Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muonekano wa ndani na nje ya ukumbi wa Simba Hall, AICC, jijini Arusha ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atafanya uzinduzi wa 'The Royal Tour' leo Aprili 28, 2022 kuanzia saa 8:00 mchana.

Uzinduzi huu utahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wadau wa Sekta ya Utalii nchini.
Screenshot_20220428-132512_OGInsta%2B.jpg
 
Watu wanne wakiwemo Polisi wawili na Watuhumiwa wawili wamefariki dunia na Watu wengine wanne wamejeruhiwa baada ya kupata ajali eneo la kijiji cha Ibanda Barabara ya Geita kuelekea Sengerema iliyohusisha gari la Polisi na lori.

RPC wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni kukatika kwa usukani wa gari la Polisi na kupelekea kukosa uelekeo na kuligonga lori lililokuwa mbele yao.

"Waliofariki ni G.4467 D/CPL Mussa Askari Polisi wa Mkoa wa Mwanza , G.5702 D/C Faraji Askari Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na Twaha Saidi na Tesha Luiza ambao walikuwa Watuhumiwa"

"Chanzo cha ajali ni gari namba PT.3798 Toyota Land Cruiser ilikatika usukani na kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kusababisha kugongana na gari namba T.691 DBQ Scania, Majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Geita na miili ya Marehemu imepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza"
Screenshot_20220428-132700_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia akiwa Uwanja wa Ndege wa KIA akitokea Marekani leo amesema akiwa nchini Marekani amefanya mazungumzo na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani na wameahidi kuipa Tanzania fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

"Tumefanya mazungumzo na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) nao pia mambo mazuri tumekubaliana vizuri na kuna fedha kama ile tuliyoleta tukaipeleka kujenga vituo vya afya, madarasa na mengine, tunatarajia nyingine inakuja ya aina ile ili iende kwenye maendeleo"
Screenshot_20220428-133302_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia akiwa Uwanja wa Ndege wa KIA akitokea Marekani leo amesema Meya wa Jiji la Dallas nchini Marekani, Eric Johnson, anajipanga kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dallas mpaka Tanzania, hiii ni baada ya kufanya mazungumzo na Mawaziri wa Tanzania waliomuwakilisha Rais Samia ambapo wamekubaliana kuanzisha uhusiano wa kibiashara wa utalii na mawasiliano na Tanzania.

"Tukiwa Marekani kuna kundi lilienda kufanya mazungumzo na Meya wa Dallas (Eric Johnson) na matokeo ya mkutano ule kwamba wenzetu wa Dallas wamekubali na wana hamu wafanye Udugu na Miji yetu ya Tanzania, DSM, Dodoma, Arusha na Miji mingine na tunaangalia uwezekano wa kuwa na Ndege zitakazotoka moja kwa moja kutoka Dallas hadi Tanzania, hiki ni moja ya mambo mazuri tuliyoyavuna"
Screenshot_20220428-133550_OGInsta%2B.jpg
 
Urusi na Marekani zimetangaza kubadilishana Wafungwa licha ya mivutano mikali inayoshuhudiwa baina ya Mataifa hayo mawili yenye nguvu za kijeshi kuhusiana na vita nchini Ukraine.

Urusi imemwachia Mwanajeshi wa zamani wa Marekani Trevor Reed aliyefungwa nchini Urusi mwaka 2020 huku Marekani ikitangaza kumwachia rubani wa kirusi aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.

Rais wa Marekani, Joe Biden amesema ilikuwa jambo gumu kufikia uamuzi huo lakini hiyo ni ishara kuwa utawala wake unatoa kipaumbele katika kuwarejesha nyumbani Wamarekani wanaoshikiliwa kimakosa ughaibuni.

Urusi nayo imesema tukio hilo la kubadilishana Wafungwa ambalo halikutarajiwa ni matokeo ya mchakato mrefu wa mashauriano baina ya Mataifa hayo mawili.
Screenshot_20220428-133726_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama nchini Morocco imemhukumu Mwanaharakati kifungo cha miaka minne jela baada ya kumchukiza Mfalme Mohammed wa sita kwenye mtandao wa kijamii.

Rabie Al Ablaq amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kumkosoa Mfalme mtandaoni, kesi hiyo ilifunguliwa Aprili 11 baada ya kupost mtandaoni video zinazokosoa tofauti za kijamii na ufisadi nchini humo.

Mwanaharakati na Mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 35 pia alipigwa faini ya dirham 20,000 ($2,000).

Human Rights Watch imesema Al Ablaq alitiwa hatiani kutokana na video mbili zilizopostiwa Facebook na YouTube mnamo Septemba na Novemba 2021 ambapo alimzungumzia Mfalme na kulinganisha hali yake binafsi na umaskini ulioenea nchini Morocco.
Screenshot_20220428-133928_OGInsta%2B.jpg
 
Ripoti mpya iliyotolewa na kampuni ya utafiti ya New World na Henley Partners imeitaja nchi ya Tanzania katika nafasi ya saba barani Afrika kwa idadi ya Mamilionea ikiwa na jumla ya Mamilionea 2400.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Tanzania ina jumla ya Mamilionea wa Dola, 2400 kulingana na ripoti ya utajiri ya Afrika 2022 huku ikiwa na Bilionea mmoja tu na kuipiku Kenya, Ghana, Ethiopia, Uganda, Rwanda, Zambia ambazo hazina Bilionea hata mmoja.

