Rais Samia wakati wa uzinduzi wa filamu ya Royal Tour Arusha leo amesema wakati wa uandaaji wa filamu hiyo wapo Watu mitandaoni walisema amejigeuza Rambo au Arnold Schwarzenegger badala ya kufanya kazi lakini amesema faida ya filamu hiyo ni kubwa.
"Wakati nafanya hili jambo kuna Wadogo zangu, Wanangu kwenye mitandao wakawa wanasema 'Huyu Mama badala ya kufanya kazi amejigeuza Rambo au Schwarzenegger anafanya mafilamu huko anaigiza' lakini nikasema ngoja tuone kitakachotoka"
"Tumeanza kuizindua Marekani, tulipoanza New York ile siku salamu za Watu laki tatu na zaidi wakawa wanapongeza , Los Angeles nako tukapata mrejesho mzuri sana, kufanya jambo kama hili kunahitaji kujitoa, nimetumia siku nane nje ya Ofisi na siku nane kukaa nje ya Ofisi ya Rais ni muda mrefu sana"
"Niwahikikishie hasara ambayo nimeisababisha kwa kutokaa kwenye Ofisi kwa siku nane na kutohudumia Wananchi kwa kipindi kile italipa mara elfu mbili mara hadi mara elfu tatu kutokana na filamu hii, tumefanya vikao na Watu mbalimbali marekani baada ya kuuona filamu wanasema wanataka kuja Tanzania"




auntie maki njooo umsome mama yako kumbe anafatilia mitandao nimecheka sana
View attachment 2203957