Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220501-093953_Opera%20Mini.jpg
 
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amefika mjini Kyiv nchini Ukraine leo na kukutana na Rais wa Ukraine.

Pelosi akiwa Ukraine amesema "Marekani ndio inayoongoza kwa kuunga mkono vita vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi".

Pelosi aliongozana na Mwanademokrasia mwenzake Adam Schiff na Wabunge wengine watatu
Screenshot_20220502-041228_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia leo kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi amezungumzia walioondole kazini kisa vyeti feki ambapo amesema "Serikai iliwarudisha Watumishi wa Darasa la saba walioondolewa kwa makosa au ambao walienda kujiendeleza walirudishwa makazini kwa mamia, nimepoka malalamiko ya TUCTA kuhusu darasa la saba waliiondoshwa na mkumbo wa vyeti feki"

"Tumewaza wale wote waliofanyaka kazi kisha wakafukuzwa kisa vyeti feki na hawakupata chochote cha kuondoka nacho, nimewaagiza Wizara ya Fedha waangalie ni kiasi gani walikatwa kwenye jasho la mishahara yao, kisha walipwe jasho walilitoa kile walichochangia kwenye mfuko walipwe jasho walilolitoa"

"Watumishi waliofanya kazi kwa muda mrefu na wakabakiza miaka kiwili au mitatu kustaafu na wenyewe waangaliwe ni kiasi gani itagharimu tukiwapa mafao yao"
Screenshot_20220502-041444_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia leo kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi ametoa msisitizo kwa Wafanyabiashara kuacha kupandisha bei za bidhaa kiholela nchini na kusababisha ugumu wa maisha.

"Wafanyabiashara wanapandisha bei za bidhaa kiholela na kuongeza ugumu wa maisha, Waziri Mkuu alishatoa kauli kuhusu hili nami nasisitiza tuache visingizio twende kwenye uhalisia"
Screenshot_20220502-041807_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia akiwa kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi Dodoma leo ametoa msisitizo kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanawapanga Wamachinga bila matumizi ya mabavu wala kuwasumbua.

"Wamachinga nilitoa agizo kuwa wawekewe utaratibu na sio kuwasumbua nimeshaletewa malalamiko kutoka kwenye baadhi ya maeneno ya nitayafanyia kazi, Viongozi fanyeni zoezi hili bila kutumia mabavu na ningependa lifanyike mchana sio kuwavizia usiku"
Screenshot_20220502-041900_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom