Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa Madini, Dotto Biteko leo Bungeni Dodoma amesema changamoto ya vita kati ya Urusi na Ukraine inaweza kusababisha mahitaji makubwa ya madini ya dhahabu.

"Uchumi wa madini nchini kwa kiasi kikubwa unatokana na madini ya dhahabu, ambayo huchangia takribani asilimia 80 ya mapato yatokanayo na rasilimali madini, Wachambuzi wa masuala ya uchumi duniani walitarajia bei ya dhahabu kuendelea kuwa tulivu kwa mwaka 2022, hata hivyo, bei ya madini ya dhahabu imepanda kutoka wastani wa dola za Marekani 1,412.98 Julai 2019 hadi kufikia 1,947.83 Machi, 2022

"Kuongezeka kwa bei ya dhahabu kunatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo wa UVIKO-19, vita kati ya Urusi na Ukraine inaweza kusababisha mahitaji makubwa ya madini ya dhahabu, hii ni kwa sababu watu na taasisi duniani hupendelea kuhifadhi thamani ya fedha zao katika madini ya dhahabu kwa kuwa ni amana iliyo salama zaidi hasa wakati wa mitikisiko ya kiuchumi"

"Kwa upande mwingine, ukuaji wa teknolojia umesababisha ongezeko la mahitaji ya madini ya palladium, nickel, aluminium, cobalt na madini ya kinywe (graphite), hivyo, bei ya madini hayo inatarajiwa kupanda na kuongeza fursa za uwekezaji" Waziri Biteko
Screenshot_20220429-181116_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha Cedric Kaze wa Yanga amesema presha ni kubwa kuhusu mechi yao ya kesho wakicheza na Simba “Kesho tunaenda kucheza mechi kubwa na inahusisha Klabu kubwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, tumejiandaa vizuri na tunaamini tutakuwa na mchezo mzuri"

“Ukweli presha ya mchezo wa kesho ni kubwa lakini presha hiyo ipo kwenye mechi zote tunazoenda kucheza kikubwa ni maandalizi lazima yawe mazuri kwenye kila mchezo tunakwenda kucheza”

“Mechi ya Derby ni mchezo special kwa Watu wote, Mashabiki, Wachezaji na kila mmoja wetu cha kufanya ni hakikisha tunajiandaa kukabili hisia zetu tunapokwenda kucheza mchezo huu"

"Tunakwenda kucheza mchezo wenye nidhamu kwasababu tunajua tunaenda kukutana na mpinzani mzuri na mwenye uzoefu na kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mechi ya kesho kwetu sote na naamini kesho tuna nafasi" Kocha msaidizi Cedric Kaze, Yanga.
Screenshot_20220429-181316_OGInsta%2B.jpg
 
Vyombo vya Habari nchini Ethiopia vimeripoti kwamba Misikiti na Makanisa yamechomwa moto na makundi ya Watu katika maeneo mbalimbali kaskazini na kusini mwa Ethiopia siku ya Alhamisi chanzo kikitajwa kuwa ni sehemu ya kulipiza kisasi.

Vurugu hizo zinadaiwa kusababishwa na hasira za zilizotokana na kitendo cha Waislamu 20 kuuawa na Mamia ya wengine kujeruhiwa walipokuwa wakihudhuria mazishi ya kiongozi wa kidini wa eneo hilo siku ya Jumanne katika mji wa Gondar mkoani Amhara.

Makanisa matatu pia yamechomwa moto katika kile kinachoonekana kuwa ni mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa ghasia za awali.

Serikali ya Ethiopia imesema Watu 280 wamekamatwa kuhusiana na ghasia hizo huko Gondar.
Screenshot_20220429-181446_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220429-181503_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220429-181520_OGInsta%2B.jpg
 
Deus Kaseke amezungumza leo kueleka mchezo wa kesho wa Yanga dhidi ya Simba SC ambapo wao wana mtihani wa kutetea rekodi yao ya kutofungwa mchezo hata mmoja wa Ligi Kuu msimu huu.

“Kwa ujumla maandalizi yako salama na kila Mchezaji ana hamu ya kushinda mchezo wa kesho japo tuna waheshimu Wapinzani wetu ni timu nzuri sababu ni timu ambayo ina nafasi (Ubingwa) kama sisi tulivyokuwa na nafasi” Kaseke
Screenshot_20220429-181705_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amesema kuruhusu wageni kutoka nje ya nchi kwenda moja kwa moja Mererani kununua madini ya Tanzanite kunaondoa fursa kwa watu mbalimbali walioko nchini katika soko la madini hayo.

Pia, ametaka kuwe na masoko mengi ya Tanzanite ndani ya nchi ili kuongeza ushindani wa soko la madini hayo.

Gambo amesema hayo leo Ijumaa Aprili 29, 2022 wakati akichangia makadilio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara wa Madini mwaka 2022/23 bungeni jijini.
Screenshot_20220429-181847_OGInsta%2B.jpg
 
Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson ameahirisha mkutano wa Bunge hadi Alhamisi ya Mei 5, 2022 saa tatu asubuhi.

Sababu ya kuahirishwa kwa siku zote imetajwa ni kutokana na kutokuwa na uhakika wa mwanadamo wa mwezi ambao utafanya uwepo wa sikukuu ya waumini wa dini ya Kiislamu inayoendana na mwandamo wa mwezi.

Spika amesema kulingana na tangazo la Mufti wa Tanzania kuwa huenda sikukuu ikawa kati ya jumatatu au siku ya jumaa, anaona busara kuahirisha Bunge hadi Alhamisi kwa kuwa hakutakuwa na siku ya kukutana tena.
Screenshot_20220429-181949_OGInsta%2B.jpg
 
Mazishi ya kitaifa ya Rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki yanafanyika leo Ijumaa Aprili 29, 2022 katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, yakiongozwa na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.
Kibaki alifariki akiwa na umri wa miaka 90.
Screenshot_20220429-182049_OGInsta%2B.jpg
 
Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto kutoka Makao Makuu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Faidha Suleiman amefanya Ukaguzi wa Madawati ya Jinsia na watoto katika mkoa wa Mtwara ili kubaini changamoto na kuzitafutia ufumbuzi ambapo pia amezungumza na Watendaji wa Dawati, Maafisa Ustawi Jamii katika Manispaa ya Mtwara na Wakaguzi wa Kata.
Screenshot_20220429-182201_OGInsta%2B.jpg
 
Benki ya NMB imekusanya Sh74.27 bilioni katika mauzo yake ya hatifungani ya Jasiri (NMB Jasiri Bond), ikiwa ni zaidi ya lengo ililojiwekea la kukusanya Sh25 bilioni.

Makusanyo hayo yanayoweka rekodi ya ukubwa Afrika Mashariki, yamebainishwa jana Aprili 28 baada ya benki hiyo kufunga hati fungani na kuiorodhesha hati hiyo rasmi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Akizungumza katika hafla ya ufungaji wa hati fungani hiyo, Naibu Katibu Mkuu- Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, amesema fedha hiyo iliyokusanywa itasaidia kutoa mikopo kwa wanawake wanaojishughlisha na biashara.

“Hii sio mara ya kwanza kwa NMB kuja na Hati Fungani na kuvuka lengo la makusanyo, hii ni mara ya nne na kwa hati hii ambayo ni ya kipekee, kama jina lake lilivyo, kumekuwa na ujasiri mkubwa sana, kwani jina Jasiri linaashiria mambo mengi sana," amesema.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema NMB ilipokea maombi 1,630 yaliyowezesha kukusanya kiasi hicho cha fedha badala ya kilichotarajiwa

“Kuaminika kwa NMB katika hili kunathibitishwa na kuwa asilimia 96 ya waliotuma maombi ya kununua Hati Fungani, yamepitia katika matawi yetu, huku asilimia 4 tu yakifanyika kupitia Madalali wa Soko la Hisa waliosajiliwa," amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), Nicodemus Mkama, amesema kuorodheshwa kwa hati fungani hiyo katika DSE kunafungua fursa kwa walioshindwa kununua awali, kufanya hivyo kupitia soko hilo.
Screenshot_20220429-182316_OGInsta%2B.jpg
 
“Kazi ya kuimarisha udhibiti wa biashara haramu ya utoroshaji wa madini hufanywa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania, Mamlaka ya Mapato nchini, Ofisi ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Idara ya uıhamiaji, Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa na wilaya pamoja na raia wema wanaotoa tarifa.

Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 madini ya aina mbalimbali yakiwemo dhahabu, vito, mchanga na madini ya viwandani yenye thamani ya Sh500.1 milioni yalikamatwa katika matukio ya utoroshaji biashara haramu ya madini katika mikoa ya Mbeya, Morogoro, Manyara, Dodoma, Lindi, Geita, Dar es Salaam na mwanza,” - Waziri wa Madini, Dotto Biteko
Screenshot_20220429-182422_OGInsta%2B.jpg
 
Trevor Jacob, rubani wa ndege ndogo nchini Marekani amefutiwa leseni kutokana na uzembe alioufanya ndege yake ilipopata ajali halafu yeye akaitumia kujirekodi video aliyoituma kwenye Youtube ili apate watazamaji wengi.

Jacob alipata ajali hiyo Novemba mwaka jana na Desemba akatuma video kwenye akaunti yake ya Youtube ikimwonyesha alivyonusurika katika ajali hiyo.

Hata hivyo, baada ya uchunguzi, Mamlaka ya Anga nchini Marekani (FAA) imesema hakuzingatia kanuni za dharura, ikiwamo kukitaarifu kituo cha uongozi ndege wala kujaribu kuiwasha tena ndege au kutua sehemu salama zaidi.

“Haukuwa makini, haukuwajibika wala kujishughulisha ulipoamua kuruka kutoka kwenye ndege uliyokuwa unaiendesha ukilenga kujirekodi video ya ajali hiyo,” inasomeka sehemu ya barua aliyoandikiwa Jacob akijulishwa sababu za kufutiwa leseni ambayo imeonwa na gazeti la New York Times
Screenshot_20220429-182533_OGInsta%2B.jpg
 
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango leo Ijumaa Aprili 29 ,2022 akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akiondoka kwenda Nairobi nchini Kenya kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa tatu wa Kenya, Hayati Mwai Kibaki.
Screenshot_20220429-182649_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Simba, Pablo Franco kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Yanga hapo kesho kwenye uwanja wa Mkapa amesema timu yake ina wachezaji bora kuliko wapinzani wake.

“Wenzetu wana timu yenye ushindani lakini sisi tuna wachezaji bora zaidi kuliko wao na tunacheza mpira mzuri zaidi. Mashabiki wetu wana imani kubwa na sisi, sijawahi kuona popote timu inapoteza lakini tunarudi na kupokewa vizuri na mashabiki” amesema Pablo.
Screenshot_20220429-184949_OGInsta%2B.jpg
 
“Hatuwezi kuwapa faida wapinzani wetu” maneno ya kocha wa Simba, Pablo Franco baada kuulizwa wachezaji watakaokosekana kwenye mechi ya Kariakoo Derby dhidi ya Yanga hapo kesho.

Pablo aligoma kutaja wachezaji hao na kusema wasubiri mpaka kesho ndio itajulikana na hakuishia hapo alisema anajua ugumu wa mechi yenyewe kwaiyo hawezi kuwapa wapinzani faida.

Yanga na Simba zitachezo kesho Aprili 30 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 11 jioni.
Screenshot_20220429-185207_OGInsta%2B.jpg
 
"Kesho tunaenda kucheza mechi kubwa na inahusisha klabu kubwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, tumejiandaa vizuri na tunaamini tutakuwa na mchezo mzuri" amesema kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze.
Screenshot_20220429-185520_OGInsta%2B.jpg
 
MSHAMBULIAJI wa Azam, Prince Dube anajivunia rekodi yake ya kuifunga Yanga ambayo imedumu kwa mwaka mmoja sasa bila ya kuvunjwa.

Rekodi hiyo ni ile ya Aprili 25, 2021, wakati alipoifungia timu yake ya Azam bao 1-0 dhidi ya Yanga ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha Nasreddine Nabi alipoanza kukinoa kikosi hicho na tangu hapo haijawahi kuvunjwa zaidi ya kutoa vipigo na sare.

“Ni jambo nzuri kwangu kuona rekodi ambayo niliiweka mwenyewe haijavunjwa lakini binafsi nilitamani sana kuivunja wakati tulipokutana kwenye michezo yote miwili kwa msimu huu ila bahati mbaya kwangu ilishindikana,” alisema Dube na kuongeza;

“Ni mapema kusema rekodi hiyo haitavunjwa kwa sababu michezo iliyosalia bado ni mingi na lolote linaweza kutokea hivyo tuendelee kusubri na kuona kitakachojiri ingawa kwa sasa akili zangu ni kuisaidia timu yangu kufanya vizuri na wala sio vinginevyo.”

Bao hilo la ushindi kwa Dube lilikuwa la mwisho kwa Yanga kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo imetimia mwaka mmoja sasa bila kuonja ladha ya kichapo, ambapo tangu Aprili 25, 2021, timu hiyo imecheza michezo 27, ikishinda 21 na kutoka sare sita.

Screenshot_20220429-185649_OGInsta%2B.jpg
 
Kiungo wa zamani wa Yanga, Papy Tshishimbi alisema anaipa nafasi kubwa Yanga kuondoka na ushindi licha ya kukiri mchezo huo ni mgumu kutokana na uhasama uliopo baina ya wapinzani hao pindi wanapokutana na kwa kuangalia rekodi zao za hivi karibuni.

“Dabi siku zote huwa ni ngumu na haitabiriki ingawa nikiangalia kikosi cha Yanga msimu huu na jinsi ambavyo wanacheza nawaona kabisa wakiibuka na ushindi licha ya ukweli yeyote atakayejiandaa vyema kisaikolojia ataibuka mshindi,” alisema Tshishimbi.
Screenshot_20220429-185819_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom