Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika safari yake nchini Marekani, ikiwepo kusaini mikataba na wawekezaji yenye thamani ya Sh11.7 trilioni.

Akizungumza leo Alhamisi April 28, 2022 baada ya kuwasili nchini na ndege ya Qatar airways katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Rais Samia amewataka Watanzania kujiandaa kuwapokea wawekezaji hao wakija nchini.

Rais Samia ambaye leo anazindua filamu ya Royal Tour jijini Arusha, amesema wawekezaji hao kama wakija nchini, wanatarajiwa kutoa ajira kwa watu 301,000.
Screenshot_20220428-152507_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limemkamata Iddi Omari Ndakae maarufu Chuma Steel kwa tuhuma za kupora pikipiki katika maeneo ya Kigamboni na maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam "Mtuhumiwa akiwa na wenzake April 16,2022 alimkodisha dereva pikipiki Jumanne Mpenja kutoka Mbagala charambe kumpeleka Kigamboni, walipofika Visikini, Kigamboni alimpiga dereva kwa kitu kizito kichwani hadi kufariki na kuiba pikipiki yake"

"Katika mahojiano ya kina na Mtuhumiwa huyo Jeshi la Polisi lilibaini kuwa Mtuhumiwa alishiriki katika tukio lingine la kumpiga kwa kitu kizito kichwani kisha kumuua Mkapa Nuru miaka (20-25) tarehe 27.08.2021 aliyekuwa mkazi wa Mbagala Kiburugwa na kumpora pikipiki"

"Baada ya kufanya tukio hilo la mauaji Mtuhumiwa aliutupa mwili eneo la Visikini Dege Kigamboni ambapo katika ukaguzi wa eneo hilo kumepatikana mifupa idhaniwayo ya binadamu ambayo ni fuvu la kichwa, mifupa ya nyonga na kaptula ya jeans vyote vinavyodhaniwa kuwa ni vya marehemu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu"

"Pia amekamatwa Mfaume Donald Kapela (23) mkazi wa Kibiti sokoni ambaye alishirikiana nae na baada ya mahojiano ya kina Jeshi lilifanikiwa kuipata pikipiki ya marehemu" Muliro Jumanne, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
Screenshot_20220428-152637_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati page nyingi kubwa za habari Ulaya na vyombo vya habari vya kimataifa vikitangaza kuwa Mino Raiola amefariki

Taarifa kutoka hospitali aliyopo nchini Italia zinasema, Mino bado hajafa na anapigania uhai wake hospitali

Source: Fabrizio Romano
Screenshot_20220428-155143_OGInsta%2B.jpg
 
...huyo aliyekwambia kuwa mimi ni mzee ndiye adui yangu, sina hakika kama ni Nigendako au mkwepu jr , yaani siku wameniona tu nimevaa foo engo tayari wakasema mimi ni mzee!!!!. Hiiiiiiiii, mimi ni kijana kabisa, mafao nnayokula ni vile tu nilistaafishwa ajira mapema
binamu hautaki kukubaliana na hali, jua limeshazama binamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom