Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220608-064126_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20220608-064411_Opera%20Mini.jpg
 
Imeandikwa na @swalehmawele

Taifa Stars vs Algeria ( Afcon 2023 Qualifier ).

Kinyumbani zaidi.

Ni mechi ngumu, Taifa Stars itacheza katika ardhi ya nyumbani lakini inakwenda kuingia kama second team mbele ya Algeria ambayo ina kila kitu katika kikosi chao, quality, uzoefu na
form yao katika mechi zao za hivi karibuni.

Taifa Stars inaweza kufunguka mbele ya Algeria? bila shaka ingawa ni hatari mbele ya timu ambayo ina ubora mkubwa katika kuzitumia side ways ( maeneo ya pembeni ) na ubora wa mtu kama Baghdad Bounedjah katika kucheza aina hiyo ya mpira, Djamel Belmadi anafanikiwa.

Kitu kimoja tu kwa wachezaji wa Taifa Stars, uoga wa mechi unaopelekea mipira mingi kupotea hasa kwenye eneo la kiungo, Algeria ni timu hatari kwenye turn overs ( wanapoupora mpira ), kasi, uwezo wa kufungua patterns za ulinzi kwa wapinzani ndio silaha yao nyingine katika kupata matokeo.

Algeria wameshinda michezo mitatu katika mitano ya mwisho, wamepoteza mmoja na sare moja, wamekuwa bora katika kuzuia wakipata cleansheet nne, inahitaji ubora katika kutumia madhaifu machache yatakayojitokeza, si timu inayokuruhusu uwafikie mara nyingi katika eneo lao la mwisho, mtego wa mechi uko hapa.

Kila la kheri kwa Taifa Stars.View attachment 2253809
allez,stars
 
Wizara ya Afya imetoa taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa Covid-19 nchini katika kipindi cha kuanzia tarehe 05 Mei hadi 03 Juni 2022 ambapo kipindi hicho, jumla ya maambukizi mapya 161 yamethibitika ikilinganishwa na maambukizi 68 kwa kipindi cha tarehe 02 Aprili hadi 4 Mei 2022.

Ongezeko hili ni sawa na asilimia 137, Aidha, katika kipindi cha miezi miwili mfululizo hakuna kifo kilichoripotiwa, halii hii inaashiria kuwa maambukizi yameanza kuongezeka katika jamii.

"Mchanganuo wa idadi ya waliothibitika katika kipindi cha tarehe 05 Mei hadi 03 Juni 2022 inaonesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam uliripoti maambukizi 130, Arusha (10), Mwanza (5), Shinyanga (4), Mtwara (3), Dodoma (2), Mara (2), Morogoro (1), Simiyu (1), Katavi (1), Kilimanjaro (1) na Mbeya (1), jumla ya wagonjwa watatu (3) waliothibitika kuwa na Covid-19 walilazwa na wote walikuwa hawajapata chanjo"

"Kwa takwimu hizi, inaonyesha kuwa, chanjo ni kinga dhidi ya madhara ya Covid - 19, Serikali imeendelea kutoa huduma za chanjo nchini ili kuwezesha wananchi kupata kinga dhidi ya ugonjwa huu"

"Kuanzia tarehe 05 Mei hadi 03 Juni 2022 jumla ya wananchi waliopata dozi kamili ya chanjo ya Covid 19 ni 775,680, Wizara inaendelea kuwasisitiza wananchi kupata na kukamilisha dozi za chanjo ili kuzuia kupata ugonjwa mkali hata kifo pale Mtu anapopata maambukizi" Mganga Mkuu wa Serikali Dr. Aifello SichwaleView attachment 2253770
Huh!! Korona tena!
 
Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Henry Maganga akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 ameitaka Serikali kufungulia zaidi pesa ili hata wale Wanyonge wapate.

"Kweli tunasema hali sasa hivi ina unafuu lakini hali bado ni ngumu Waziri wa fedha angalia kama kuna sehemu yoyote fungulia pesa ili kusudi zifunguke hata kwa wanyonge zijae mifukoni maana kwenye kampeni huwa tunasema tunawapigania wanyonge sasa wanyonge hawajapata hela bado"

"Tunashukuru kwa jitihada mnazozifanya, tumeona kwa watumishi mmeongeza mishahara, watumishi wanafurahi lakini kuna wengine hawana nafasi ya kuingia kwenye manufaa haya, kwa hiyo ni vyema Waziri kwa kuwa wewe ni msomi mzuri jaribu kufikiria jinsi gani unaenda Taifa kulisaidia ili kila mtu apate haki yake" ——— Mbunge Nicodemus Maganga. View attachment 2253771
Akifungulia kwa watumishi basi na kwa wengine pia kafungua. Hivyo waongezepo kale kaasilimia tena na kakodi kapungue
 
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limetaja majina tisa ya watuhumiwa waliokutwa na viungo vilivyodhaniwa kuwa vya binadamu katika taarifa iliyotolewa mnamo Juni 02, 2022 ikiwa viungo hivyo ni mbavu na mguu mmoja.