Tanzania iko nafasi ya saba barani Afrika kwa idadi ya Mamilionea ikiwa imezidiwa na Afrika Kusini, Misri, Nigeria, Morocco, Kenya na Ghana.
Screenshot_20220428-134144_OGInsta%2B.jpg
 
Ikulu ya Marekani imesema Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amethibitika kuugua Covid 19, Kamala ambaye alishapata chanjo zote kamili zinazohitajika licha ya kukutwa na Corona hana dalili zozote za kuumwa.

Taarifa hiyo ya Ikulu ya Marekani imesema Kamala atajitenga wakati akiendelea kufanya majukumu ya kiofisi kutoka kwenye Makazi ya Makamu wa Rais na atarejea Ikulu akithibitika kuwa hana tena Covid 19.

Ikulu hiyo imesema Harris hajakutana kwa ukaribu na Rais Joe Biden wala Mke wa Rais katika siku za karibuni kutokana na ratiba zao za safari kutofautiana.
Screenshot_20220428-134243_OGInsta%2B.jpg
 
Maafisa wa Afya wa Ulaya wamesema bado hawajagundua chanzo cha ugonjwa wa ajabu wa homa ya ini kwa Watoto, hadi sasa zaidi ya Watoto 190 wanaugua ugonjwa huo ambao asili yake haijulikani na 140 kati yao wapo barani Ulaya.

Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Ulaya, Andrea Ammon, amesema mjini Stockholm kwamba hadi sasa hakuna ushahidi unaoonesha kuwa ugonjwa huo unahusiana na safari za nje ya nchi na kwamba Watoto wanaougua ugonjwa huo wengi wao walikuwa ni wenye afya njema hapo awali.

Ugonjwa huo wa homa ya ini wa aina yake ambao husababisha ini kushindwa kufanya kazi hadi mgonjwa kuhitaji huduma ya upandikizaji umeripotiwa katika nchi za Bara la Ulaya, Israeli na Marekani.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema kifo kimoja kimeripotiwa kuhusiana na mlipuko huo, WHO imesema Watoto wenye umri wa kati ya mwezi 1 na miaka 16 ndio walioripotiwa kupata maradhi hayo, Wataalamu wa afya wanasema ugonjwa huo unaweza kuhusishwa na virusi vinavyosababisha mafua lakini utafiti bado unaendelea.
Screenshot_20220428-134512_OGInsta%2B.jpg
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amelazimika kufuta ratiba ya kazi zake kwa mara ya pili ndani ya muda usiozidi wiki moja kutokana na kupatwa na maumivu ya goti ya mara kwa mara.

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi yake iliyo katika makao makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican, Papa Francis amevunja shughuli zake zote ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye mkutano wa Baraza la Makadinali.

Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 85 pia anasumbuliwa na maumivu ya nyonga yanayomfanya adhoofike, hata hivyo, anatarajiwa kufanya ziara katika nchi kadhaa baadaye mwaka huu, ikiwa pamoja na nchi za Afrika ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.
Screenshot_20220428-134638_OGInsta%2B.jpg
 
WAMBURA: ITAKUWA MAAJABU YANGA WASISHINDE
.
“Pointi 13 ambazo wanazidiana na Simba ni nyingi sana, kuziba pointi hizo ni mechi tatu ama nne Yanga ipoteze na Simba ashinde mechi zote sioni Yanga ikipoteza mitatu, ila bado mechi nyingi lolote linaweza kutokea ila itakuwa maajabu,”
.
“Simba walikuwa bize Kimataifa, huku Yanga wanazidi kujipanga zaidi.” - amesema Michael Wambura.
Screenshot_20220428-141114_OGInsta%2B.jpg
 
FODEN NI HATARI
.
Hakuna mchezaji Muingereza 󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 aliyefunga mabao mengi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na umri wa miaka 21 au chini ya umri huo zaidi ya winga wa Man City, Phil Foden (mabao 9, sawa na Wayne Rooney).
.
Screenshot_20220428-141354_OGInsta%2B.jpg
 
WAAFRIKA WENYE MABAO MENGI UCL
.
Didier Drogba — 14
Sadio Mane — 14
.
Sadio Mane amefunga Bao lake la 14 katika mashindano ya UEFA Champions League na sasa ameifikia rekodi ya gwiji Didier Drogba kama Mwafrika mwenye mabao mengi katika historia ya mashindano ya UCL.
Screenshot_20220428-141600_OGInsta%2B.jpg
 
MAMELODI MABINGWA MARA 5 MFULULIZO
.
2017/18 — Mamelodi
2018/19 — Mamelodi
2019/20 — Mamelodi
2020/21 — Mamelodi
2021/22 — Mamelodi
.
Klabu ya Mamelodi Sundowns imeweka Rekodi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya TANO mfululizo.
Screenshot_20220428-141704_OGInsta%2B.jpg
 
Mabingwa watetezi wa taji la ligi ya mabingwa Afrika klabu ya Al Ahly kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii imetangaza kuwa Rais wa klabu ya Zamalek SC bwana Mortada Mansour amepewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela nchini Misri kwa kosa la kumtusi na kumchafua mchezaji wa zamani wa soka nchini humo na Rais wa Al Ahly bwana Mahmoud El Khatib Bebo pamoja na familia yake.

Source: Al Ahly.
Screenshot_20220428-142328_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom