Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi leo ametangaza kuongeza kima cha chini cha mshahara wa Wafanyakazi kwa asilimia 12.

Rais Kenyatta amesema uamuzi wa kuongeza kima cha chini cha mshahara una lengo la kuongeza nguvu kazi ya nchi dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha kunakosababishwa na sababu kadhaa za kiuchumi za nje.

Kima cha chini cha mshahara Kenya kwa sasa ni Ksh. 13,500 ( Tsh. 271,089) ambacho kilifanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 2018.
Screenshot_20220502-042003_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi Dodoma leo amewaonya Vijana wanaojiita panya road ambao wanajeruhi na kupora kuacha tabia hiyo mara moja kwasababu wanahatarisha maisha ya Raia na maisha yao pia.

"Kumeanza kujitokeza uhalifu kuna vijana wanajiita panya road au panya buku wanavamia, kujeruhi na kupora, nawaonya waache mara moja unyama huo kwasababu wanapohatarisha maisha ya Raia wanajitaharishia usalama wao pia"
Screenshot_20220502-042117_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia leo kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi ambayo yamefanyika Kitaifa Dodoma amewahakikishia Wafanyakazi kuwa jambo la nyongeza ya mishahara mwaka huu lipo kama alivyowaahidi mwaka jana na kusema mahesabu yanaendelea ili kujua itapandishwa kwa kiasi gani.

"Ulezi wa Mama unaendelea, lile jambo letu (kupandisha mishahara) lipo, sio kwa kiwango kilichosemwa na TUCTA kwasababu hali ya uchumi wa Nchi yetu na uchumi wa Dunia sio nzuri sana, uchumi wetu ulishuka mnoo tumejitahidi sana kuupandisha na kwasababu tulishatoa ahadi mwaka jana nimeagiza jambo liwepo, mahesabu yanaendelea tutajua lipo kwa kiasi gani lakini jambo lipo"
Screenshot_20220502-042220_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia akizungumza kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi yanayofanyika Kitaifa Dodoma leo amesema Serikali imeunda Bodi za kushughulikia kima cha chini cha mshahara ambazo zitafanya tathmini ya kima cha chini kwenye Sekta za umma na binafsi ili kuboresha maslahi ya Wafanyakazi ambapo ameziagiza pia Wizara zinazohusika kuziwezesha Bodi hizo kufanya kazi vizuri.

"Kuhusu viwango vya mishahara nakubaliana nanyi kwamba viwango havikidhi mahitaji ya Mfanyakazi na Familia yake, natambua jukumu la Bodi za kima cha chini cha mishahara, la kuishauri Serikali kuhusu kima cha chini cha mishahara"

"Serikali imeunda Bodi za kima cha chini cha mishahara ili kufanya tathimini ya kima cha chini cha mshahara kwenye Sekta binafsi na za Umma, naziagiza Wizara zinazohusika kuziwesha Bodi hizi kufanya kazi"
Screenshot_20220502-042500_OGInsta%2B.jpg
 
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), leo kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi yanayofanyika Kitaifa Dodoma, kwa niaba ya Wafanyakazi wote limemuomba Rais Samia atimize ahadi yake aliyoitoa mwaka jana ya kuwapandishia Wafanyakazi mishahara.

"Rais Samia mwaka jana ulisema 'Mimi ni Mama na Mama ni Mlezi' hivyo Mama tuna imani na matarajio makubwa juu ya ahadi uliyotoa katika siku ya Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka jana kuhusu kutupandishia mishahara Wafanyakazi wa Tanzania"

"Bila shaka hotuba yako hii ya leo Rais Samia itakata kiu yetu, Mama endelea kuupiga mwingi, Mama yetu mpenzi sema kitu leo ili roho zetu zitulie" Katibu Mkuu TUCTA, Henry Mkunda
Screenshot_20220502-042601_OGInsta%2B.jpg
 
Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuiba tani laki kadhaa za nafaka kutoka katika eneo linalokaliwa na vikosi vyake.