Majina hayo yalihifadhiwa kwa lengo la kuondoa hofu ya kuharibu upepelezi wa kesi hiyo iliyoanza kufanyiwa kazi Mei 30,2022 lakini sasa RPC Kigoma ACP James Manyama amewataja Watuhumiwa waliokuwa ndani ya gari aina ya Probox T948 DQU kuwa ni Miraji Nyambi (45) ambaye ni Mwalimu wa sekondari ya Mwandiga Kigoma, dereva wa gari hilo Thobias Fundo (33) mkulima kutoka Muyama wilayani Buhigwe pamoja na Mathayo Ndayishimiye (40) Mganga wa kienyeji kutoka Katue nchini Burundi.

Waliopatikana wakati wa upepelezi ni pamoja na Bankana Zakayo (41) mwalimu wa sekondary ya Mwandiga ambaye kwa sasa anaishi Nyehunge wilayani Sengerema, Ramadhan Abrahaman (52) mganga wa kienyeji kutoka Swaga mkoani Mwanza, Nguno Manyanza kutoka wilaya ya Geita na Kelvin Fedha mkazi wa Nyehunge.

Kamanda amewataja wengine kuwa ni Adizino John (62) mkazi wa Matiazo mkoani Kigoma, James Kibeba (68) kutoka Kasulu.

"Kaburi lilifukuliwa kuwa ni lla Bilihanyuma Suminda (90) aliyefatiki mnamo January 2022 wilayani katika kijiji cha Migongo wolayani Buhigwe, alifariki kwa marazi ya kawaida na kwa tukio hilo tumewashikilia jumla ya washitakiwa Tisa na tunakamilisha taratibu ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani." View attachment 2253773
Huu ukanda jamani
 
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha mika 30 na fidia ya Tsh. Milioni 1 Mfanyabiashara Kaloli Mkusa (30) mkazi wa kijiji cha Msisina kwa kosa la kumbaka Mama yake Mzazi, hata hivyo Mtuhumiwa na Baba yake Joseph Mkusa ambaye alimuwekea dhamana wametoweka kusikojulikana na hati ya kukamatwa tayari imetolewa.

Akitoa Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Emmy Msangalufu amesema Mtuhumiwa alifanya tukio hilo May 07,2021 ambapo siku ya tukio Mtuhumiwa alikwenda nyumbani kwa Mama yake majira ya usiku na kuvunja mlango huku akiwa ameshika panga na kumtisha kumkata kwa kumpiga na ubapa wa upanga.

Licha ya Mama yake kumsihi asifanye hivyo lakini Mtuhumiwa aliendelea na kumbaka Mama yake mpaka alipomaliza, baada ya tukio Mama alitoa taarifa kwa majirani baadae Serikali ya Kijiji ndipo taratibu za kumkamata zikafanyika.

Tukio Hilo linasadikiwa ni kutokana na Imani za kushirikiana kutokana na biashara ya Mtuhumiwa kuyumba, Mtuhumiwa alikuwa akifanya biashara zake Tunduma Mkoani Songwe na alirudi akafikia kwa Baba yake ambaye anaishi nyumba tofauti na Mama yake kutokana na kupeana talaka.

Hata hivyo hati ya kukamatwa ilitolewa Tareh 09/03/2022 lakini mpaka Sasa Mtuhumiwa pamoja na Baba yake aliyemuwekea dhamani hawajulikani walipo, kwa mujibu wa Mahakama kifungo hicho kitaanza kutumika pindi Mtuhumiwa atakapokamatwa.
View attachment 2253775
Auntie hii umechelewa kuileta.
 
Yaani nilivyotupa simu, nikajua Leo napelekwa Indira Gandhi St, kwa maneno

Miss you sana mama Muinjili
Hapana aiseee mama mchungaji ukiona naongea sana ujue nimechokozwa na nina vidhibiti ila me ni binti mpole sana

Kingine una hekima sana na busara nakupenda bure nilikuona sehemu unampa mtu ushauri aisee nikasema mama mchungaji kamaliza mwenye kusikia na asikie
 
INJINIA KUCHUKUA FOMU YA URAIS LEO
.
Dk Mshindo Msolla amewaambia watu wake wa karibu lazima awanie tena kuendeleza mafanikio yake ya msimu huu. Hata hivyo, Msolla atakuwa na vita nzito kutokana na majina ya vigogo ambayo nayo yanakitaka kiti hicho.
.
Injinia Hersi Said ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, baada ya kuiwezesha Yanga kupitia nafasi yake ndani ya GSM na kamati ya mashindano sasa anataka kiti cha urais wa klabu hiyo na wakati wowote kuanzia LEO atatua Makao Makuu kuchukua fomu.
Screenshot_20220608-094324_OGInsta%2B.jpg
 
Hapana aiseee mama mchungaji ukiona naongea sana ujue nimechokozwa na nina vidhibiti ila me ni binti mpole sana

Kingine una hekima sana na busara nakupenda bure nilikuona sehemu unampa mtu ushauri aisee nikasema mama mchungaji kamaliza mwenye kusikia na asikie
Siku nikikuchokoza, unifuate tu PM kimyakimya mama Muinjili😂😂😂😂.

Kwa kweli huna baya na mtu mtoto mtoto mlito. 🙏🙏🙏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom