

Farhan Jr
Kuna taarifa kutoka Shirikisho la soka barani Afrika kuhusiana na Makocha ambao hawapaswi kukaa kwenye mabenchi ya michuano ya Afrika
Kwenye hayo majina kuna jina la Kocha wa Simba, DIDIER GOMES DA ROSA ikanilazimu kwanza niwasiliane na wajuzi wa mambo kutoka CAF na ndani ya nchi
Nikaenda kwanza kwenye page ya CAF kujiridhisha kama taarifa ni sahihi? YES ni kweli ipo pale na ni sahihi kabisa bila shaka
Nikamcheck Mtu wa karibu na Klabu ya Simba kutaka kujua kama taarifa hiyo wameipokea! Akanijibu YES taarifa hiyo ipo, ni sahihi
Kwakuwa FARHAN wa Morogoro sio mbobezi sana wa masuala haya ya Ukufunzi nikalazimika kumtafuta Mwandishi nguli barani Afrika anipe uzoefu wake
Swali langu la kwanza kwake! Kocha GOMES ANA UEFA A! Kwanini CAF hawaitambui na wanataka CAF A? Utofauti ni upi?
Akaniambia Mdogo wangu UEFA A zamani ilikuwa kubwa ila baada ya ujio wa UEFA PRO LICENCE, hii UEFA A kwa Afrika ni sawa na CAF B! Ambayo ilitolewa Morogoro miezi kadhaa nyuma, Matola akiwemo (CAF B) kumaanisha kwamba hakuna Kocha wao mwenye vigezo kwasasa
Nikamuuliza Simba wanapaswa kufanya nini? Akanijibu kuwa cha kwanza wanaweza kumleta Kocha mwenye CAF A kama Thierry Hitimana ambae wanafahamiana vyema, anaweza kupewa mikoba kisha yeye akawa kivuli (Assistant Coach)
Ama plan B ni kuwa Gomes anapaswa kuondoka kwakuwa CAF walishatoa taarifa hii mwaka mzima sasa! Na Makocha wengi walienda kusoma wakiwemo wakina Gavin Hunt wa Afrika Kusini, uwezekano ni mdogo wa CAF kulegeza
Akanambia Makocha wengi Vijana ndio wana CAF A na UEFA PRO LICENCE kama Sundey Oliseh, Benny McCarthy, Sven Van Der Broek! Ila wengi wazee na ambao wapo Afrika kwa muda mrefu hawana
Nikamuuliza kuna shida yoyote kati ya UEFA na CAF? Akanijibu YES! Maana UEFA hawatambui CAF A kama Kocha anaweza kufundisha, hivyo na CAF hawatambui UEFA A kama unaweza kufundisha
Mwisho nikamuuliza unaona Kocha gani anafaa? Kiutani tu akanambia yule Sven wenu ana UEFA PRO LICENCE, mrudisheni bwana Basi tukamalizana hivyo