Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210909-084748_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210909-084807_Opera%20Mini.jpg
 
Farhan Jr

Mkataba wa Djuma Shaban ulikuwa unaenda mpaka Agosti 31 pale AS VITA, wala hakukuwa na shida ya yeye kusaini Yanga na wala hakuna shida kwa Vita kugoma kutoa ITC

As per agreements Djuma angeweza kutumika na Vita mpaka Agosti 31 ambayo ni siku ya mwisho ya mkataba wake na Vita, pia Djuma alikuwa ana haki ya kudai mshahara wake pale Vita wa mwezi Agosti kwakuwa ni Mchezaji wao

Mkataba unaendelea kuwa VALID hata kama umesalia sekunde moja tu, kisheria bado ni mali ya Klabu husika!

According to the elders in the village by quoting @michaelmwebe ni kuwa Yanga walipaswa kuwapooza AS VITA ili watoe ITC kwa haraka hata kama Djuma Shaban 'Soda ya Bemba' alikuwa anamalizia tu muda wake

Kupoozana! Wananchi obviously hawakutaka kuwapooza! Per the elders in the village





Screenshot_20210909-101654_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Kupitia mitandao yake ya Kijamii, Bernard Morrison wa Simba amepost kuwa atatumia jina la Mama yake kwenye jezi yake, EFUA MORRIS kwa heshma yake

Kuweka majina kwenye jezi mfano kwa England walianza rasmi 1993 huku wakianza kwa sheria ngumu ikiwa ni lazima jina la ukoo (surname litumike)

Hii iliwapa tabu mtu kama Jordi Cruyff mtoto wa Johann Cruyff alietaka kucheza nje ya kivuli cha Babake pale Manchester United, akihitaji jezi yake iandikwe tu JORDI, ijapo baadae sheria zikalegezwa

Kwenye mabadiliko ya sheria duniani kuhusu majina kwenye jezi yakaleta matumizi ya Majina ya utani (nicknames) na mengineyo (other names)

Sasa nini vigezo vya majina kwenye jezi kwa wachezaji?

Mosi! Jezi ya Mchezaji inapaswa kuwa na majina yake eidha lake au mzazi, ukoo! Ama jina lolote lile, ambayo yameidhinishwa na bodi ya Ligi, kwa hapa kwetu ni TPLB

Ikumbukwe Klabu yake itajaza fomu maalum yenye majina ya wachezaji, namba zao za jezi na majina mengine, ambayo mchezaji ataandika, iwapo TPLB wataridhia kuwa halina shida kimaadili basi linapita, haswa matusi

Na hapo kwenye majina mengineyo yanaweza hata kuwa ya utani kama vile GAUCHO, NADO, BABI, MACHEJO au SURE BOY kwa kadri Mchezaji anavyojisikia yeye, mfano hayo yamewahi kutumika nchini

Pia katika kupitisha hayo majina mpaka kigezo cha mahusiano ya kifamilia haswa wazazi yanaweza kuchagiza mabadiliko mfano Ravel Morrison kama mnamkumbuka au Nuno Gomez wa Ureno, ama Dele Alli

Hivyo Morrison anaweza kutumia jina la Mama yake bila tatizo lolote, baada ya Bodi ya Ligi (TPLB) kuridhia kuwa hakuna shida kabisa, hiyo ipo duniani kote kama ilivyo kwa CHICHARITO au KUN AGUERO

EFUA MORRIS ! Ready for PREMIER LEAGUE
Screenshot_20210909-101851_Instagram.jpg
 
Wafungwa 41 wamefariki katika ajali ya moto iliyotokea kwenye gereza moja lililokuwa na idadi kubwa ya Wafungwa katika jimbo la Banten nchini Indonesia.

Moto huo ulizuka wakati Wafungwa wengi walipokuwa wamelala usiku wa saa nane kasoro ambapo japo Walinzi walijaribu kufungua milango lakini ilishindikana kutokana na moto kuwa mkubwa.

Kwa jumla walikuwepo Wafungwa 122 kwenye sehemu iliyopaswa kuwa na Wafungwa 40 ambapo mmoja wa Wafungwa waliofariki ni Raia wa South Africa huku Watu wengine 80 wakijeruhiwa.
Screenshot_20210909-131501_Instagram.jpg
 
UNAAMBIWA

Hili ni moja ya Magereza ya Nchini Bolivia ambalo Wafungwa wameanzisha Jamii yao na wanaweza kujisimamia wao wenyewe hakuna Askari anayewalinda au kuwasimamia ndani ya Gereza.

Wafungwa wanafanya uchaguzi Wao wenyewe na kuchagua Viongozi wao, wanatunga sheria na kanuni zao, wanatafuta pia kazi za kufanya ili kuendesha maisha na kulipia pango ya Gereza na wanaruhusiwa hata kupeleka Familia zao na kuishi nazo Gerezani, yaani kama una Mke, Mume au Mpenzi wako amefungwa unaweza kuamua tu na wewe kuhamia zako Gerezani ukaishi nae hadi siku akiachiwa huru mnarudi wote Uraiani.
Screenshot_20210909-131704_Instagram.jpg
Screenshot_20210909-131727_Instagram.jpg
Screenshot_20210909-131745_Instagram.jpg
Screenshot_20210909-131804_Instagram.jpg
Screenshot_20210909-131826_Instagram.jpg
 
UNAAMBIWA

Huko Madrid Hispania kuna shindano hufanyika ambapo Washiriki hutakiwa kuonesha uwezo wao wa kuupata usingizi kwa lazima ndani ya dakika 20 na kuhakikisha Mtu anapata usingizi mzito ili aibuke Mshindi, Washindi huzawadiwa pesa taslimu na zawadi nyingine.

Waandaaji wa shindano hilo wanasema lengo lao ni kukuza uelewa kwa Watu kuhusu umuhimu wa usingizi na kuonesha wale wanaofanya kazi sana hadi wanasahau kupumzisha akili kuwa inawezekana kabisa Mtu kujilazimisha kupata usingizi kwa saa kadhaa kwa faida ya afya ya mwili na akili.
Screenshot_20210909-132037_Instagram.jpg
 
Masule Cosmas (05) amefariki dunia baada ya kujeruhiwa na fisi wakati akiwa machungani na wenzake na baadhi ya viungo vyake kuliwa na mnyama huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea leo Alhamisi Agosti 09, 2021 katika Kijiji cha Mwamang'ori wilayani Maswa mkoani hapa.

Kamanda Abwao amesema kuwa mtoto huyo alikuwa na wenzake wawili wakiwa wanachunga ng'ombe na mbuzi katika mashamba ambayo yapo mbali kidogo na makazi yao.

"Fisi huyo alitokea kwenye kichaka na kuanza kuwakimbiza na alifanikiwa kumkamata na kuanza kula baadhi ya viungo vya mwili, ambavyo ni shavu la kulia, na kumtoa ngozi yote ya kichwa na macho yote mawili."

Abwao amesema kuwa wananchi walimtafuta fisi huyo na baada ya kumpata walimuua, mwili wa mtoto huyo umefanyiwa uchunguzi na daktari na baadae kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Pia jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa watoto wao dhidi ya wanyama wakali.
Screenshot_20210909-132538_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametoa wiki moja kwa wamachinga wanaofanya biashara kwenye njia za watembea kwa miguu kuondoka na kuagiza wakuu wa wilaya kuratibu maeneo ya kufanyia biashara zao.
Screenshot_20210909-132749_Instagram.jpg
 
"Nimeshiriki kuandaa makala ya Tanzania itakayorushwa katika kipindi maarufu Duniani cha Royal Tour. Ni matarajio yangu kuwa makala hii itasaidia kuitangaza vizuri nchi yetu, kuinua utalii, kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji na kuondoa upotoshaji wa makusudi kuhusu Tanzania," ameandika Rais Samia Suluhu Hassan
Screenshot_20210909-132916_Instagram.jpg
 
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 amekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Tabora.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika nyumba ya kulala wageni ya Uyowa.

Nyumba hiyo ipo jirani kabisa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete.

Amesema chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana na kwamba huenda siku zake zilikuwa zimefika.

"Mtu anakufa mahali popote siku zake zikifika na huyu huenda siku zake zilikuwa zimefika, hata hivyo uchunguzi wa chanzo cha kifo chake kutoka kwa madaktari, utaeleza chanzo,"amesema.

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Kitete kwa uchunguzi.
Screenshot_20210909-133422_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kati ya mahabusu 16 waliotoroka kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai, Mbagala wilayani Temeke, wanne tayari wamekamatwa.

Septemba 4, mwaka huu Mwananchi liliripoti kutoroka kwa watuhumiwa hao waliokuwa wamehifadhiwa katika kituo hicho baada ya kumpiga askari kisha kuvunja mlango wa chumba cha mahabusu na kukimbia.

Akizungumza jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema jeshi hilo linaendelea kuwasaka waliosalia na kuongeza kuwa lazima watakamatwa wote.

“Nasema hivi, hadi sasa mahabusu wanne wameshapatikana, tunaendelea kuwatafuta wengine 12 ambao hawana sehemu ya kukimbilia, wote watakamatwa tu,” alisema Kamanda Muliro.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita saa 1:30 usiku katika kituo hicho.
Screenshot_20210909-133758_Instagram.jpg
 
Zikiwa zimepita siku 15 tangu Hamza Mohammed (30) auawe, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema upelelezi wa kina hadi nje ya nchi unaendelea kufanyika dhidi ya tukio hilo.

Hamza aliuawa Agosti 25 mwaka huu nje ya geti la Ubalozi wa Ufaransa katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, baada kufanya shambulio la kurusha risasi na kuua askari wanne, akiwamo mmoja wa kampuni ya ulinzi na kujeruhi wengine sita. Muliro alisema upelelezi huo unafanyika ndani na nje ya familia.

Pia, alisema wanafanya upelelezi mwingine ndani na nje ya nchi, licha ya ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kudai kuwa upelelezi umebaini Hamza alikuwa ni gaidi wa kujitoa mhanga.

Kamanda Muliro alisema hayo alipozungumza na Mwananchi jana muda mfupi baada ya ndugu wa karibu wa Hamza kuiambia Mwananchi kuwa watu watano waliokuwa wanashikiliwa na polisi bado hawajaachiwa.
Screenshot_20210909-133918_Instagram.jpg
 
Taliban, kwa msaada wa moja kwa moja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Pakistan iliyoongozwa na Jenerali Babar, ilifaidika na ile hali ya kukosekana kwa uongozi wa kitaifa nchini Afghanistan na kuleta asilimia 80 ya nchi chini ya udhibiti wao.

Lakini baada ya hapo, zile ahadi za Taliban za amani na haki zilipotea, zikibadilishwa na sera zao kali na ukatili dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa na dhidi ya wale ambao si wapinzani wao, lakini wana siasa za wastani.

Ubaguzi wao wa kijinsia na wa kikabila, wa kidini, ukiukaji wa haki za kimataifa za binadamu na uharibifu wa urithi wa kihistoria, ulimvuruga karibu kila mtu katika jamii za watu wa Afghanistan katika maeneo yanayodhibitiwa na Taliban.

Ingawa waliondolewa madarakani mwishoni mwa mwaka 2001 baada ya uvamizi wa kijeshi wa Marekani mara baada ya Septemba 11, miaka 20 baadaye wamerejea tena madarakani kama walivyoingia.

Kwa undani wa makala hii jipatie nakala yako ya Mwananchi au tembelea tovuti yetu.
Screenshot_20210909-134409_Instagram.jpg
 
KOCHA SIMBA NGOMA NGUMU

Shirikisho la soka Afrika, limetoa orodha ya Makocha ambao hawaruhusuwi kukaa kwenye bench la timu zao, kutokana na kukosa vigezo vya CAF A au UEFA PRO LICENCE

Didier Gomes (UEFA A Diploma) Simba SC

Erradi Mohamed Adil (UEFA Advanced Diploma) APR

Bosa Wasswa (CAF B) Express FC (To be replaced)

Diego Garzitto (UEFA A) El Merreich SC

Comlan Mathias (German License) ESAE FC

Pascal Lafleurial (UEFA Elite Youth A) DFCB

Roque Sapir (CAF C Diploma) GD Sagrada Esperança

Ame Khamis (CAF B) () KMKM

Abalo Jean-Paul (UEFA A) ASKO
Screenshot_20210910-044010_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom