Mahakama nchini Morocco imemhukumu Mwanaharakati kifungo cha miaka minne jela baada ya kumchukiza Mfalme Mohammed wa sita kwenye mtandao wa kijamii.
Rabie Al Ablaq amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kumkosoa Mfalme mtandaoni, kesi hiyo ilifunguliwa Aprili 11 baada ya kupost mtandaoni video zinazokosoa tofauti za kijamii na ufisadi nchini humo.
Mwanaharakati na Mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 35 pia alipigwa faini ya dirham 20,000 ($2,000).
Human Rights Watch imesema Al Ablaq alitiwa hatiani kutokana na video mbili zilizopostiwa Facebook na YouTube mnamo Septemba na Novemba 2021 ambapo alimzungumzia Mfalme na kulinganisha hali yake binafsi na umaskini ulioenea nchini Morocco.
View attachment 2203687