Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,971
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammedi Mchengerwa Bungeni Dodoma leo amesema "Katika kipindi hiki mafanikio lukuki yamepatikana kupitia BAKITA, naweza kujinasibu kuwa matumizi ya Kiswahili yanazidi kukubalika kitaifa, kikanda na kimataifa ambapo jitihada hizo kwa kipindi cha mwaka 2021/22 zimezaa matunda kwa Kiswahili kuvishwa joho jipya kuwa lugha ya kazi katika Umoja wa Afrika"
"Kiswahili kilipitishwa kuwa Lugha ya Kazi ya Umoja wa Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika tarehe 5 - 6 Februari, 2022 Jijini Addis Ababa, Ethiopia, hatua hii ni fursa muhimu kwa Wataalamu wetu wa Tafsiri na Ukalimani nchini ambao katika muda mfupi tu tayari Watanzania 65 wamesajiliwa kupata fursa za ajira za muda na za kudumu katika Umoja wa Afrika na Kamisheni zake"
"Pia, kutokana na nafasi ya Kiswahili, kuendelea kushamiri, baadhi ya Vyuo Vikuu vya nje ya Tanzania ambavyo awali havikuwa na programu za Kiswahili vimeanza harakati za kuingiza Kiswahili katika programu zao ambapo tayari kuna makubaliano ya awali ya kushirikiana kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Ethiopia, Chuo Kikuu cha Port Harcourt (Nigeria) na Chuo Kikuu cha Joachim Chisano (Msumbiji) katika kufundisha Kiswahili"

Enjoy...