Naibu Waziri wa Kilimo wa Ukraine, Taras Vysotskyi, amesema anahofia kwamba Urusi inaweza kuiba tani nyingi za tani milioni 1.5 za nafaka katika maeneo ambayo sasa inayadhabiti.

Urusi haijazungumzia madai hayo, mashambulizi ya makombora ya Urusi na hatua yake ya kuziba bandari ya Bahari Nyeusi ya upande wa Ukraine yametatiza uzalishaji wa nafaka na kuzua wasiwasi wa kimataifa juu ya kupanda kwa bei ya vyakula.

Ukraine ni mojawapo ya wauzaji wa juu wa mafuta ya nafaka na mboga duniani na imepewa jina la utani ghala la mkate.
Screenshot_20220502-042803_OGInsta%2B.jpg
 
Kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) limedai kuhusika na mashambulizi kwenye Msikiti mmoja kwenye Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul, siku moja baada ya Waumini 10 kuuawa kwenye mashambulizi hayo.

Kupitia ujumbe wake kundi hilo limesema lilitega bomu kwenye basi karibu na eneo liitwalo Sekta 6 mjini Kabul, kundi hilo limetoa idadi hiyo hiyo ya Watu kumi waliouawa, sawasawa na idadi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan.

Polisi mjini Kabul wanasema Watu wengine 30 walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya siku ya Ijumaa, Maafisa wa Afghanistan wanasema mashambulizi hayo yaliwalenga waumini wa madhehebu ya wachache ya Sufi, ambao walikuwa wakiendelea na tasbihi zao baada ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alitowa taarifa ya kulaani mashambulizi hayo jana Jumamosi.
Screenshot_20220502-042854_OGInsta%2B.jpg
 
Sweden imesema ndege ya jeshi la Urusi imeingia kwenye anga lake kinyume na sheria, tukio hilo linaripotiwa kutokea kwenye Bahari ya Baltiki karibu na kisiwa cha Bornholm.

Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Sweden ilisema kuwa ndege ya Urusi chapa AN-30 iliruka kwenye anga la Sweden na kuingia kwenye eneo lake kwa muda mfupi kabla ya kuondoka.

Jeshi la Anga la Sweden lilituma ndege yake iliyoipiga picha ndege hiyo ya Urusi, Waziri wa Ulinzi wa Sweden, Peter Hultqvist, amesema kupitia redio ya umma kwamba hatua hiyo ya Urusi haikubaliki na si ya kitaalamu, tukio kama hilo lilitokea mwanzoni mwa mwezi Machi, ambapo ndege nne za Urusi ziliingia kwenye anga la Sweden.

Sweden na jirani yake, Finland, zinafikiria kujiunga na jumuiya ya kijeshi ya NATO kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine lakini Urusi imeonya kuwa hatua kama hiyo itakuwa na matokeo mabaya bila kufafanua zaidi.
Screenshot_20220502-044620_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati wataalamu wakiendelea na utafiti wa dawa ya kutibu ukimwi, imegundilika mbinu mpya ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa wanawake kwa kutumia pete maalumu iitwayo ‘Dapivirine Vaginal Ring’.

Pete hiyo ambayo inapewa nafasi kubwa ya kushusha maambukizi kwa kundi hilo, ina madini ya silikoni inayovaliwa ukeni na hudumu kwa siku 28 na hutoa dawa kinga ya ‘dapivirine’ inayoua virusi vya ukimwi ukeni.

Imeelezwa kuwa ni rahisi kuivaa, inakinga virusi kwa asilimia kubwa na hata mwenza hawezi kubaini iwapo mwanamke ameivaa.

Ujio wa pete hiyo umetokana na utafiti wa muda mrefu uliolenga kutafuta njia ya kuwalinda wanawake dhidi ya maambukizi ya VVU wakati wa kujamiiana bila kutegemea wanaume kuvaa mipira (kondomu).

Kinga hiyo imekuja baada ya utafiti wa miaka zaidi ya 10 kufanyika nchini Marekani na Afrika na mwaka 2020 Shirika la Afya Duniani (WHO) liliruhusu pete hizo kutumika kama njia ya kinga na mpaka sasa nchi nne zimeanza kutumia ikiwemo Afrika Kusini, Uganda, Zimbabwe na Malawi.

Kwa upande wake, Serikali imekiri kuifuatilia pete hiyo na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale alipoulizwa alisema Wizara ya Afya ina taarifa na uwepo wa kinga hiyo mpya.

“Taarifa pia zimepokelewa kupitia asasi zisizo za kiserikali (CSOs) pamoja na umoja wa wanawake wanaoishi na maambukizi ya VVU wakihimiza upatikanaji na matumizi ya dawa yaanze.

“Wataalamu wizarani kupitia NACP (Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi) watashirikiana na Taasisi ya utafiti na TMDA (Mamkala ya Dawa na Vifaa Tiba) kuendelea na mjadala kuangalia ubora na usalama wa dawa hiyo kabla ya kuanza kutumika nchini na kama ina faida zaidi ukilinganisha na kinga za aina nyingine zinazotumika,” alisema Dk Sichwale

ABJ njoo usome tumefafanuliwa
Screenshot_20220502-044944_OGInsta%2B.jpg
 
KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekuwa kocha wa Kwanza duniani kuwahi kushinda mataji yote matano ya Ligi 5 kuu za Ulaya yani;
Serie A - AC Milan (2003/04)
󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 EPL - Chelsea (2009/10)
Ligue1 - PSG (2012/13)
Bundesliga - Bayern (2016/17)
LaLiga - Real Madrid (2021/22).
Screenshot_20220502-050107_OGInsta%2B.jpg
 
Wanasimba wanamuita Varane, beki wa mpira, Henoc Inonga Baka jana ameonyesha ustadi mkubwa sana kwa kuuweka salama ukuta wake katika mechi ya Kariakoo Derby baina ya Simba dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Mkapa mchezo uliomalizika kwa suluhu ya 0-0.
Screenshot_20220502-050402_OGInsta%2B.jpg
 
Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele aliahidi kuwa na deni na timu mbili Ligi Kuu ya NBC ambapo ni Namungo na Simba.
Deni la Namungo alifanikiwa kutimiza ila kwa upande wa Simba limekuwa gumu maana katika mchezo wa jana dhidi ya Simba hakufanikiwa.
Screenshot_20220502-050507_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Niliwahi kusoma kitabu cha mbabe Adolph Hitler kinaitwa Mien Kampf yani My Struggle kwa lugha ya Malkia Elizabeth, ndani yake kuna kurasa za ubabe, mambo ya kutisha ila lengo ni Ujerumani imara mbele ya dunia

Nisikilize tena, niliwahi kusoma simulizi nzito za Benito wa Musollini kutoka ardhi ya Warumi, ndoto yake ilikuwa mkono wake kutawala kuanzia milima saba ya Roma mpaka Vingunguti, Dar Es Salaam, hata Miungu ya Olympus pale Ugiriki iliogopa

Ni simulizi kubwa za wababe tena za kutisha sana! Haikutosha nikamsoma tena Fidel Castro kwenye kitabu cha The Spy who loved Fidel Castro, ndani yake kuna Maria Ortega, ni simulizi ya kutisha

Inatisha mno, Mwanamama alipewa kazi ya kumuuwa Castro, lakini hakufanikiwa! Ni moja kati ya simulizi za kutisha sana, ambazo mpaka kesho Walimu wa Historia husimulia kwa kutisha, dunia ilikuwa ya wababe

Naweka vitabu chini vya watu watatu wa kutisha, nashika kalamu yangu namkumbuka Nemanja Vidic kutoka Belgrade Serbia, beki wa kutisha aliekuwa akishuhudia mkono wa damu ukiitesa Serbia, anaenda mazoezini anapisha na mizoga ya binadamu

The tough the character, the tough the man! Alisema Mwalimu wangu Ezekiah Mwashilindi wa Language two pale Lubala, Tukuyu! HGL CLASS OF 2017! Ndicho hicho kimenikumbusha kuhusu nyakati

Nyakati zimekwenda wapi?? Lini tutapata Binadamu kama wale!?? Binadamu wa mwisho mwisho ndip kama HENOCK INONGA BAKA, anaingia kwenye mechi anasema tu HUPITI, anasema tu HUCHEZI, anasema tu MIMI NDIO MWANAUME

Undava kama huu, ubabe kama huu ndio ulileta vita za dunia, ulileta vita baridi! Ni basi Wanaume wachache wa damu hizi wamesalia, man like Inonga are very rare

Zipo wapi nyakati?? Alaa tupo kwenye kizazi cha Snapchat, Tiktok na comments Instagram, samahani Braza nisaidie kushea! Anha zipo wapi nyakati??

Screenshot_20220502-050800_OGInsta%2B.jpg
 
Salehe Mawele

Kuna nyakati ni ngumu sana kuuelewa mpira wa kisasa, unatuvuruga vichwa na unatuchanganya sana akili, mpira unaotazama zaidi roles ( majukumu ) na nafasi ( position ), Meddie, Meddie, Meddie Kagere anaangushwa na soka la kisasa hasa linapokuja swala la kucheza kama single striker, ni ngumu kuelewa.

Meddie, kama anacheza katika ubora wake anawaacha mbali washambuliaji wengi wa Tanzania, bahati nzuri huwezi kumtilia shaka katika consistency ( muendelezo ), ndani ya misimu mitatu ana goli zaidi ya 50 na akichukua golden boot mara mbili mfululizo.

Ukitembelea katika vijiwe vya kahawa au kwenye vibanda umiza kilio kikubwa cha mashabiki wa Simba ni safu yao ya ushambuliaji, ni kweli, ukiwatazama washambuliaji wao wote watatu hakuna hata mmoja aliefikisha goli kumi, mbaya zaidi wawili kati yao bado hawana goli hata moja.

Kitu cha kwanza kilichowaangusha msimu huu ni ingia toka ndani ya kikosi, majeraha ya mara kwa mara yamekuwa yakiwatoa mchezoni, angalau Meddie amekuwa fiti mara nyingi lakini bado hajakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza mbele ya Pablo Franco.

Hoja yangu ipo hapa sasa, kwenye roles, timu nyingi Duniani kama sio zote ambazo zinacheza katika system ya 4-2-3-1 zinakuwa na mshambuliaji ambae hasimami kama wafungaji pekee, anakuwa kama playmaker wa ziada, ndio soka la kisasa na itabidi tuishi nalo tu.

Mugalu vs Meddie, Mugalu ana vitu vingi ingawa hawezi kukwepa lawama za kutokuweka mpira wavuni kwa dakika hizohizo chache alizozipata, ni kweli anaisaidia timu kwenye link up (kutengeneza muunganiko kwenye eneo la mwisho), kushuka between the line (baina ya mabeki na viungo).

Mugalu akicheza kama central striker utategemea kuwaona pia mawinga wakicheza kwenye zile flanks mbili, kwanini? kwa sababu ya ile mikimbio yake ambayo inavunja patterns za ulinzi katika mstari wa mabeki wa timu pinzani kitu ambacho Kagere hawezi.

Meddie ni mfungaji mzuri lakini si mchezaji mzuri katika hiyo system ya mshambuliaji mmoja mbele, kwenye soka la kisasa anafaa zaidi katika system ambayo timu itatumia twin strikers ( 4-4-2, 3-5-2, 4-2-2-2, 3-4-1-2, 4-1-3-2 ), ni ngumu kulielewa hili lakini itabidi tulielewe.

Asante.
Screenshot_20220502-053224_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom