Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,166
GEITA Gold itawakosa nyota wake wanne akiwamo beki Kelvin Yondani wakati itakapoikabili Azam katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa leo mjini hapa.
Nyota hao watakosekana kwa sababu mbalimbali, huku wenyeji wakiwa na kiu ya kuendeleza wimbi la ushindi kwani mchezo uliopita ilishinda 2-0 dhidi ya KMC.
Katibu wa Geita, Simon Shija alisema maandalizi yanaendelea, ila itaikosa huduma ya Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Mussa Gadi (mgonjwa), Aaron Katambo na Yusuph Kagoma wenye matatizo ya kifamilia.