzi imeonekana kuwa mshtakiwa John Simon sio mara yake ya kwanza kutegeshea wenzake nyara za Serikali na baadaye kutoa taarifa Polisi kwamba Wahusika wamekutwa na nyara hizo za Serikali kwa lengo la kijipatia kiasi cha shilingi laki moja.

Pia Wakili Mgaya amesema Mshtakiwa huyo amekuwa akitumwa na Mtu aliyefahamika kwa jina la Petro Damas kuweka mitego hiyo kwa Watu ambao amegombana nao kwa lengo la kuwakomesha na baadae kulipwa laki moja baada ya kutekeleza agizo hilo.

"Amekuwa anatumwa kwenda kutegesha mitego(nyara za Serikali) kwa Watu ambao wamekuwa na kutokuelewana na Petro Damas alafu yeye mwenyewe anapiga simu Polisi kutoa taarifa akieleza kwamba nyumba fulani kuna nyara za serikali sehemu fulani ambapo kiuhalisia nyara hizo anakuwa ametegesha yeye mwenyewe kwa tamaa ya kupata laki moja aliyoahidiwa lakini mwenzake huyo Petro Damas amekimbia kusiko julikana" Mgaya

Hukumu hiyo imetolewa leo June 13 katika Mahakama hiyo ya wilaya na hakimu Victor Kimario kwenda jela miaka 20 ila mshtakiwa anayo haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia leo June 13.
Screenshot_20220614-042545_OGInsta%2B.jpg
 
VIDEO: CCM Mkoa wa Mjini Znz imemfukuza Uwanachama Mwanasiasa Baraka Shamte ikisema ni sababu amekashifu madaraka ya Rais Dr. Hussein Mwinyi hadharani.

Uamuzi huu umekuja baada ya Shamte kuzungumza mambo mbalimbali na video yake kusambaa huku moja ya kauli zake ikisema “ukitaka utajiri acha uongozi ukafanye biashara, miiko ya uongozi haifuatwi”

Imeelezwa kwamba Mzee Baraka Shamte amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja Zanzibar kutokana na kupigwa na Watu wasiojulikana ambapo Polisi Znz leo wamekiri kupokea taarifa za kujeruhiwa kwa Mzee huyu mwenye umri wa miaka 83 akiwa eneo la Unguja Ukuu.
Screenshot_20220614-042658_OGInsta%2B.jpg
 
Ili kuendelea kuwapa wananchi huduma huduma ya uhakika, kwenye safari za Magogoni na Kigamboni Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Tamesa) imefikia makubaliano na kampuni ya Azam marine ya kuvusha abiria.

Siku za hivi karibuni wananchi wanaokaa Kigamboni na vitongoji vyake, walipata adha ya usafiri baada ya kivuko cha Mv Magogoni kuharibika na kushindwa kufanya safari zake kama ilivyo kawaida.

Hali hiyo ilisababisha kivuko cha Mv Kigamboni kuelemewa na abiria walikuwa wakivuka kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili, huku wakijazana, ambapo magari yakizuiliwa kuvuka kutokana na kivuko hicho kuwa kidogo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Juni 13, 2022 na kitengo cha masoko na uhusiano Tamesa imeeleza kuwa, imefikia makubaliano na kampuni hiyo wakati wakiendelea kufanyia matengenezo vivuko vyake.

Aidha katika taarifa hiyo Tamesa imewashauri wananchi kuacha kutumia mitumbwi ili kulinda usalama wao.
Screenshot_20220614-051822_OGInsta%2B.jpg
 
MOSIMANE NDO BASI TENA AL AHLY
.
Klabu ya Al Ahly imekubali ombi la kocha Pitso Mosimane la kutaka kuondoka baada ya mafanikio aliyopata na timu hiyo. Katika kikao kilichokaa kimekubaliana kwa pande zote kuwa Mosimane ataacha kazi hiyo na wamemtakia kila la kheri.
.
Mosimane ameshinda mataji 5 tangu ajiunge na timu hiyo 2020 yakiwemo ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara 2, Egyptian Cup mara moja na Caf Super Cup mara mbili.
Screenshot_20220614-052019_OGInsta%2B.jpg
 
KELVIN AITWA MAPEMA GENK !!
.
Mara baada ya mapumziko yake kumalizika, mshambuliaji kinda wa Tanzania Kelvin John ambaye alikuwa akichezea kikosi cha vijana cha KRC Genk, ametakiwa kuripoti mapema kwenye kambi ya kikosi cha kwanza cha KRC Genk kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Screenshot_20220614-052131_OGInsta%2B.jpg
 
Simba imeshinda tuzo ya Klabu Bora kwenye Mitandao ya Kijamii Tanzania ambayo imetolewa na kampuni ya Serengeti Bytes.

Simba imeshinda tuzo hiyo baada ya kuvishinda kura vilabu vya Azam FC, Mbeya City, Ruvu Shooting na Yanga SC.

Hongereni sana
Screenshot_20220614-052357_OGInsta%2B.jpg
 
Inasemekana kuwa Bayern Munich wapo kwenye hatua za mwisho za kuinasa saini ya Msenegal Sadio Mane kutoka Liverpool, baada ya Liverpool kupata mbadala wake Darwin Nunez

Uwezekano mkubwa ni Mane kujiunga na miamba ya soka ya Ujerumani kabla ya mwezi Julai
Screenshot_20220614-052632_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom