Makapuku Forum

Makapuku Forum

Vinara wa muda wote kwenye chati ya Ufungaji mabao kwenye Timu za Taifa.
.
CR7 on Top
Screenshot_20220608-040940_OGInsta%2B.jpg
 
EDO: Kando ya kipaji soka linahitaji juhudi Kubwa
.
“Yanga wametoka kumuongezea mkataba Kibwana. Ni mchezaji wa kwanza kuongezewa mkataba kabla ya kina Bakar Mwamunyeto na Zawadi Mauya. Kwanini? Kwa sababu amejitokeza kuwa mchezaji muhimu katika kikosi chao. Anajituma sana. Ilidhaniwa kwamba ujio wa Djuma Shaban ungemuondoa kikosini. Matokeo yake Kocha Nasreddine Nabi akamhamishia upande wa kushoto na bado anapiga kazi.”
.
- Edo Kumwembe
Screenshot_20220608-041046_OGInsta%2B.jpg
 
FEITOTO AWASHTUA WAARABU
.
Confirmed: Klabu ya Yanga imepokea ofa mbili kutoka vilabu vya Morocco vikiitaji huduma ya kiungo Feisal Salum Feitoto (24) ila kipaumbele chao sio kumuuza kwa sababu wana malengo ya kufanya makubwa CAF.
.
Hata hivyo taarifa za ndani zinasema bado hawajafunga milango yote wapo tayari kusikiliza ofa nono, endapo watakuwa na uhakika kumpata mchezaji wa kuziba pengo lake.
.
WANANCHI mnasemaje __!!
Screenshot_20220608-041331_OGInsta%2B.jpg
 
MPOLE: Nikipata nafasi nitafunga
.
Mchezaji aliyefunga bao pekee la Tanzania katika mchezo uliopita, George Mpole amesema kazi yake kubwa ni kutumia vyema nafasi atakazozipata katika mchezo wa kesho dhidi ya Algeria endapo atapata nafasi.
.
“Mimi ni mshambuliaji na lengo langu ni kuwapa raha Watanzania kwa kushinda kila mechi. Tunajiandaa kufanya vyema mechi hiyo ardhi ya nyumbani,” amesema Mpole.
.
Screenshot_20220608-041527_OGInsta%2B.jpg
 
DUH !! MAELEKEZO YA CAF TFF WAJITAFAKARI
.
Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, limetoa maelekezo kwa vyama wanachama wake ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwamba mwisho wa kuwasilisha majina ya klabu na wachezaji wao kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Afrika msimu ujao ni Juni 30, 2022. Baada ya hapo hakutakuwa na klabu itakayopokewa na wala wachezaji watakaoruhusiwa kushiriki mashindano ya Afrika.
.
Hii ina maana kwamba Tanzania inaweza kukosa wawakilishi wa mashindano ya Afrika msimu ujao kama msimu wake wa soka hautakamilika ndani ya muda huo. Hadi sasa kwa mujibu wa ratiba ya TFF, msimu wa Tanzania utakamilika Julai 2 kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.
.
Yaani fainali ya Shirikisho ambayo itamtoa mshiriki wa Kombe la Shirikisho la Afrika itafanyika nje ya tarehe rasmi ya CAF. Hii ni changamoto kubwa INASIKITISHA..
Screenshot_20220608-041643_OGInsta%2B.jpg
 
CLARA: Mimi ni mwanamke napiga kazi !!
.
Clara Luvanga ni kati ya wachezaji walioonyesha mchango mkubwa wa kuisaidia timu ya Serengeti Girls kufuzu kucheza michuano ya Dunia, itakayofanyia nchini India 2022.
.
Amejibu swali la wanahabari waliomuuliza anachukulia mashabiki wanapomuona kama mwanaume? Amejibu "Naona ni moja ya njia ya mafanikio yangu, najijua ni mwanamke hizo nyingine ni changamoto tu.
.
Ameongeza "Wakati tulivyokwenda Cameroon walinikagua wakanikuta mimi ni mwanamke, sikutaka kuliweka hilo akilini maana lingeweza kuniondoa kwenye ari ya mchezo, nilichukua kama changamoto ya kupita na imepita,"
Screenshot_20220608-041858_OGInsta%2B.jpg
 
MATIC AS ROMA
.
Inaripotiwa kwamba tayari mabosi wa AS Roma wameshamalizana na kiungo wa Manchester United na Serbia Nemanja Matic, 33, na supastaa huyo anasubiri mkataba wake umalizike ifikapo mwisho wa mwezi huu ili atangazwe rasmi kuwa mchezaji wa AS Roma.
.
Matic ni aina ya wachezaji ambao kocha wa Roma, Jose Mourinho amekuwa akiwahusudu kuwa kwenye timu anayoifundisha.
Screenshot_20220608-042424_OGInsta%2B.jpg
 
BALE: OFA MBONA ZIPO TU
.
Supastaa Gareth Bale amesema hatapata changamoto ya kutafuta timu ya kuchezea msimu ujao kwani ana ofa nyingi mezani zinamsubiri baada ya kuondoka Real Madrid.
.
Kauli ya Bale imekuja baada ya kuisaidia Wales kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika Qatar mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu 1958.
.
Gareth Bale kaichezea Real Madrid mechi 258 na kuifungia mkubwa mabao 182 kwa misimu 8.
Screenshot_20220608-042515_OGInsta%2B.jpg
 
Inaki Williams amewasili nchini Ghana ambapo ni taifa lake la asili, huku tetesi zikisema huenda akabadili uraia na kuitumikia timu ya taifa ya Ghana

Ikumbukwe nyota Tariq Lamptey tayari amekamilisha kila kitu kwa ajili ya kuiwakilisha Ghana, Hudson Odoi na Eddie Nketiah wapo pia kwenye hatua za mwisho
Screenshot_20220608-042637_OGInsta%2B.jpg
 
Ndani ya kipindi cha miezi 6 tumeweza kusajili Wanachama 34,650 na kukusanya mapato ya Tsh. Bilioni 1.07

Mikoa inayoongoza kwa Usajili wa Wanachama kwenye mfumo wetu wa Usajili wa Kidigitali.

  • Dar es salaam 12,124
  • Mwanza 1,982
  • Mbeya 1,655
  • Dodoma 1,521
  • Morogoro 1,410
  • Pwani 1,341

-Mohammed Saleh, Mkurugenzi Mtendaji Kilinet
Screenshot_20220608-042814_OGInsta%2B.jpg
 
Imeandikwa na @swalehmawele

Taifa Stars vs Algeria ( Afcon 2023 Qualifier ).

Kinyumbani zaidi.

Ni mechi ngumu, Taifa Stars itacheza katika ardhi ya nyumbani lakini inakwenda kuingia kama second team mbele ya Algeria ambayo ina kila kitu katika kikosi chao, quality, uzoefu na
form yao katika mechi zao za hivi karibuni.

Taifa Stars inaweza kufunguka mbele ya Algeria? bila shaka ingawa ni hatari mbele ya timu ambayo ina ubora mkubwa katika kuzitumia side ways ( maeneo ya pembeni ) na ubora wa mtu kama Baghdad Bounedjah katika kucheza aina hiyo ya mpira, Djamel Belmadi anafanikiwa.

Kitu kimoja tu kwa wachezaji wa Taifa Stars, uoga wa mechi unaopelekea mipira mingi kupotea hasa kwenye eneo la kiungo, Algeria ni timu hatari kwenye turn overs ( wanapoupora mpira ), kasi, uwezo wa kufungua patterns za ulinzi kwa wapinzani ndio silaha yao nyingine katika kupata matokeo.

Algeria wameshinda michezo mitatu katika mitano ya mwisho, wamepoteza mmoja na sare moja, wamekuwa bora katika kuzuia wakipata cleansheet nne, inahitaji ubora katika kutumia madhaifu machache yatakayojitokeza, si timu inayokuruhusu uwafikie mara nyingi katika eneo lao la mwisho, mtego wa mechi uko hapa.

Kila la kheri kwa Taifa Stars.
Screenshot_20220608-042928_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom